Baada Ya Kufanya Maamuzi, Usiangalie Tena Nyuma.

Ili kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha na kwenye chochote unachofanya, unahitaji kufanya mambo mawili.

Jambo la kwanza ni kuamua ni nini hasa unachotaka. Hapa unaamua maisha yako unataka yaweje, unataka kuwa mtu wa aina gani na unataka kuwa na vitu gani. Hii ni hatua ya kwanza na muhimu sana ya wewe kufikia mafanikio. Maana kama hujui unachotaka ni nini utakipataje? Yaani ni sawa na unatembea halafu hujui unakokwenda, utafikaje?

Hatua ya kufanya maamuzi juu ya kile unachotaka kwenye maisha ni muhimu sana na unahitaji kuiheshimu sana.

Jambo la pili ni kulipa gharama, ndio kuna gharama kubwa unatakiwa kulipa ili kuwez akupata kile unachotaka. Mpaka sasa bado hujakipata kwa sababu hujawa tayari kulipa gharama. Na kusingekuwa na gharama, kila mtu angekuwa na kile anachotaka. Ni gharama ndio inawatenganisha wenye kiu hasa ya kufanikiwa na wanaofikiria kufanikiwa kunaweza kutokea tu. Baadhi ya gharama unazotakiwa kulipa ili kupata mafanikio ni kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, kuwa mvumilivu, kujifunza kila siku na kuwasaidia wengine kupata wanachotaka.

Mambo haya mawili nina uhakika unayajua vizuri, maana tumeshayaandikia mara nyingi sana. Na hapa nimerudia tena ili kukuwekea msisitizo na kukutia moyo uendelee kufanya, maana safari hii sio rahisi kama unavyofikiri au kama utakavyoambiwa.

SOMA; UKURASA WA 47; Kuwa Na Subira, Hakuna Unachopoteza.

pay price

Ufanye nini baada ya kufanya maamuzi?

Kwanza kabisa maamuzi ni neno kubwa sana na lenye maana nzito kuliko tunayoitumia kila siku. Unaposema umefanya maamuzi maana yake ni umeondoa uwezekano mwingine wowote wa wewe kufanya jambo tofauti na ulilolifanyia maamuzi. Maana halisi ya maamuzi ni kwmaba umechagua kitu kiwe hivyo tu, au umeamua kufanya kitu ulichokiwekea maamuzi na sio kitu kingine hasa kinachopingana na hiko.

Lakini katika maisha yetu ya kila siku tunafanya maamuzi na muda mfupi baadae unavunja maamuzi uliyofanya mwenyewe.

Unasema kwanzia sasa nitajisomea na kujifunza kila siku ili kuweza kupata maarifa yatakayoniwezesha kufikia mafanikio makubwa zaidi. Lakini baada ya muda unaanza kuona kujifunz ani jambo la kawaida na kutokufanya tena kila siku. Hapa ndio unaanza kurudi nyuma, na usipostuka mapema utapotea vibaya mno.

SOMA; Mambo 10 Unayotakiwa Kujua Kuhusu Uwekezaji.

 

Unasema kwamba kazi ndio msingi wa maendeleo na utafanya kazi kw ajuhudi na maarifa ili kuweza kufikia mafanikio makubwa. Baadae unaanza kufikiria kama unaweza kushinda bahati na sibu, au unaweza kushinda kamari. Hatimaye unajiingiza kwenye michezo hiyo, unapoteza muda na unatapeliwa.

Unasema utakuwa mwaminifu kwa sababu uaminifu ni mtaji muhimu wa wewe kufikia mafanikio makubwa. Baadae mtu anakufuata na kukuambia kuna njia ya mkato ya kupata fedha nyingi, ya kupata mafanikio, unashawishika kuijaribu, unafanya makosa na mbaya zaidi unatapeliwa. Hasara ya kutokuwa mwaminifu ni kutapeliwa.

Unapofanya maamuzi unahitaji kuwa na nidhamu ya hali ya juu sana. Unahitaji kuheshimu maamuzi yako mwenyewe na kutambua kwamba hiki ndio kitu ulichochagua kufanya kwenye maisha yako.

Usiangalie tena nyuma wala pembeni, unaweza kushawishika na vitu unavyoweza kuona ni vizuri kumbe ukivitazama kwa undani sio vizuri kama unavyofikiri.

Unapoanza kuvunja maamuzi yako mwenyewe unajijengea nidhamu mbovu na hivyo kushindwa kukomaa na kitu kimoja ulichochagua ili kuweza kufikia mafanikio.

SOMA; Sehemu Tano Unazoweza Kupata Mtaji Wa Kuanzia Biashara.

 

Unapofanya maamuzi, maana yake hiko ndio kitu ambacho umechagua kukifia, na ukiweza kukomaa nacho ni lazima utakipata.

Kama kweli unajua unachotaka, na ukawa unakitaka kweli na ukakomaa nacho kweli, dunia nzima itainama na kukupatia kile unachotaka. Ila utakapoanz akufanya maamuzi, ukayavunja, ukafanya mengine tena, ukayavunja hapa dunia yenyewe inakushang’aa maana haijui ikupatie nini hasa.

Amua leo kusimamia maamuzi yako hata uwe unapitia kitu gani. Chagua kutokuyumbishwa au kuona vingine ni vizuri kuliko ulichochagua mwenyewe. Fanyia kazi maamuzi yako na utaona mabadiliko.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, maana kwa kuamua tu na kuweza kusimamia maamuzi yako tayari umeshafanikiwa.

TUPO PAMOJA.

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

SOMA; Mambo Matano(5) Ambayo Ni Marufuku Kufanya Kwenye Eneo La Kazi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: