Kama Umeshaweka Malengo Ya Mwaka Huu Karibu Hapa Upate Msaada Wa Kuyafikia.

Kama umeshaweka malengo ya mwaka huu 2015 hongera sana, maana hiyo ndio hatua ya kwanza na muhimu sana ya kuweza kufikia malengo yako na hata kufikia mafanikio makubwa.

Kama hujaweka malengo yoyote kwa mwaka huu 2015 ishia tu hapa na usiendelee kusoma maana utakayosoma hapa hayatakusaidia. Badala yake fungua makala hii na hii na hii ambazo zitakuwezesha wewe kuweka malengo ya maisha yako.

Kwa wale ambao tayari mmeshaweka malengo tunaweza kuendelea.

Mpaka sasa unajua ya kwamba kuweka malengo tu ni hatua ya kwanza kuyafikia, ila sio uhakika kwamba utayafikia. Utakuwa shahidi mzuri kwenye hili kwa sababu kwa miaka mingi umekuwa unaweka malengo ambayo huwa huyafikii. Na mwaka huu pia umeweka malengo ambayo kwa sehemu kubwa unaweza usiyafikie.

SOMA; Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.

 

Najua vizuri na hasa kwa mazingira yetu ya kitanzania, miezi mitatu baada ya kuweka malengo yako, utakuwa umeshasahau karibu kila kitu na utakuwa umerudi kwenye maisha yako ya kawaida. Hii inatokana na kwamba utaendelea kuzungukwa na watu wale wale ambao hawaoni umuhimu mkubwa wa kuweka malengo na kuyafanyia kazi. Na wakati mwingine unakuwa umezungukwa na matatizo ambayo yanakufanya usahau kuweka kipaumbele kwenye malengo yako.

Itaanza kidogo kidogo na baadae unajikuta umeshasahau kabisa na kukata tama.

Pia ni rahisi sana kutokuweka mkazo kwenye malengo yako hasa pale unapokutana na changamoto kwa sababu kama hakuna anayekusimamia kwa karibu unaweza kujiridhisha kwamba haiwezekani.

Ili kukusaidia usifikie katika hali hiyo nimeandaa mpango maalumu wa kukufuatilia wewe na malengo yako. Hii ina maana kwamba mimi nitakuwa nakufuatilia wewe ili kujua unaendeleaje na malengo yako. Kwa njia hii utalazimika kufanya juhudi hata pale ambapo unafikia kukata tama.

Katika mpango huu kila jumamosi ya kwanza ya mwezi kila mwezi utanijulisha kuhusu maendeleao yako katika malengo yako. Baada ya hapo tutajadili changamoto unazopitia na kama kuna mengine muhimu ya kujadili.

Mpango huu utaanza tarehe 01/02/2015 na siku hiyo utanitumia email yenye malengo yako ya mwaka huu 2015. Tutafuatiliana kwa miezi yote mpaka mwaka huu 2015 unaisha.

SOMA; Fanya Mambo Haya Matatu Na Usipokuwa Tajiri Ndani ya miaka 10, sahau kuhusu utajiri kwenye maisha yako.

Gharama ya kujiunga na mpango huu ni tsh elfu thelathini(30,000/=) kwa mwaka mzima na unalipa mara moja tu ndio unaingia kwenye mpango huu. Ili kuhakikisha naweza kuwafuatilia vizuri nafasi zitakuwa chache sana(nafasi 20 tu). Na nafasi hizi zitatolewa kwa anayelipa wa kwanza ndio anapata nafasi. Zikishajaa hakutakuwa na nafasi nyingine tena.

Mwisho wa kujiunga ni tarehe 31/01/2015 lakini kama nafasi zitakuwa zimejaa zoezi litafungwa mapema zaidi. Nafasi hizi ni chache ili mimi niweze kuwahudumia vizuri wale ambao watajiunga na mpango huu.

Mpango huu utakuwa mzuri sana na wale ambao nitafanya nao kazi hii ni lazima uwe kweli umejitoa kufikia malengo yao.

Kama upo tayari kuingia kwenye mpango huu tuma fedha ya ada tsh 30,000/= na email yako kwenye namba 0717396253/0755953887.

Karibu sana kwenye nafasi hii ya mimi na wewe kwenda bega kwa bega mpaka utakapofikia malengo uliyojiwekea mwaka huu 2015.

Kama una nia ya kweli ya kufikia malengo yako kwa mwaka huu 2015 hii ndio fursa muhimu sana kwako kuitumia.

Nakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

TUPO PAMOJA.

kitabu-kava-tangazo4322

 

SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s