Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutatua Tatizo Ulilonalo Kwa Usahihi Zaidi.

Mara nyingi katika maisha yetu tunayoishi kukutana na changamoto ama matatizo ni kitu ambacho huwa hakikwepeki. Changamoto hizi huwa tunakutana nazo kila siku na kila mara katika maisha yetu. Wengi wanapokutana na changamoto hizi huwa ni watu wa kukata tamaa na kujiona kama vile wasiofaa kitu na kujisahau kuwa kumbe wana uwezo wa kutatua chngamoto hizo kwa usahihi zaidi.
Na ijulikane kuwa maisha kama maisha yalivyo yenyewe, huwa hayakosi  changamoto hizi hata iweje. Changamoto ama matatizo tunayoweza kukutana nayo mara nyingi ni  kama vile ukosefu wa pesa, tatizo la afya ama ukosefu wa amani katika sehemu zetu tunazoishi na vurugu nyingine nyingi. Hizi huwa tu ni baadhi ya changamoto chache kati ya nyingi ambzazo huwa tunaweza kukutana nazo katika jamii zetu kila siku.
Lakini kitu cha kujiuliza hapa huwa tunaweza kukabiliana vipi na changamoto hizo na kuishi maisha ya ushindi na furaha. Hiki ndicho kitu ambacho tunataka ujifunze kupitia makala hii unayoisoma. Badala ya kulia na kuumia ni vyema ukajua namna ya kukabiliana na tatizo lako kwa njia sahihi. Tambua lipo jibu na unaweza kulitatua tatizo lako mpaka likafika mwisho. Utawezaje?
Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutatua Tatizo Ulilonalo Kwa Usahihi Zaidi:-
1. Acha kuliwekea mkazo zaidi.
Ili uweze kulitatua tatizo ulilonalo kwa urahisi, moja ya kitu muhimu unachotakiwa kukifanya ni kutolizingatia sana hilo tatizo lako. Sio ninamaanisha uliache, hapana. Ila  jifunze kuweka nguvu zako nyingi kwenye suluhisho na siyo kulifikiria sana tatizo lako hilo. Kwa kulifikiri a tatizo lako kwa muda mrefu na ukafikiri utapata majibu hiyo itakuwa ni sawa na kujidanganya wewe kwani utaongeza zaidi tatizo kutokana nguvu hasi utakazokuwa ukizivuta.

Wengi kwa kutokujua hujikuta ni watu wa kufikiria sana matatizo yao kiasi cha kwamba mpaka hufikia hatua ya kuweza kukonda. Acha kukondoshwa na tatizo ulilonalo zaidi chukua hatua ya kuweza kulitatua tatizo hilo kwa njia sahihi. Lakini  Kama utendelea kulifikiria tu hilo tatizo lako elewa hutaweza kufanikiwa kulitatua zaidi utaumia. Ukumbuke tu wewe siyo wa kwanza kukutana na tatizo kama hilo, wapo watu walioshinda na wewe unaweza.
2. Acha kulikuza zaidi tatizo hilo.
Ni kweli kuna wakati matatizo au changamoto tunazokutana nazo huwa zinakuwa kubwa zaidi kutokana na sisi wenyewe kuzikuza zaidi. Inawezekana kabisa tatizo ambalo lingetatuliwa kwa njia rahisi, lakini kwa sababu ya kukuzwa huweza kuonekana kubwa zaidi na lisilowezekana.
Inabidi tuweze kujifunza kukabilabna na tatizo kwa uhalisia halisi kuliko kulikuza tu. Unapokuza tatizo hiyo itakufanya wewe uonekane mnyonge na mshindwaji kabisa. Jipe moyo na nguvu kuwa, una uwezo wa kutatua tatizo ulinalo. Ukiweza kutolikuza tatizo lako elewa kabisa utakuwa umelikabili hilo tatizo kwa njia rahisi na usahihi.
3. Acha kuwa na mtazamo hasi juu ya tatizo lako.
Kama unataka usifanikiwe na kubaki hapo ulipo endelea kuwa na mtazamo hasi juu yamatatizo yako. Unapokuwa na mtazamo hasi unakuwa hauna uwezo wa kukabiliana nalo kwani unakuwa sawa na umejikabidhi kuwa wewe umeshindwa.
Watu wengi wanaoshindwa kufanikiwa kutatua matatizo yako kwa njia sahihi huwa ni watu wa tabia za mitazmo hasi sana juu ya matatizo waliyonayo. Kwa mitazamo hii ndiyo huwa inawafaanya kushindwa kwa namna moja au nyingnie. Kama unataka kuwa mshindi katika maisha yako jifunze kuwa na mtazamo chanya.
4. Acha kukata tamaa.
Mara nyingi unaweza ukajiona wewe ndiyo umefika mwisho wa tatizo lako ulilonalo kuwa limekushinda na huwezi kutoka tena hapo ulipo. Hii yote inakuja kutokana na kuangalia tatizo lako na kuliona kubwa sana na kwamba huwezi kulishinda kabisa.
Ili uweze kuondokana na hali hiyo, jifunze kutokukata tamaa mapema. Kitu kikubwa kwako tambua kuwa tatizo ulilonalo litapita na itafika muda utalisahau kabisa. Kwa kulitambua hilo unaweza ukaelekeza nguvu zako zote kwa kulitatua tatizo hio badala ya kukaa na kuanza kukata tamaa hiyo haitakusaidia sana. Jipe moyo kisha songa mbele.

Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kuboresha maisha yako.

Tunakutakia kila la kheri katika safari ya maisha yako iwe ya ushindi na endelea kutembelea AMKAMTANZANIA kujifunza kila siku.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: