Mwaka huu 2015 ni mwaka wa kusema hapana kwa VITU VIZURI ili uweze kupata VITU BORA. Kila mmoja wetu anapenda kupata kilicho bora lakini ni wachache sana wanaoweza kufikia lengo hilo. Hii ni kwa sababu watu wengi tumejikuta tukisema ndio kwa kila kitu na hatimaye tunashindwa kupata nafasi ya kuweka vile vilivyo muhimu.

Wahenga wanasema ukikimbiza sungura wawili utaishia kukosa wote, na ukilenga kundi la ndege utaishia patupu. Ni heri uamue kumkimbiza sungura mmoja na kama ukifanya juhudi utamkamata. Vile vile ni bora kumlenga ndege mmoja kwenye kundi la ndege 100 utakuwa na uhakika wa kumpata na kama mambo yakiwa mazuri unaweza kupata na ndege mwingine wa pili.

Kwa hiyo kufanya mambo machache ambayo unaweza kuwa bora ndio lengo lako kuu mwaka huu 2015. Na kusema hapana kwenye mambo mengine yasiyo ya msingi ni hatua muhimu ili kuweza kuboresha maisha yako mwaka huu 2015.

Yafuatayo ni mambo 30 unayotakiwa kusema HAPANA kwa mwaka huu 2015.

1. Sema hapana kwa uvivu.

2. Sema hapana kwa tabia ya kuahirisha mambo.

3. Sema hapana kwa tabia ya kufuata mkumbo.

4. Sema hapana kwa tabia ya kulalamika.

5. Sema hapana kwa tabia ya kutoa au kupokea rushwa.

6. Sema hapana kwa tabia ya kutokujiwekea akiba.

7. Sema hapana kwa mahusiano ambayo hayakujengi.

8. Sema hapana kwa vipindi vya tv vinavyokupotezea muda.

9. Sema hapana kwa tabia ya kutegemea wengine ndio wabadili maisha yako.

10. Sema hapana kwa tabia ya kukwepa majukumu yako.

11. Sema hapana kwa tabia ya kutafuta njia ya mkato ya kupata mafanikio.

12. Sema hapana kwa tabia ya kutegemea kupata vitu vya bure.

13. Sema hapana kwa tabia ya kusengenya wengine, kupika majungu.

14. Sema hapana kwa tabia ya kufikiri hakuna fursa.

15. Sema hapana kwa imani kwamba wewe huna bahati.

16. Sema hapana kwa imani kwamba wenye fedha wana roho mbaya.

17. Sema hapana kwa kazi ambayo unaifanya lakini huipendi.

18. Sema hapana kwa biashara ambayo unaifanya lakini inakusumbua.

19. Sema hapana kwa ulevi.

20. Sema hapana kwa tabia ya kufuatilia maisha ya wengine.

21. Sema hapana kwa tabia ya kufanya mambo kwa mazoea.

23. Sema hapana kwa kwa hofu zinazokuzuia kufanya mambo makubwa.

24. Sema hapana kwa tabia ya kutokujiamini.

25. Sema hapana kwa kuendelea kuwa wa kawaida.

26. Sema hapana kwa tabia ya kupoteza muda muda kwenye mitandao.

27. Sema hapana kwa tabia ya kukosa uaminifu.

28. Sema hapana kwa tabia ya kunyanyasa au kukandamiza wengine.

29. Sema hapana kwa tabia ya kufikiri kwamba kuna uhaba wa fedha.

30. Sema hapana kwa tabia ya kuanza mambo na kuishia katikati.

Kuna mambo mengi sana, zaidi ya 100 ya wewe kusema hapana ili uweze kuboresha maisha yako. Anza na mambo hayo 30 na baadae utaendelea kuongeza mengine kadiri utakavyofanikiwa kuachana na hayo.

Kumbuka pia huu ni mwaka wa JUST DO IT, yaani kama kuna chochote unataka kufanya ANZA KUFANYA SASA. Hivyo unaposema unaacha tabia fulani iache sasa, mara moja na hakuna kujibembeleza.

Nakutakia kila la kheri kwenye kuufanya mwka 2015 kuwa mwaka wa mabadiliko kwenye maisha yako.

TUPO PAMOJA,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

kitabu-kava-tangazo4322