Jarida maarufu kwa kufuatilia watu matajiri duniani hivi karibuni limetoa orodha mpya ya watu matajiri sana duniani. Katika orodha hii mpya, mmiliki wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates amerudi kwenye nafasi ya kwanza na kuwa mtu tajiri kuliko watu wote duniani. Gates ana utajiri wa dola za kimarekani bilioni 79.2

Orodha hii ya 29, inaonesha kwamba duniani kuna jumla ya mabilionea 1826 na kwa mwaka jana tu mabilionea wapya 290 wameingia kwenye orodha hii. Pia vijana hawajaachwa nyuma, kwani mabilikonea 46 wana umri chini ya miaka 40.

Katika orodha hii ya mabilionea, 29 wanatoka Africa na hata hapa Tanzania tunaye bilionea ambaye ni Mohamed Dewji.

Orodha hii ya mabilionea inamengi sana ya kujifunza ambayo yanatuonesha kwamba nafasi hizi sio kwa ajili ya watu wachache tu. Bali kwa yeyote anayetaka kufikia nafasi hizi anaweza na hata anayezifikia hahakikishiwi kuwepo hapo milele.

bilionea

Leo katika makala hii tutajadili mambo kumi muhimu ya kuzingatia ili na wewe uweze kuingia kwenye orodha hii miaka ijayo. Mimi tayari nina mpango huo na najua hakuna kinachoweza kunizuia, kama na wewe una mpango huu karibu uongeze mbinu zitakazokusaidia. Kama huna mpango huu pia endelea kusoma na unaweza kuuweka au hata usipouweka bado utakuwa umejifunza mambo muhimu yatakayotatua matatizo yako ya kifedha.

SOMA; Kama Unafikiri Huwezi Kuwa Bilionea Soma Hapa Na Uanze Kuelekea Kwenye Ubilionea.

 

1. Amini kwamba inawezekana wewe kuwa bilionea.

Hatua ya kwanza kabisa ya wewe kuweza kuwa bilionea ni kuamini kwamba inawezekana. Maana kila kitu kwenye maisha kinaanza na imani. Kama unaamini unaweza ni kweli utaweza. Kama unaamini huwezi ni kweli hutaweza na hakuna atakayeweza kukulazimisha.

Kubali sasa kwamba unaweza kuwa bilionea na amua kuwa bilionea hayo mengine utajifunza ndani ya safari.

2. Mshahara hauwezi kukufikisha kwenye ubilionea.

Kama umeajiriwa unaweza kuchukuia hili ila ndio ukweli wenyewe. Mshahara hauwezi kukufikiasha kwenye ubilionea, sahau kabisa ndugu yangu. Niliangalia kwenye orodha hii ya forbes katika mabilionea 1826, 1191 ni wajasiriamali, yaani wametengeneza ubilionea wao wenyewe. 230 wamerithi utajiri wao na 405 wamerithi sehemu ya utajiri wao na wanaufanyia kazi kuukuza zaidi. Moja kwa moja wewe huwezi kurithi ubilionea kwa hiyo umebakiwa na njia moja tu, UJASIRIAMALI.

SOMA; Njia Nne Za Uhakika Za Kufikia Utajiri, Angalizo; Ajira Sio Mojawapo.

3. Chagua kitu kimoja, au vichache vya kufanya.

Ukiangalia orodha hii ya forbes, asilimia kubwa ya mabilionea wanafanya vitu vichache sana. Kwa mfano Bill Gates anamiliki kampuni ya kutengeneza program za kompyuta, Warren Buffet ni mwekezaji, Aliko Dangote yupo kwenye viwanda.

Ni muhimu sana wewe kuchagua kitu kimoja au vichache unavyopenda kufanya na uvifanyie kazi kwa juhudi na maarifa ili uweze kufikia mafanikio makubwa na utajiri.

4. Usichukie mabilionea.

Baada ya orodha hii kutoka, vyombo mbalimbali vya habari viliweka kwenye mitandao yao ya kijamii na wananchi wakaanza kutoa maoni yao. Wengi walikuwa wanatoa maoni ambayo ni ya hasira dhidi ya mabilionea hawa. Wengi walisema kwamba ni watu ambao ni wabinafsi, hawajali, wana fedha nyingi wakati watu wengine wanakufa njaa na kadhalika. Huenda na wewe una mawazo kama haya, sasa nakwambia mawazo hayo yanakurudisha nyuma. Kwa kuwachukia mabilionea unajizuia na wewe mwenyewe usiwe bilionea. Mambo mengi yanayosemwakuhusu mabilionea ni ya uongo. Soma namba tano hapo chini.

5. Wasaidie wengine.

Kutoa misaada ni moja ya mambo yatakayokuwezesha kufikia ubilionea. Watu wengi na huenda wewe ni mmoja wao wameaminishwa kwamba mabilionea ni watu ambao wanajali fedha zao tu na hawajali masikini. Lakini tukianza na mtu tajiri kuliko wote duniani, Bill Gates ndio mtoa msaada mkubwa duniani kupitia taasisi yake ya BILL AND MELLINDA GATES FAUNDATION. Taasisi hii imesaidia watu wengi sana huku africa na hata hapa Tanzania inafanya kazi. Unahitaji kutoa sehemu ya utajiri wako kwa watu ambao hawajiwezi na utapata utajiri mwingi zaidi.

Siri ya kupokea ni kutoa.

SOMA; Tumia Siri Hii Moja Kupata Chochote Unachotaka Kwenye Maisha Yako.

6. Fanya kazi kwa juhudi na maarifa.

Tabia ya kutega tega kazi haiwezi kukufikisha kwenye ubilionea. Na kwakuwa tumeshakubaliana kwamba ajira haiwezi kukufikisha kwenye ubilionea, unahitaji uwe mtu wa kujituma sana ili uweze kufanikiwa kwenye ujasiriamali. Unahitaji kujua vizuri kile unachofanya na kukifanya kwa ubora wa hali ya juu sanakuliko watu wengine wote walivyowahi kukifanya hapa duniani.

7. Usiridhike na mafanikio kidogo.

Hii ni sumu kubwa kwa watanzania kufikia ubilionea. Mtu anakuwa na biashara inayompatia faida kubwa kuliko wengine wanaomzunguka anaanza kujiona yeye yuko mbali sana. Anaanza kula starehe, kununua magari ya kifahari ambayo hayahitaji, kununua majumba makubwa ambayo hayamzalishii na vitu vingine vingi vya kujionesha. Sikiliza, hakuna wakati ambao unaweza kusema kwamba mimi ndio nimeshayaweza maisha, mimi nimeshakuwa mshindi, wakati huo utakaokubali hivyo ndio wakati ambao utaanz akuanguka, ndio wakati ambao utaanza kushindwa.

Usiridhike na mafanikio kidogo unayopata, endelea kuboresha zaidi na zaidi.

8. Soma, soma, soma.

Nafikiri hiki ni moja ya vitu ambavyo ni muhimu sana kuliko hata hivyo tulivyojadili hapo juu. Maana hata kama huna sifa tulizojadili hapo juu na hata kama hutaki kuwa nazo kwa kuanza kusoma leo, na kuendelea kusoma kila siku utashangaa unaanza kujijengea sifa hizo.

Siku moja mwanafunzi anayemaliza chuo alimuuliza Warren Buffet ni kitu gani anaweza kufanya ili na yeye awe tajiri sana. Warren Buffet alichukua karatasi na kumuonesha akamwambia, soma karatasi 500 kama hizi kila siku. Warren ni mzee, ana miaka 84 ila asilimia 80 ya muda wake wa kazi anautumia kusoma. Hii inamfanya aone ni kampuni gani zinafanya vizuri na kuweza kuzinunua, kusoma kumempa faid akubwa sana kuliko wengine ambao hawasomi kama yeye.

SOMA; Kama Hutajifunza Chochote Mwaka Huu 2015, Basi Jifunze Hiki Kimoja Tu

 

9. Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA.

Hili ni eneo muhimu ambapo utapata nafasi ya kujengewa misingi yote muhimu itakayokuwezesha wewe kuwa bilionea. Utajifunza kuhusu biashara na ujasiriamali, utajifunza kuhusu tabia za mafanikio, utapata uchambuzi wa vitabu mbalimbali ambavyo vitakubadili mtazamo wako na kukuongezea maarifa na kikubwa zaidi utapata nafasi ya kuwa kwenye kundi la wasap ambapo unakutana na watu wengine wanaoelekea kwenye ubilionea kama wewe. Yote hayo ni kwa ada ya tsh elfu 50 tu kwa mwaka. Kujiunga bonyeza maandishi haya KISIMA CHA MAARIFA.

SOMA; Faida Kumi Za Kujisomea Ukiacha Kuongeza Maarifa.

10. Soma kitabu; KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIO TAJIRI.

Kama unataka kujifunza zaidi mbinu ambazo zitakuwezesha kufika kwenye mafanikio makubwa na hatimaye kuwa bilionea, soma kitabu hiko. Hiki ni kitabu ambacho kimeeleza sababu 25 kwa nini mpaka sasa wewe ni masikini. Kama ukikisoma na kuyafanyia kazi mambo hayo 25, hakuna kitakachoweza kukuzuia kufikia ubilionea. Kitabu hiki kipo kwa sofy copy yaani PDF na kinatumwa kwa email. Gharama yake ni tsh elfu 5, kukipata tuma fedha hiyo kwenye namba 0717396253/0755953887 na utume email yako kisha utatumiwa kitabu.

Unaweza kuwa bilionea, ila sio kazi rahisi, unahitaji kujitoa, unahitaji kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, unahitaji kuweka malengo, unahitaji kuw amvumilivu, unahitaji kushirikiana vizuri na watu na unahitaji kujifunza kila siku, namaanisha kila siku. Endelea kutembelea mtandao huu wa AMKA MTANZANIA na hakikisha umeweka email yako ili kupata mambo mazuri yatakayokuwezesha kufikia mafanikio makubwa bure kabisa. Kujiunga bonyeza hapa na weka email yako.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio makubwa na kuwa bilionea.

TUPO PAMOJA.

Makirita Amani.

makirita@kisimachamaarifa.co.tz