Kama kuna kitu kimoja ambacho naweza kumshauri mtu yeyote anayetaka kubadili maisha yake basi ni hiki; JIFUNZE KILA SIKU. Ndio mabadiliko ya maisha yako yataanza pale ambapo utakuwa na maarifa sahihi halafu ukayafanyia kazi maarifa hayo na maisha yako yakawa bora.
Lakini jambo kubwa la kushangaza ni kwamba wengi wetu huwa hatujifunzi, tunaona tunajua kila tunachotaka kujua. Mwishowe tunalalamika kwa nini maisha yetu hayawi bora licha ya kuweka juhudi. Sasa leo nakuambia kwamba juhudi pekee bila ya kuwa na maarifa sahihi ni kazi bure.
Watu wengine pia wamekuwa wakilalamika kwamba wanapenda kujifunza lakini hawana muda wa kusoma vitabu, au kuhudhuria mafunzo mbalimbali. Huenda ni kweli kwamba kazi nyingine zinabana na kuchosha kiasi kwamba mtu hawezi kupata muda wa kutulia na kusoma vitabu. Lakini hii sio sababu ya wewe kutokujifunza, kwani kuna njia nzuri sana unazoweza kutumia kujifunza kila siku hata kama unafanya kazi masaa 24 kwa siku.
Na hapa nitakupa njia hiyo bora kabisa itakayobadili maisha yako KAMA UTACHUKUA HATUA.

 
Njia ninayokwenda kukushirikisha hapa ni kusikiliza vitabu vilivyosomwa (AUDIO BOOK) vitabu hivi vinatoa maarifa bora kabisa ya kukufundisha na kukuhamasisha. Vitabu hivi unaweza kuvisikiliza popote pale unapokuwa, iwe kwenye gari yako binafsi, iwe kwenye foleni, iwe kwa kutumia simu, iwe kw akitumia redio na njia nyingine yoyote.
Tumekuandalia vitabu kumi na mbili(12) bora sana kwako na kama ukivisikiliza na kufanyia kazi maisha yako hayatabaki kama yalivyo sasa. Vitabu hivi vimewekwa kwenye memory card yenye ukubwa wa 4GB na kadi hii unaweza kuiweka kwenye kifaa chochote kinachopokea memory card.
Leo nakupa mbinu kubwa sana ya kujifunza ambayo mimi binafsi huwa naitumia. Lengo lako kuu liwe unapokuwa barabarani kuelekea sehemu yoyote basi sikiliza vitabu hivi vilivyosomwa. Kama upo kwenye gari lako binafsi weka memory card hii kwenye redio yako ya gari na sikiliza mafunzo. Kama unatumia usafiri wa uma kuwa na head phone/ ear phone zako nzuri na weka masikioni usikilize. Wakati watu wanafuatilia udaku, na habari nyingine zisizo na maana wewe unapata maarifa unayoweza kutumia kwenye kazi zako, biashara zako na hata maisha yako kwa ujumla. Sasa hebu niambie ukienda hivi kwa mwaka mmoja, utaendelea kuwa sawa na wale wasiojifunza kabisa? Haiwezekani, utakuwa mbali sana.
Karibu leo upate memory card namba tatu ambayo ina vitabu vizuri vitakavyokupatia mtazamo tofauti kabisa wa maisha.
VITABU VILIVYOPO KWENYE AUDIO BOOKS CARD 3
1. The 7 Habits Of Highly Effective People – Steven Convey
Hapa utajifunza tabia saba za watu wenye ushawishi mkubwa na mafanikio pia. Unataka kufikia mafanikio makubwa? Fanyia kazi tabia hizi saba.
2. Donald Trump – Never Give Up
Katika kitabu hiki bilionea mwekezaji kwenye majengo Donald Trump anatushirikisha mbinu alizotumia yeye kutoka kwenye madeni mpaka kufikia kuwa bilionea kwa kuwekeza kwenye majengo, tena bila hata ya kuanza na fedha zake mwenyewe. Sikiliza kitabu hiki.
3. Anthony Robbins – Time of Your Life
Ningekuw ana muda ningefanya hiki, ningefanya kile na kadhalika. Hizi ni kauli maarufu sana kwa watu wengi. Anthony Robbins anakuambia una muda mwingi kuliko unavyofikiri. Muda huo uko wapi? Pata memory card na usikilize kitabu hiko.
4. Your Right To Be Rich – Napoleon Hill
Unafikiri wewe huna haki ya kuwa tajiri? Unakosea sana, haki yako ipo, sema hujaijua ili uweze kuidai na kuisimamia. Napoleon Hill anakupa haki yako kwenye kitabu hiki.
5. Rich Dad’s Guide to Investing – Robert Kiyosaki
Kama mpaka sasa hujaanza kuwekeza, upo kwenye hatari kubwa. Kama utapita siku ya leo bila ya kujifunza kitu kuhusu uwekezaji na kukifanyia kazi, hakuna kitakachokusaidia wkenye dunia hii. Robert Kiyosaki anakupatia muongozo mzuri sana wa uwekezaji kwenye kitabu hiki, ni wewe kusikiliza tu.
6. Guide to Becoming Rich – Robert Kiyosaki
Robert kiyosaki na hapa tena anaendelea kukupa mbinu nzuri za kuweza kufikia utajiri. Haihitaji uibe au udhulumu, haihitaji uende kwa mganga, bali inahitaji wewe kujua misingi na kuifuata, na utajiri unakuja wenyewe.
7. 177 Mental Toughness Secrets of the World Class – Steve Siebold
Kuna tofauti kubwa sana ya kimawazo kati ya watu waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa. Steve Siebold anakupa siri 177 za watu waliofanikiwa sana ambazo watu wasiofanikiwa hawazijui. Unataka kuzijua? Pata kadi hii na sikiliza hiko kitabu.
8. Lessons from the Richest Man Who Ever Lived – Steven K. Scott
Kitabu hiki kina masomo muhimu sana kuhusu maisha na mafanikio kutoka kwa mtu tajiri sana aliyewahi kuishi na pia mtu mwenye busara sana kuwahi kutokea. Huyu ni mfalme Selemani. Steven Scott amekuchambulia siri muhimu za maisha kutoka kwenye maandiko ya Mfalme Selemani, nakusihi sana, usiache kusikiliza kitabu hiki. Yaani ni tuisheni kamili ya maisha, sio mafanikio na utajiri tu.
9. Neil Cavuto – Your Money Or Your Life
Maisha ni kuchagua na kila unachochagua kila siku kinakupeleka kwenye umasikini au kwenye utajiri. Sikiliza kitabu hiki ufanye maamuzi yatakayokupeleka kwenye utajiri.
10. Anthony Robbins – Power To Influence
Mafanikio yako kwenye kazi, biashara na hata maisha kwa ujumla yatatokana na jinsi unavyoweza kushawishi wale watu ambao ni muhimu kwako. Utamshawishije mteja anunue? Utamshawishije boss akuongeze mshahara? Anthony Robbins anakupa mbinu hizo, utazisikiliza hapa.
11. Anthony Robbins – Personal Training System
Kutengeneza mkakati wa kubadili maisha yako sio kitu rahisi. Anthony anakupa mfumo mzuri utakaoweza kuutumia kujifunza na kubadili maisha yako. Utasikiliza na kujifunza hapa.
12. David Bach-The Automatic Millionaire
David Batch anakupa siri ambazo zitakuwezesha wewe kufikia utajiri hata kama unapata kipato cha kawaida. Anakupa siri ambayo watu wengi wameitumia kufikia utajiri kwa kufuata misingi mizuri na kwa muda mrefu. Kama hutaki misukosuko ya kibiashara, unapenda kuendelea na kazi ya kuajiriwa lakini pia ufikie utajiri basi sikiliza kitabu hiki.
Sina mengi ya kuongeza hapo, elimu kubwa sana ipo kwenye vitabu hivyo kumi na mbili, ni wewe kujipatia kadi yako na kila siku kusikiliza vitabu hivyo.
Kadi inapatikana kwa gharama ya tsh elfu thelathini(30,000/=), na kama upo mkoani utaongeza fedha ya nauli na utatumiwa ulipo. Nauli inakuwa tsh elfu kumi(10,000/=).
Kupata kadi hii tuma fedha kwenye namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha utaandaliwa kadi na kupewa au kutumiwa. Kama upo dar tuma tsh elfu 30, kama mkoani tuma tsh elfu 40. Tuma fedha na maelezo kisha utapatiwa kadi yako.
Kujifunza kila siku ndio hitaji la chini kabisa la wewe kufikia mafanikio makubwa. Vitabu vya kusikiliza ni njia rahisi sana kwako kujifunza hata kama huna muda. Unasubiri nini? Pata kadi yako sasa ili uendelee kujifunza na uboreshe maisha yako.
Kuna memory kadi nyingine mbili zimewahi kutolewa kipindi cha nyuma na zina vitabu vizuri sana. Kuzipata bonyeza maandishi haya.
JIFUNZE, JIFUNZE, JIFUNZE,
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani.
makirita@kisimachamaarifa.co.tz