Hii Ndiyo Siri Kubwa Ya Kuishi Maisha Marefu Na Yenye Mafanikio Makubwa.

Kwa mamilioni ya watu, hasa wakazi wa mijini maisha yamekuwa yakutatanisha sana, na yenye hekaheka nyingi zenye kuchosha. Ukweli ni kwamba, maisha ya kisasa yamejaa kila aina ya sononi na kusongeka kwa wingi, ikilinganishwa na maisha yalivyokuwa katika miaka ya nyuma, pengine kufikia mwaka 1980, maisha yalikuwa rahisi, sahihi na yalikuwa ya hekaheka kidogo zaidi.

Watu walikuwa wakiishi kufuatana na kanuni za asili za mazingira na majira ambapo , wakati wa mchana walifanya kazi na usiku walikuwa na familia zao pamoja wakifurahia maisha na kisha kwenda kulala.

Kuna kabila moja linaloishi jangwani katika nchi ya Israel. Kabila hili linafahamika kama mabedui ambao, ni wafugaji wazuri sana wa kondoo na ngamia. Inaamika kuwa watu hawa wana uwezo wa kuishi miaka mingi zaidi hadi kufikia 100. Mtindo wao wa maisha ni ule wa kuhamahama jangwani kwa ajili ya kutafuta malisho.

Utafiti uliofanywa na serikali  ya Israeli kwa lengo la kutaka kugundua siri inayowafanya watu hwa kuweza kuishi kwa muda mrefu zaidi , uliweza kugundua mambo yafuatayo:-

Chakula chao kikuu ni pamoja na nafaka zisizokobolewa, hawatumii kabisa vyakula kutoka kiwandani, hula nyama kwa kiasi kidogo sana. Watu hawa pia hawana hofu kubwa ya maisha kama ilivyo kwetu huku kwa sasa. Na kwa hiyo hawana sononi na wala hawasongeki kirasi katika maisha yao.


Pia watu hawa siri nyingine ya kuweza kuishi maisha hayo marefu ilikuja kugundulika kuwa ni watu ambao katika maisha yao yote huamka asubuhi na mapema kabla ya jua kuchomoza na kuanza kuchapa kazi kwa bidii tokea asubuhi hadi jioni wanaporejea nyumbani kwa ajili ya kumpumzika.


Lakini zaidi, ni kawaida kwao kila jioni kwa familia nzima kuweza kukutana na kujipati chakul cha jioni . na baada ya hapo familia hiyo hukaa na kuota moto na huku watu wazima wakiwasimulia watoto wao hadithi na hata wakati mwingine kuimba nyimbo mbalimbali kwa muda wa saa 3 au 4 hivi baadaye ndipo wanakwenda kulala.

Hawasumbuliwi na kelele za magari, viwanda  au mashine nyingine. Wao huweza kufurahia uumbaji asilia ambao huwachochoea katika kufikiri na kutafakari kwa kina zaidi na kuwajengea matumaini mema katika maisha yao.

Hawaishi maisha yenye pilikapilika nyingi ambazo zisizokwisha  na ambayo yamekosa msingi imara wa uhusiano na ushirikiano miongoni mwa watu katika familia na jamii nzima. Wanaishi maisha rahisi kabisa na kwa umoja wa kufuata mtindo wa maisha unaoongozwa na kanuni za asili za uumbaji ambazo, huwafanya waweze kuishi miaka mingi.

Wao hawatumii fedha katika kutimiza mahitaji yao muhimu wala hawatumii matibabu ya kisasa. Na wala hawayahitaji hayo. Wao hutumia mitishamba kwa ajili ya tiba zao wanazozihitaji. Wao pia hujenga uhusiano  mshikamanifu na hutumia muda wao mwingi sana kwa njia iliyotofuti na ya yetu. Hii ndiyo siri yao kubwa.


Ni kama vile wanafuata mtindo wa maisha unaocheza muziki unaopigwa na uumbaji wa asili. Njia yao ya maisha ni njia ambayo, iko huru kutoka kwenye kila aina ya mfadhaiko, sononi na kusongeka kimaisha na vilevile huru kutoka kwenye mtindo wa maisha unaosababisha afya mbaya ya kimwili na kihisia.

Jambo moja kubwa la kufurahisha ni kwamba, mtindo huu wa maisha hauwezi kununuliwa kwa feha. Ukweli ni kwamba, kuna watu wengi wenye fedha nyingi  za ziada ambao wamesongeka na hawafurahii maisha ukilinganisha na mabedui ambao wanaishi maisha ya kawaida tu tofauti na wao.

Bila shaka, hakuna mtu anayeweza kupunguza kasi ya ulimwengu huu wa kisasa. Hata hivyo , sisi wenyewe tunaweza kufanya marekebisho yanayofafaa katika mitindo yetu ya kimaisha, ili tuweze kuishi maisha tulivu, yenye usawazisho , yanayoridhisha, yanayofurahisha na yanayowezakutuongezea siku zetu za kuishi.

Kwa  kumudu kuishi maisha hayo tutajikuta ni watu wa amani kubwa, utulivu ndani yetu na pia hii ndiyo siri kubwa ya kuweza kuishi maisha ya furaha na mafanikio makubwa katika maisha. Huwezi kutegemea kuwa na mafanikio makubwa kama wewe wenyewe hulindi afya yako inayokuwezesha kufikia hayo mafanikio unahitaji.

Hivyo tunakuja kuona kuwa, katika harakati za mafanikio kuwa na afya njema, kuishi maisha ya utulivu na kufuata mtindo wa maisha unaendana na uasili wetu ni siri kubwa sana ya kuweza kutufanikisha kwa kile tunachokifanya katika maisha yetu.

Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kuboresha maisha yako.

Tunakutakia kila la kheri katika safari ya maisha yako iwe ya ushindi na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kujifunza kila siku.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: