KITABU; Tofauti Kumi Kati Ya Waliofanikiwa Na Walalamikaji.

Mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA karibu kwenye mwaka mwingine wa kujisomea vitabu ili kuongeza maarifa zaidi. Mwaka jana kila mwezi ulitumiwa kitabu kimoja cha kujisomea. Na mwaka huu kwa miezi kumi nambili ijayo utatumiwa vitabu kumi na mbili ambavyo kama utavisoma vitabadili maisha yako kwa kiwango kikubwa.

WINNERS

Kama bado hujajijengea tabia hii ya kujisomea, kuweza tu kusoma kitabu kimoja kila mwezi na ukafikisha vitabu 12 kwa mwaka utakuwa na maarifa mengi kukiko asilimia 90 ya watanzania wote. Hii ni kweli kabisa kwa sababu watanzania wengi, wakishahitimu masomo yao, wanaona kusoma ndio mwisho, wanasahau kwamba ndio mwanzo tu.

SOMA; Wajasiriamali Wenye Mafanikio Hufanya Mambo Haya Matano Kila Siku.

 

Kama unaweza kusoma vitabu 12 vijavyo hongera sana, kama unaweza kusoma zaidi ya hapo nakukaribisha kwenye VORACIOUS READERS ambapo utaweza kusoma vitabu vingi zaidi. Kwa mfano mimi kwa mwezi huu wa kwanza mpaka leo nimeshazoma vitabu kumi na kwa mwaka mzima nimepanga kusoma vitabu 150. Ni kitu ambacho kinawezekana kama ukiweka vipaumbele vyako vizuri.

Mwezi huu wa kwanz akabisa naanza na kukushirikisha kitabu ambacho kitakufanya utengeneze uelekeo mzuri kwa mwaka huu 2015. Kitabu hiki kinatupatia tofauti kumi kati ya watu waliofanikiwa(washindi) na wanaolalamika(washindwa). Moja ya vitu ambavyo nimejifunza kwenye maisha mpaka sasa ni kwamba huwezi kuwa na mafanikio na kuwa mlalamikaji kwa wakati mmoja. Ukishakuwa mlalamikaji maana yake unakuwa sio mtu wa kuchukua hatua.

SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

 

Watu wote wenye mafanikio sio watu wa kulalamika au kulaumu. Kama kuna kitu hawakipendi wanakibadilisha, kama hawawezi kukibadilisha wanaachana nacho na kufanya kingine wanachoweza kukisimamia vizuri. Kwa mfano mtu aliyeshindwa anaweza kuanza kulalamikia kukosa elimu, kukosa mtaji, kutokea familia masikini, kuwa na bahati mbaya na kadhalika. Kwa kulalamika huko anajiridhisha kwamba hawezi kutoka hapo alipo kwa sababu vitu hivyo ndio vinavyomzuia. Kwa bahati mbaya anapolalamika hakuna kinachobadilika na hivyo anabaki pale alipo kwa maisha yake yote.

Watu waliofanikiwa wao sio watu wa kulalamika, kama kuna kitu ambacho kinawazuia kufanya wanachotaka wanaangalia jinsi ya kukabiliana nacho na kama hawawezi wanaangalia kingine cha kufanya. Kwa mfano kama anaona hana elimu ya kutosha, anajifunza, kama hana mtaji, anatafuta pa kuanzia kidogo kidogo.

SOMA; Hii Ni Kazi Yenye Malipo Makubwa Sana Ambayo Unaweza Kujifunza Kuifanya

 

Tofauti hizi mbili tu za kimtizamo zinaleta mabadiliko makubwa sana kwenye mafanikio ya kimaisha na hata furaha kwenye maisha. Mtu anayelalamika tu ni vigumu sana kufurahia maisha yake. Hii ni kwa sababu anaona kama kila kitu kinachotokea kwenye maisha yake kimekuja kumharibia maisha yake. Watu wasiolalamika, wanaochukua hatua, hufurahia maisha yao katika kila hali kwa sababu wanajua chochote kitakachotokea wanaweza kukabiliana nacho.

Katika kitabu hiki utajifunza kwa urahisi sana tofauti kumi za washindi na walalamikaji na utajua ni hatua gani ya kuchukua kwenye maisha yako.

Natamani sana wewe mtanzania mwenzangu uache kulalamika mwak ahuu 2015 na uanze kuchukua hatua. Na kusihi sana usome kitabu hiki na utekeleze yale uliyojifunza kwenye maisha yako.

Kitabu hiki ni cha kiingereza na ni kifupi sana, utaweza kukidownload(pakua) na kukisoma kwenye kompyuta au simu yenye uwezo wa kusoma vitabu. Ni kitabu kifupi na hakichoshi kusoma.

Kupata kitabu hiko bonyeza maandishi haya ya kitabu; Top 10 Distinctions between Winners and Whiners.

Anza kukisoma leo na uboreshe maisha yako kwa mwaka huu 2015.

Ongeza maarifa na tumia maarifa hayo kuboresha maisha yako.

Nakutakia kila la kheri katika harakati zako za kuboresha maisha yako.

TUPO PAMOJA.

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

SOMA; Okoa Muda Huu Muhimu Ambao Unaupoteza Kila Siku Na Kukuchelewesha Kufikia Mafanikio.

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: