Mtu akishatoa sababu kama hiyo jua kabisa hayupo tayari kwa ajili ya mafanikio.

Kwamba mtu akipata muda atafanya kitu ambacho ni muhimu kwake. Labda pia kitu hiko sio muhimu.

Ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye atapata muda zaidi ya alionao sasa. Hakuna mtu anayeweza kutengeneza muda. Tutaendelea kuwa na haya masaa 24 kwa siku.

HABARI ZA KUSIKITISHA NILIZOPOKEA NI KWAMBA HAKUNA HATA DAKIKA MOJA ITAONGEZWA KWENYE MUDA TULIONAO SASA. UTUMIE VIZURI.
HABARI ZA KUSIKITISHA NILIZOPOKEA NI KWMABA HAKUNA HATA DAKIKA MOJA ITAONGEZWA KWENYE MUDA TULIONAO SASA. UTUMIE VIZURI.

Hivyo ili kufanya kile ambacho ni muhimu kwako husubiri kupata muda, bali unatenga muda. Ili kutenga muda inabidi uache kufanya vitu unavyofanya kwa sasa, ambavyo sio muhimu kama hiko ambacho unataka kufanya.

Hivyo basi kuliko kutudanganya kwamba ukipata muda utakuwa unajisomea, kwa nini usituambie ukweli kwamba kuangalia tv ni muhimu kwako kuliko kusoma? Kuliko kutudanganya kwamba ukipata muda utaanza kuboresha kazi zako kwa nini usituambie kwamba kupoteza muda kwako ni muhimu kuliko kuboresha kazi yako?

Ili ufanye kitu kipya kwenye maisha yako, unahitaji kuacha kufanya kitu ulichokuwa unafanya zamani. Husubiri upate muda, bali unatenga muda katika huu ulionao sasa.

Swali ni je mabadiliko unayohitaji kwenye maisha yako ni muhimu kuliko vitu ambavyo unafanya sasa? Jibu ni ndio na unafanya mabadiliko au hapana na unaendelea kufanya ulichozoea kufanya. Maisha ni yako chaguo ni lako.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba nimekuwa najidanganya kwamba nikipata muda nitafanya vitu ninavyotaka kufanya ili kuleta mabadiliko kwenye maisha yangu. Ukweli ni kwamba sitapata muda zaidi ya huu nilionao sasa. Ili nifanye kitu kipya ni lazima niache kufanya kitu cha zamani. Nitaacha kufanya vitu vyote ambavyo sio muhimu kwangu ili nitenge muda wa kufanya vitu ambavyo ni muhimu.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.