Mambo 5 Yanayoashiria Kuwa Hutaki Mafanikio.

Kila mtu huwa ana nia ya kufanikiwa na kufikia maisha bora yenye hadhi ya kuitwa maisha, na siyo bora maisha. Hili ndilo hitaji la msingi ambalo kila binadamu anayetaka mafanikio analo na kutamani kuona mafanikio makubwa yanatokea katika maisha yake. Wengi wetu huwa tunafanya kila linalowezekana ili kufanikiwa, hii yote huwa inaonyesha wengi  tunapenda kufanikiwa,hata wewe unapenda kufanikiwa, hata mimi pia napenda kufanikiwa kama ulivyo wewe. Lakini swali la msingi ni kwamba je, ni kweli unayataka mafanikio unayoyatafuta? Je, ni kweli una nia thabiti ya kufikia lengo na mafanikio makubwa unayohitaji?

Wengi wetu ingawa huwa ni watu wa kujishughulisha na kutafuta mafanikio tunayoyataka lakini wakati mwingine huwa ni watu wa kujidanganya sisi wenyewe bila kujua. Huwa ni watu wakufikiri tunatafuta mafanikio kumbe kiukweli tunakuwa tupo tayari mbali na mafanikio. Kuna usemi unaosema, vitendo vinaongea zaidi kuliko maneno ndivyo ilivyo hata kwenye maisha yako. Unaweza ukawa unaona kama unatafuta mafanikio kumbe upo nje na mafanikio unayoyatafuta kutokana na nia uliyonayo. Kitu gani kitakachoashiria kuwa huna nia thabiti ya mafanikio unayoyataka?

Haya Ndiyo Mambo Yanayoashiria Ya Kuwa Hutaki Mafanikio Katika Maisha Yako:-

1. Kuahirisha mipango.
Wote wanaopanga mipango na kuiahirisha kwa sababu zisizo za msingi ni dalili tosha kwamba hawana nia thabiti ya kufikia malengo hayo na kufanikiwa. Kwa jinsi unavyozidi kuairisha mipango yako ndivyo ambavyo unazidi kujichelewesha kufikia kwenye mafanikio. Hii ni tabia sugu ambayo watu wengi wanayo na mara kwa mara wamekuwa wakijikuta ni watu wa kuairisha mambo tu katika maisha yao na kujikuta kushindwa kufanikisha kitu chochote. Kama una nia thabiti ya kufanikikiwa basi epuka kuweka mipango kuiahirisha bila sababu za msingi.

Mara nyingi watu wasio na nia thabiti ya kufanikiwa katika shughuli zao mara nyingi huwa hawana bidii katika shughuli zao. Huwa ni watu wakufanya kazi kwa uvivu kana kwamba hizo kazi si zao wanawafanyia watu wengine bila malipo. Unatakiwa kujua kuwa ili uweze kufikia viwango vya juu vya mafanikio katika maisha yako unatakiwa kujituma na kufanya kazi kwa bidii zote. Hili ni jambo ambalo liko wazi kabisa, una nia ya kufanikiwa katika mipango yako epuka kuwa mvivu katika kazi zako. Jitume siku zote bila kuacha.

3. Kutokuthamini kazi.
Siku zote watu wasio na nia thabiti ya kufanikiwa hawathamini kazi zao.Wako tayari kuacha ofisi au kazi na kwenda kufanya mambo mengine yasiyo na tija, kwa mfano mtu anaweza  kufunga duka na kwenda kuanglia mpira ambao yeyé mwenyewe hanufaiki nao hata kidogo zaidi ya kupoteza muda na pesa. Mtu mwingine hujikuta yeyé ni wa kuchelewa tu kufika kazini kwake  karibu kila siku kwa sababu zisizo za msingi na anapofika kazini pia anakua bado hatulii kuzingatia kazi ile anayoifanya. Kama unaishi maisha haya na unadai unatafuta mafanikio, unajidanganya.

4. Kukata tamaa mapema.

Kukata tamaa ni dalili nyingine ya kutokuwa na nia thabiti ya kufanikiwa katika maisha. Mafanikio hayaji bila kuwepo na juhudi za makusudi na hakuna mafanikio ya kirahisi rahisi tu. Shetani mwenyewe hakati tamaa anapokuwa anashughulika na wanadamu,inakuwaje wewe unakata tamaa?  Kama ndani mwako unajisikia kukata tamaa kutokana na jambo unalolifanya elewa unajiweka katika wakati mgumu wa kuagana na mashindano ya mafanikio. Tambua kabisa, unapokata tamaa hiyo ni ishara ya kuonyesha kuwa  hutaki mafanikio tena katika maisha yako.
SOMA; Kama unafikiri  umechelewa na umekosea sana  katika maisha yako.    
                                                                                   
5. Kutokutulia katika maisha yako.
Kuna watu ambao huanzisha mradi na kuacha na kuanzisha mwingine na kuacha,hawatulii na mradi mmoja  kwa muda wa kutosha ili kuona kama watafanikiwa au la.Hii ni dalili ya kutokuwa na nia thabiti ya mafanikio yako.Mtu mwenye nia thabiti ya kufanikiwa huanzisha mradi na kujipa muda wa kutosha kushughulikia mradi huo.Baada ya kuufanyia kazi mradi huu kwa muda mrefu na kujiridhisha kwamba haumpi maslahi ya kutosha huamua kubadili mradi.Kumbuka kuwa,hatubadili miradi kiholela tu,tunabadili pale tunapojiridhisha kwamba miradi hailipi kwa wakati huo na eneo husika,kweli haina maslahi.Ukitaka kufanikiwa epuka kosa hili.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea mtandao huu wa AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA kwa kupata maarifa bora yatakayobadili maisha yako.

Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza na kuhamasika zaidi.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,


IMANI NGWANGWALU,


0767 048 035/dirayamafanikio.blogspot.com


0713 048 035/ingwangwalu@gmail.com


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: