FEDHA: Hivi Ndivyo Unavyoweza Kumudu Kujiongezea Kipato Chako Kwa Kutumia Njia Hizi Rahisi.

Ni ukweli usiopingika pesa ni kitu muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Wengi wetu tunalijua hili kwa kuwa bila pesa hakuna kitu kinachoweza kuwezekana katika maisha. Tunahitaji pesa zitusaidie katika mahitaji yetu ya kila siku, hapa ndipo umuhimu wa pesa unapokuja na kuonekana ya thamani sana siku hadi siku katika maisha ya mwanadamu.
 

Kutokana na umuhimu huu wa pesa kwetu, kuwa ndiyo kitu pekee kinachoweza kuongoza maisha yetu na kutufanya tujisikie huru zaidi hasa pale tunapokuwa nazo, hatuna budi kuwa nazo kwa kadri tunavyoweza, kwani ni sehemu ya maisha yetu na ni lazima tuzipate ili zitusaidie kuendesha maisha yetu na hatimaye kutufikisha katika mipango na malengo yetu tuliyojiwekea.
Na ili tuweze kumudu hili la kuwa na pesa za kutosha ambazo zitasaidia kumudu na kendesha maisha yetu kwa ufasaha, tunalazimika kuwa na njia mbadala za kutengeneza kipato cha ziada mbali na kile tunachokipata kutokana na kazi tunazozifanya sasa. Utawezaje kumudu kujiongezea kipato chako, ili kikusaidie kukabiliana na changamoto za maisha za kila siku? 

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kumudu Kujiongezea Kipato Chako Kwa Kutumia Njia Hizi Rahisi:-
1. Kuwa na mipango na malengo.
Hakikisha unajiwekea malengo mazuri ya kuweza kutimiza kile kipato unachotaka uwe nacho baada ya muda Fulani. Anza kuweka mipango taratibu na ujue nini cha kufanya ili kutimiza malengo yako. Kama unataka kufungua biashara Fulani na unaona pengine huna mtaji, unaweza ukaanza kuweka pesa kidogo kidogo mpaka ukafikisha lengo. Ukiwa na mipango na malengo, hiyo itakusaidia kuelekea kwenye kuongeza kipato chako.( Soma Pia Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutajirika Kwa Kuanza Na Shilingi Elfu Moja )

2. Chukua hatua kwa vitendo.
Acha kufikiria tu juu ya kuongeza kipato chako, chukua hatua kwa vitendo. Kama una majukumu ulitakiwa kuyafanya kwa siku, wiki au mwezi anza kuyatekeleza, hakikisha unayafanya na acha tabia ya kuairisha mambo. Ukichukua hatua juu ya mipango yako, hata kama ni kwa kidogo kidogo, utajikuta unasogea na mwisho wa siku utaona lengo lako la kuongeza kipato linaonekana na kuwa la kweli.
3. Jifunze kuishi na watu waliofanikiwa.
Kama ukiishi na watu waliofanikiwa na kujua nini hasa wanachokifanya hadi kufanikiwa itakusaidia wewe kutimiza ndoto zako juu ya kile unachokitafuta hususani uhuru wa kipesa na hatimaye kuweza kuongeza kipato chako. Kupitia wao utajinza mbinu na njia walizotumia na wanazotumia mpaka sasa kuweza kuongeza kipato chao siku hadi siku. Ukiweza kufanya hivi hii itakusaidia wewe kujenga uwezo wako wa kuongeza kipato zaidi.
4. Jifunze kuwa kiongozi wa maisha yako wewe mwenyewe.
Kati ya vitu vitakavyokufanya uishi maisha magumu na ambayo yatakunyima uhuru mkubwa wa kifedha ni kutokuendelea kuishi kama kiongozi. Unapoishi kama kiongozi unakuwa wewe ndiye mwamuzi na hakimu wa maisha kuwa unataka yaweje. Watu wengi wanaishi maisha magumu kwa sababu ya kutegemea watu wengine wawe viongozi wa maisha yao. Ni watu wa kukaa chini kusubiri mishahara ipande nayo haipandi. Ukiishi kama kiongozi wewe ndiye utakaye amua baada ya muda ufanye nini cha kuweza kukuongezea kipato zaidi.
5. Jifunze kutumia muda wako vizuri.
Haijalishi unaishi maisha ya aina gani muda ulionao wewe ni masaa 24 tu kwa siku. Je, katika muda huu wa saa 24 unanufaika nao vipi au unaupoteza tu bila sababu. Muda ni kitu cha muhimu sana katika kufanikisha na kukamilisha ndoto zako unazozitaka. Kama unataka kufikia uhuru wa kipesa na kuweza kuongeza kipato chako jifunze kutumia muda wako vizuri. Kwa kila dakika unayopata itumie vizuri ili ikuzalishie kile unachohitaji, vinginevyo utakuwa hufanyi kitu kama wewe ni mtu wa kupoteza muda tu.( Unaweza Ukasoma pia Jinsi Unavyoweza Kutumia Muda Muda Mchache Kufanya Mabadiliko Makubwa Na Endelevu Katika Maisha )
6. Jaribu kufanya kitu kipya.
Kama vitu ulivyokuwa ukivifanya havijaweza kukuletea matunda unayotaka, jaribu kufanya vitu vipya. Acha kung’ang’ania kufanya mambo yaleyale ambayo hayana uwezo wa kubadili maisha yako. Upo hivyo ulivyo kwa sababu ya kufanya mambo yaleyale siku zote. Chukua hatua juu ya maisha na kubali kubadilika, utaona matokeo ya kipato chako kuongezeka.
Hivyo ndivyo unavyoweza kumudu kujiongezea kipato kwa kutumia njia hizo rahisi.
Nakutakia ushindi katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea mtandao huu wa AMKA MTANZANIA kwa kujifunza mambo mengi yatakayobadili maisha yako.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE.
IMANI NGWANGWALU
0713 04 80 35/ingwangwalu@gmail.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: