KITABU; Change Your Thinking, Change Your Life(Badili Fikra Zako, Ubadili Maisha Yako).

Karibu tena kwenye utaratibu wetu w akutumiana kitabu kimoja cha kujisomea kila mwezi. Leo utajipatia kitabu cha kujisomea kwa mwezi huu wa sita.
Kila mmoja wetu anapenda maisha yake yabadilike na kuwa bora zaidi. Hakuna anayependa kuendelea kuwa pale alipo kwa sasa. Tunapenda kwenda mbele zaidi ili tuweze kufikia mafanikio makubwa na kuwa na maisha yaliyo bora.
Lakini pamoja na kutaka mabadiliko haya, bado wengi wetu hatujui ni kitu gani hasa tunahitaji kufanya ili kuyafikia mabadiliko ya kweli. Huwa tunatamani watu wengine wabadilike, uchumi uwe sawa, serikali iwe nzuri, ndugu zetu watuelewe na mengine mengi. Tunaamini kwamba hatufikii mafanikio kwa sababu kuna watu wengine wanatuzuia kufikia mafanikio yetu.
Huu ni uongo mkubwa sana, hufikii mafanikio sio kwa sababu watu wengine wanakuzuia. Hubadiliki sio kwa sababu watu wengine wanakuzuia ila kwa sababu bado wewe mwenyewe hujaamua kubadilika. bado wewe mwenyewe unaendelea kufanya yale ambayo ulikuwa unafanya na hivyo kuendelea kupata matokeo ambayo ulikuwa unapata.
Huwezi kubadili maisha yako kama hutobadili fikra zako. Kubadili fikra ndio hatua ya kwanza kabisa ya kuleta mabadiliko ya kweli kwenye maisha yako na mabadiliko haya yakakuletea mafanikio. Watu wengi hawaelewi hili, watu wengi hawajui nguvu ya fikra kwenye kuleta mabadiliko.
Mwandishi na mhamasishaji Brian Tracy aliliona hilo hivyo kuandika kitabu CHANGE YOUR THINKING, CHANGE YOUR LIFE. Katika kitabu hiki mwandishi ameeleza kwa kina uhusiano wa fikra zako na kila kinachoendelea kwenye maisha yako. Na pia ameeleza umuhimu wa kubadili fikra zako ili uweze kubadili maisha yako.
Ninachoweza kukuambia ni kwamba kama hutobadili fikra zako, huwezi kubadili maisha yako. Hiki ni kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho na nimekuwa naona kinawatesa watu wengi sana. Uko hapo ulipo sasa kutokana na fikra ambazo umekuwa unaweka kwenye akili yako. Kutoka hapo ulipo ni lazima uanze kuweka fikra nyingine mpya kwenye akili yako. Lazima uanze na fikra mpya zinazoendana na yale mabadiliko na mafanikio unayotaka kwenye maisha yako.
Sisi wanadamu ni kama sumaku, kile unachofikiria mara nyingi ndio kinachotokea kwenye maisha yako. Hata watu ambao wamekuzunguka umewavutia kwa mawazo uliyonayo kwenye akili yako. Utakapoanza kubadili mawazo yako utaweza kubadili hata watu wanaokuzunguka.
Nakusihi sana usome kitabu hiki, kitakufungulia njia nyingi za mafanikio kwenye kazo, biashara na maisha kwa ujumla. Hata kama utafanya kazi kwa nguvu kiasi gani, kama fikra zako sio nzuri, kama mtazamo wako ni hasi hakuna chochote kikubwa kinachoweza kutokea kwenye maisha yako.
Soma kitabu hiki na fanyia kazi yale ambayo utajifunza, ni mengi sana, hapa nimegusia tone tu. Kwa kukisoma utapata picha kubwa ya jinsi maisha yako yanavyoweza kubadilika kwa kuanzia na mawazo na fikra zako.
Kupata kitabu hiki bonyeza maandishi haya ya kitabu; CHANGE YOUR THINKING, CHANGE YOUR LIFE.
Usisahau kunishirikisha yale uliyojifunza kwenye vitabu tulivyokutumia awali na jinsi gani vimebadili maisha yako. Unapoandika yale umejifunza unayaingiza kwenye mawazo yako zaidi.
Kupata uchambuzi wa vitabu hivi kwa lugha rahisi ya kiswahili kila wiki jiunge na KISIMA CHA MAARIFA, bonyeza hayo maandishi kupata maelezo zaidi.
Nakutakia kila la kheri kwenye kubadili maisha yako, kwa kuanza kubadili fikra zako. Hakuna kitakachokushinda.
TUPO PAMOJA, TUTAKUTANA KILELENI.
Makirita AMANAI,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: