Mambo 20 Niliyojifunza Kutoka Kwenye Kitabu Cha; The25 Sales Habits Of Highly Successful Salespeople

Habari za leo msomaji mwenzangu. Kama nilivyoahidi wiki iliyopita kwamba nitakua nikishirikisha mambo 20 kila wiki niliyojifunza kutoka kwenye kitabu kimoja kati ya 2; Wiki hii tunaendelea kama ufuatavyo.

Wiki hii nitakushirkisha mambo 20 niliyojifunza kutoka kwenye kitabu cha; The25 Sales Habits of Highly Successful Salespeople –Kiilichoandikwa na mwandishi Stephan Schiffman

Karibu

1. Wauzaji mashuhri ni wale wenye uwezo wa kutatua matatizo. Lazima uwe na mtazamo wa kutatua matatizo kwa kutoa suluhisho kwa wateja wako. Mfano kama unafanya biashara ya magari lazima uwe na matazamo wa kutatua tatizo la usafiri na usafirishaji. Kama unafanya biashara ya simu lazima uelewe kwamba upo ili kutatua tatizo la mawasliano. Kwa hiyo kabla hujaingia kwenye hiyo lazma uwe na mtazamo wa kutatua tatizo.Kwanza lazima ulitambue na kulielewa vizuri tatizo kabla ya kujaribu kulitatua. Hii itakusaidia kuwa mbunifu mzuri katika kuboresha huduma au bidhaa yako ili kutatua tatizo husika ipasavyo.

2. Je bidhaa au huduma unayouza unaweza kuibadilisha ikakidhi kusudi au uhitaji mwingne ili kupanua wigo? Je bidhaa au huduma yako unaweza kubadili kukidhi uhitaji wa watu wengne zaidi wa wale wa mwanzo? Mfano mwanzilishi wa Facebook bwana Mark Zuckerberg , wakati anaanzisha Facebook ilikua kwa minajili ya kuwasaidia wanafunzi wa chuo alipokua anasoma waweze kuwasiliana, lakin aligundua kua huduma anayoitoa anaweza kuiboresha na kufikia watu wengne wengi zaidi ya wanafunzi wa pale chuoni. Leo hii ni historia bwana Mark Zuckerberg ni ndio tajiri namba moja duniani mwenye umri mdogo.

SOMA; Kwa Nini Watu Hawawaambii Wengine Kuhusu Biashara Yako.

3. Unapo deal na mteja mpya usikimbilie kumuuzia tu huduma au bidhaa yako. Hakikisha unatengeneza mahusiano naye mazuri. Sio swala la kuuza tu, unatakiwa kumfanya mteja awe na hamasa ya kurudi tena na tena

4. Sikiliza, jifunze, Ongoza (Listen, learn, and lead). Ukisikiliza kutakufanya ujue nini tatizo la mteja wako. Ukijifunza unajiongezea maarifa unakua mwerevu zaidi hivyo kua na uwezo wa kuongoza wateja kule unakotaka waelekee.

5. Kuandika maelezo (taking Notes) wakati unapokutana na mteja mtarajiwa (prospect) ni nyenzo ya mazuzo yenye nguvu sana(powerful sales tool). Hakikisha wakati wa mazungumzo unaandika mahali ili kukusaidi kujua vizuri tatizo la mteja wako mtarajiwa. Kuchukua maelezo pia kutakusaidia yafuatayo:

· Kuandika kutakusaidia kusikiliza kwa makini, na itakua ngumu kusahau pointi muhimu

· Kuchukua maelezo kunakuweka katika hali ya kua na mamlaka na uthibiti

· Kutaimarisha uwezo wako wa uchambuzi. Maana unahusisha milango mitatu ya fahamau amabyo ni Kugusa( unapoandika), kusikia ( unaandika ulichokisikiliza kutoka kwa mteja wako), kuona (Unaona ulichokiandika)

· Kutakusaidia kuapta taarifa zaidi kutoka kwa mteja wako mtarajiwa. Maana atajisikia vizuri kufunguka maana anaona unajali anchoongea na upo serious katika kutatua changamoto aliyonayo

6. Tengeneza mpango wa kila mteja wako mtarajiwa. Mpango utakua pia unaonyesha jinsi gani ya kutatua tatizo lake kutokana na maelezo uliyokua ukiyaandika kwenye vikao vya nyuma kama ilivyoelezwa kwenye pointi ya hapo juu. Mpango utakua ni dira ya kufahamu ni kitu gani cha tofauti hasa unachoweza kufanya kwa huyo mteja wako. Kusikiliza ndio siri ya kwanza, na kutambua suluhisho zitakozokubaliwa na pande zote mbili ni siri ya pili.

7. Unatakiwa uwe daktari. Mfano: Unapokwenda hospitali labda tumbo linakuuma kisasawasawa , Unapofika kwa daktari hautojali kwamba amehudumia wagonjwa wangapi au wagonjwa wangapi wako wanamsubiri. Utakachopenda ni akuhudumie. Utataka akupeleke kwenye chumba cha matibabu kwa ajli ya uchunguzi na kukupatia matibabu sahihi kabla hajakimbia kwenda kuhangaikia wagonjwa wengine. Utataka akuulize unajisiakiaje, umekua na hali hii kwa muda gani, je ulishawahi kupatwa na tatizo kama hili nyakati zilizopita, nk. Kama daktari akikufanyia hayo yote na akakupa matibabu utafurahi na utakua na mtazamo mzuri zaidi kwake, na hata utapenda kuja kumuona wakati mwingne. Pia utapenda kuwashauri wengne wenye tatizo kama lako waende kwa daktari huyo kwa sababu ya huduma yake nzuri.

Hivyohivyo basi mtu wa mauzo (Salesperson) au muuzaji ni daktari. Haijalishi umehudumia wagonjwa (wateja) wangapi. Huyu mteja mtarajiwa (new propect/customer) ndio yeye tu ambaye unapaswa kumuona kwa wakati huo, na kumhudumia kipekee. Usimhudumie kwa harakaraka ili ukimbilie wengine, hakikisha umetatua tatizo lake na ameridhika. Mfanye ajione yeye ni wa pekee kwa wakati huo unaomhudumia. Kufanya hivyo hakuta fanya tu mazingira ya kaz yawe mazuri, bali pia kutaongeza kupendwa kwako na wateja na kupelekea watamani kurudi tena na tena.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuibadili Dunia.

8. Onyesha kua na shauku. Unapohudumia wateja wako, au unapokutana na mteja mtarajiwa onyesha shauku. Hii itamfanya asijiskike kwamba ni wa kawaida tu, atajisikia vizuri maana anona uko excited kukutana naye.

9. Jipe sifa unazo stahili. Ongea kuhusu wewe lakini katika hali ya unyenyekevu ili islitete tafsiri ya kua unajivuna. Uongee kwa ujasiri kuhusu biashara yako na mambo amabayo inaweza kutatua, cha muhimu epuka mbwembwe nyingi zisizokua na maana.

10. Jifunze kusoma hali na nyakati. Sio kila kinachofaa kwa mteja A kitafanya kazi kwa mteja B… You have to learn how to read the situation

11. Kwa wataalamu wengi wapo makundi mawili;

· Kundi la kwanza ni lile la wataalumu ambao wanaongeza thamani kwenye kila kitu wanchokigusa au kukifanya.

· Kundi la pili ni wale wanaofanya thamani ya kila wanachoguza ishuke.

Kama wewe ni mtaalamu thibitisha kwamba upo kwenye kundi la kwanza. Onyesha thamani yako. Hakikisha kila unachofanya unaongeza thamani yake.

12. Ukweli ni nyenzo muhimu. Unapaswa kua mkweli maana ndio rahisi kuukumbuka. Ukweli ni rahisi kuukumbuka kuliko uongo. Ndo maana wanasema ukiwa muongo uwe na kumbukumbu vizuri, maana utaumbuka tu siku moja. Hakikisha unajenga uaminifu na wateja wako kwa kua mkweli. Tell the truth; it’s easier to remember. Don’t promise your customer what you can’t deliver

13. Jiuze kwako mwenyewe (Sell Yourself on Yourself). Jihamasishe mwenyewe kwanza kabla ya kuhamasisha wengine. Kabla hujajiuza kwa wengine anza kujiuza kwako kwanza. Taswira yako mwenyewe (Your self-image) ni ya muhimu sana. Utakavyojiona ndivyo na wengine watakavyokuona.

14. Mhusishe mteja. Usiwe wewe ndo muongeaji tu mwanzo mwisho. Mfanye aongee kuhusu yeye mwenyewe. Hii itafanya akupe taarifa ambazo utajua ni suluhisho gani anahitaji. Hata kama unaongea usijisahau ukaongea tu kuhusu wewe na biashara yako. Hakikisha kunakua kwa faida yake. Mpe nafasi pia atoe maoni yake.

SOMA; Hizi Ndizo Sifa Saba Za Kiongozi Bora.

15. Anza mapema siku yako. Hii ni moja ya siri za watu waliofanikiwa. Unapoanza mapema unashauriwa kupata wasaa wa kutulia pekee yako na kutafakari. Wakati huu ni wa kwako na wewe, unahojiana na wewe mwenyewe. Unaichaji akili yako na utaona utofauti. Ukichunguza watu wanoamka alfjiri na mapema na wale wanoamka sa 2 asubuhi utendaji wao wa kazi ni tofauti sana. Kwa watu wengi alfajiri ndio wakati akili inakua na nguvu. Mimi mweneywe siku nikiamka mapema afajiri hua nakua na hamasa kubwa ya kazi. Lakini siku umechelewa kuamka, kwanza unakua huna raha, unaona umechelewa, unakosa muda wa kutafakari au kumuomba Mungu, na hata ukitafakari wakati umeamka kwa kuchelewa akili yako haitakua imetulia maana muda wote inawaza saa ngapi utafika kazini. Ukijijengea tabia hii ya kuamka mapema na kuutumia muda huo kufanya vitu vya maana lazima utaongoza kwenye sehemu uliyopo, iwe biashara, kazini n.k

16. Usisikilize redio au kuangalia TV asubuhi. Habari nyingi utakazosikia au kuziona wakati huo ni habari mbaya (hasi) amabazo zitakutia hofu na kukukatisha tamaa. Badala yake tafuta CD au video au chochote kile cha kuhamasisha. Hakikisha siku yako unaianza kwa hamasa kubwa.

17. Soma vitabu, majarida au machapisho yanayohusiana na biashara au kazi unayofanya. Hii ndiyo njia ya uhakika ya kukuweka juu, Maana utakua na maarifa makubwa ambapo yatakusaidia katika ubunifu. Ukisoma ukafikisha vitabu au machapisho 500 utakua kati ya watu 1% ya wale waliofanikiwa sana katika hiyo biashara au kazi. Pia hii itakuongezea kujiamini maana utakua umebobea na utakua mtaalamu wa kutegemewa maana unataarifa nyingi zenye thamani kubwa.

18. Mteja sio mara zote yuko sahihi. “Mteja mara zote yuko sahihi “ Hii ni moja kati ya amri kumi za mauzo, na amri hii ya kwamba mteja yuko sahihi imekua ikivuka kizazi hadi kizazi. Lakini si kweli kwamba mteja yuko sahihi mara zote. Lakini haimaanishi kwamba umwambie mteja wako kwamba hayuko sahihi. Kua mbunifu katika kuonyesha usahihi, aidha kwa kutoa kama pendekezo. Forget the conventional wisdom. I t’s okay to tell a customer that there’s a better way.

19. Makosa hua yanatokea. Unapokosea haipaswi kujuuta mpaka unaharibu mambo mengine. Kua muwazi kukiri kosa omba msamaha na kusonga mbele. Jifunze kutokana na kosa fanya maboresho husika.

20. Ona fahari ya kile unachokifanya au unachouza. Mwambie kila unyekutana naye kuhusu kampuni unayofanya kazi na bidhaa au huduma zinazopatikana.

Makala hii imeandikwa na Ndugu Daudi Mwakalinga mwandishi, mhamasishaji na mshauri katika masuala ya kilimo. Unaweza kuwasiliana nae kwa simu 0763 071007 au 0658 587029 au email daudimwakalinga@yahoo.com au dd.mwakalinga@gmail.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s