Hiki Ndicho Kitu Kinachokuzuia Wewe Kuwa Tajiri.

Mara nyingi ni kitu ambacho umekuwa ukijiuliza na kuumiza kichwa, ‘kwa nini maisha yangu yako hivi, kwa nini mimi ni maskini na kwa nini mimi sina pesa ya kutosha ya kuweza kuendeshea maisha yangu’. Pengine umekuwa ukija na majibu yako kichwani ya kuwa huna pesa na wewe sio tajiri kwa sababu una mkosi ama huna bahati ya kutosha kama hao unaowaona wamefanikiwa wanayo. 

Kitu usichokijua na ambacho na penda kukwambia ni kuwa, hata wale matajiri ambao unawaona kama  wana bahati na pesa nyingi sana hawakuzipata tu mara moja, ni watu ambao walishikilia ndoto zao kikamilifu na kuamini kuwa ipo siku watafanikiwa na kweli wakafanikiwa na kuna wakati walipitia maisha ya kupoteza karibu pesa zote walizokuwa nazo na kuanza upya tena, hadi kufikia mafanikio walipo leo.

Kitu kinachokufanya wewe usiwe tajiri na mafanikio makubwa sio bahati kama ambavyo unafikiria mara kwa mara ni fikra ulizonazo juu ya utajiri na mafanikio kwa ujumla ndizo zinazokufanya ushindwe kufikia mafanikio makubwa na hatimaye kuwa tajiri. Bahati kama bahati haihusiki na mafanikio yako kwa asilimia mia moja umekuwa ukiitumia kama kisingizio tu cha kujitetea na kushindwa kuchukua hatua zaidi juu ya maisha yako.

SOMA: Acha Kuamini Sana JuuYa Kitu Hiki Katika Maisha Yako, Ili Utengeneze Utajiri Mkubwa Ulionao.

Mafanikio yoyote unayotafuta katika maisha yako yanategemea zaidi fikra ama imani uliyonayo kwa kile unachokiamini katika maisha yako. kama unaamini utafanikiwa na kisha ukachukua hatua dhidi ya mafanikio tambua utafanikiwa kweli, lakini unapokuwa na imani hasi juu yamafanikio yako mwenyewe inakuwa ni ngumu sana kuweza kusonga mbele kwa chochote kile unachokuwa unakifanya.

Mara nyingi sana tena sana tu, watu wengi wanashindwa kufanikiwa katika maisha yao na kushindwa kuishi maisha wanayotaka kutokana na kuwa na fikra ama imani hasi kuhusu mafanikio. Wamekuwa ni watu wanaomini hawana pesa ndio maana hawawezi kufanikiwa, lakini hiyo haitoshi wamekuwa watu pia wanaoamini kutoka moyoni kuwa hawana mafanikio kwa sababu ya kukosa bahati kitu ambacho sio kweli hata kidogo.

Kama utaendelea kuwa mtu wa visingizio na kuilaumu bahati kuwa haijakufikia kwanza, elewa kabisa utakuwa unakosea sana na hujitendei haki kwa kuwa unakuwa unajidanganya mwenyewe na pili, tambua kuwa katika maisha yako sahau kabisa suala la kuwa na mafanikio makubwa. Kwa nini nakwambia sahau mafanikio makubwa? ni kwa sababu utakuwa hufanyi chochote kile cha maana dhidi ya maisha zaidi ya kukaa ili na wewe udondokewe na fuko la bahati kama kweli lipo.

SOMA: Kama Unaendelea Kuamini Hivi Katika Maisha Yako, Sahau Kuhusu Mafanikio.

Kuna wakati niliwahi kukutana na rafiki yangu mmoja ambaye katika mazungumzo yetu aliweza kuniambia kuwa unajua ‘Imani nashindwa kufanya biashara kikamilifu kwa sababu sina muda wa kutosha wakusimamia biashara zangu kutokana na kazi nilizonazo pale ofisini.’Hivi ndivyo  watu wengi walivyo wamekuwa ni watu wa kutafuta visingizio hiki na kile ilimradi tu, kitu ambacho ni hatari sana kwa mafanikio yao ya leo na kesho.

Nafikiri katika maisha yako kama sio wewe basi umewahi kusikia mtu anasema sitaki kuwa tajiri sana, nataka kuwa mtu wa kawaida kwa sababu pesa ni shetani, pesa ni mwanaharamu, pesa ni laana kama utakuwa nazo nyingi, haya ni maneno ambayo umewahi kuyasikia sana. Kitu cha kujiuliza kati ya pesa na wewe nani shetani?Mara nyingi sisi ndio huwa mashetani na wanaharamu hasa pale tunapokuwa na pesa kutokana na tabia zetu.

Pesa kama pesa haina ubaya wowote kutokana na imani hasi uliyonayo juu ya pesa umekuwa ukiisingizia sana na ndio maana imekuwa ikikupiga chenga na huipati kutokana na fikra unazoijengea kila siku katika maisha yako. kama unataka uendelee kuwa na maisha magumu siku zote endelea kuwa na fikra hasi nyingi utakwama tu. Unachokihitaji katika maisha yako ni kuwa na mtazamo chanya wa mafanikio yako na si vinginevyo.

Kwa vyovyote vile iwavyo, sababu yoyote ile uliyonayo unayoiona inakuzuia kufikia mafanikio makubwa hiyo ni ishara tosha ya kuwa bado una unafikra ama imani hasi juu ya mafanikio yako. Badala ya kutafuta visingizio kama sina bahati, sina mtaji tafuta njia na suluhu la hivyo vyote ili uanze kuyafata mafanikio makubwa unayoyahitaji katika maisha yako na hatimaye uwe tajiri.

Nakutakia mafanikio mema, kama unahitaji kuifikia haraka safari ya kuelekea kwenye utajiri, nakukaribisha kwenye KISIMA CHA MAARIFA huko utajifunza mengi ya kubadili maisha yako ikiwemo tabia muhimu za watu wenye mafanikio makubwa.

Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kila siku kujifunza na kuhamasika.

IMANI NGWANGWALU,
Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: