Mambo 8 Muhimu Ambayo Ukiwa Mjasiriamali Ni Lazima Uyajue, Ili Kufikia Mafanikio Makubwa.

Ni ukweli usiopingika ili uweze kuwa mjasiriamali hai na kuweza kuona mafanikio makubwa yanatokea katika kile unachokifanya ni lazima kwako kujua mambo mengi sana ambayo yataweza kukusaidia na kukuweka imara hata katika kile kipindi ambacho mambo yako pengine yanapokaa vibaya.

Kwa kadri unavyozidi kujua mambo ama vitu vingi vinakuwa msaada mkubwa sana kwako na inakuwa inakusaidia wewe kuweza kukabiliana na changamoto za kijasiriamali/kibiashara kwa urahisi. Katika makala ya leo tutakwenda kuangalia mambo muhimu ambayo ukiwa mjasiriamali ni lazima uyajue, ili kuwa na mafanikio makubwa. Mambo hayo ni haya hapa kama ifuatavyo:-

1. Ni lazima ujue kuwa, hakuna mafanikio utakayoyapata bila wewe kujitoa.
Huu ndio ukweli wa mambo ambao ni muhimu sana kwako kuujua ukiwa kama mjasiriamali kuwa, huwezi na hutaweza kufanikisha chochote kama huwezi kujitoa mhanga kuweza kupigania kile unachotaka kiwe katika maisha yako. Wajasiriamali wote wana sifa ya kutengeneza maisha yao na si vinginevyo. Kama tu utakuwa ni mtu wa kukaa na kusubiri mafanikio na miujiza basi sahau mafanikio kwa upande wako. 
 
2. Ni lazima ujue kuwa, wewe ni kiongozi wa maisha yako mwenyewe.
Haijalishi unasimamia biashara yako wewe mwenyewe au umeajiri mtu, lakini kwa kitendo cha kuwa mjasiriamali ni jambo ambalo linakulazimisha kuwa kuwa kiongozi wa maisha yako na biashara yako kwa ujumla. Wajasiriamali wakubwa na wenye mafanikio wanalijua hili, ndio maana huwa ni watu wa kuendesha biashara zao kwa mafanikio makubwa kutokana na kujua kujiongoza wao wenyewe na biashara kwa ujumla.
3. Ni lazima ujue kuwa, hakuna muda maaalum wa kufanya kazi.
Mara nyingi kuna wakati huwa sio jambo geni kwa mtu mjasiriamali kulazimika kubaki macho hata usiku wa manane ili kuhakikisha mipango na malengo inaenda sawa. Hili ni jambo ambalo kila mjasiriamali aliyeamua kufanikiwa na kufika mbali ni lazima alijue kuwa kuna wakati ni lazima ujitoe hata kwa kutumia muda au saa nyingi zaidi ili mambo yaende sawa kama unavyotaka.
4. Ni lazima ujue, umuhimu wa kujijengee tabia ya kuwa mtu wa vitendo zaidi.
Wajasiriamali wenye mafanikio huwa na watu ambao hawajui kusubiri wala kuahirisha mambo, bali huwa ni watu wa kuhakikisha ni lazima ndoto na malengo yao yatimie kwa namna yoyote ile. Unapokuwa mjasiriamali ni lazima na muhimu sana kujua hili kuwa huhitaji kusubiri kesho ili kufanya mambo yako. Fanya kila linawezekana leo hiyo itakujengea nguvu kubwa ya kuweza kusonga mbele.  
5. Ni lazima ujue kuwa, hutakiwi kuogopa kitu chochote.
Katika safari yako ya ujasiriamali kitu pekee ambacho unatakiwa kujua ni kujifunza kutokuogopa kitu hususani kuogopa kushindwa. Kumbuka kushindwa ni sehemu muhimu ya mafanikio hasa kwa kujifunza zaidi pale unapokosea. Kwahiyo katika moja ya jambo muhimu ambalo kila mjasiriamali anatakiwa kulijua ni kutokuogopa makosa. Kama utaishi kwa kutokugopa makosa na kutenda mabo yako bila hofu, hiyo itakusaidia sana kufika mbali kimafanikio.
6. Ni lazima ujue kuwa, kuna umuhimu mkubwa wa kuandika mawazo yako.
Ni kitu ambacho unaweza ukakiona ni cha kawaida kabisa na ukaona pengine haina haja ya kuweka kumbukumbu muhimu kwa mawazo yanayokujia katika kichwa chako. Kwa kufanya hivi mara kwa mara umejikuta ukiwa ni mtu wa kupoteza mawazo mazuri sana ambayo pengine yangekusaidia kutatua changamoto zinazokukabili. Ukiwa kama mjasiriamali mwenye nia ya mafanikio makubwa, ni muhimu sana kwako kujiwekea kumbukumbu ya kuandika mawazo yako yale unayoona ni ya muhimu zaidi.
7. Ni lazima ujue, umuhimu wa kung’ang’ania ndoto zako mapaka mwisho.
Watu wengi huwa wana mawazo mazuri sana, lakini pia huwa ni watu wa kushindwa na ndoto zao huwa hazifanikiwi. Kitu kimojawapo kinachopelekea hali hiyo iwe hivyo kwao ni kule kushindwa kushikilia na kung’ang’ania ndoto na malengo yako mpaka mwisho. Kuwa king’ang’anizi kwenye ndoto zako ni moja ya kitu ambacho kinaweza kukutofautisha wewe na wale wanaoshindwa katika maisha. Hivyo, ni muhimu kujua hili ukiwa kama mjasiriamali.
8. Ni lazima ujue kuwa, kuna kukatishwa tamaa.
Hata ufanye nini au ufanye kwa ukamilifu vipi lakini inakulazima kuelewa hili kuwa unaishi katika dunia ambayo mara nyingi inakatisha tamaa kwa mambo mengi. Usipokuwa makini utashangaa unajikuta ukiwa mtu wa kuumia na kushindwa kupangilia mipango yako vizuri kutokana na maneno ambayo pengine unakuwa unaambiwa kuwa labda huwezi kufanikiwa kwa kile unachokifanya.
 
Kwa kumalizia, hayo ndiyo mambo muhimu ambayo ni lazima kwako uweze kuyajua ukiwa kama mjasiriamali ili kuweza kufanikiwa na kusonga mbele zaidi katika safari yako ya kibiashara. 
Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa elimu na maarifa bora yatakayoboresha maisha yako.
Nakutakia kila la kheri katika safari ya mafanikio, endelea kutembelea AMKA MTANZANIA  kila siku, kujifunza na kuhamasika.
  
TUPO PAMOJA,
 
IMANI NGWANGWALU,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: