Unahitaji Kitu Hiki Kwanza, Ili Kujihakikishia Mafanikio Ya Kudumu Katika Maisha Yako.

Kwa watu wengi huwa ni rahisi sana kujua ni wapi wanapotoka katika safari yao ya mafanikio, lakini huwa si wepesi sana wa kutambua kule wanakokwenda kutokana na kutokuwa na uhakika kama watafanikiwa au la na kinachobakia kwao, huanza kutegemea zaidi bahati na mambo mengineyo ambayo wanakuwa wakiyafikiri yatawafanikisha.
Bila shaka umeshawahi kukutana na watu wa aina hii katika maisha yako. Ni watu ambao mara nyingi ili kuwatambua angalia maisha wanayoishi. Watu hawa maisha yao yametaliwa na malalamiko mengi na manung’uniko ya kila aina iwe kulalamikia mfumo au bosi wao na wakati mwingine hata mambo ambayo wenyewe wanaweza kuyabadilisha.
Je, wewe binafsi umeshawahi kujiuliza ni miongoni mwa watu hawa ambao hawana uhakika sana na maisha yao ya kesho ya kimafanikio? Nikiwa na maana umekuwa ukiishi kwa kubahatisha kiasi cha kwamba ukiulizwa leo, baada ya miaka mitano utakuwa nani ama utawa upo ngazi ipi kimafanikio unakuwa hujielewielewi na huna uhakika wa majibu yako?
Kama jibu ni ndiyo kwako, tena ulishawahi kujiuliza utafanyaje ili kuweza kujua namna maisha yako yatakavyokuwa  kwa baadae. Pengine unaweza ukabisha na kukataa kwa nguvu zako zote kuwa haiwezekani, lakini ninachotaka kukwambia, hilo linawezekana kwako ukaelewa maisha yako yatakuwa vipi baada ya muda fulani kupita.

Hili ni zoezi dogo, naliita dogo ni kwa sababu halihitaji uwe umeenda digirii ya uchumi wala halihitaji uwe na hirizi ama miujiza kama unavyofikiri. Unachotakiwa kuwa nacho nikitu kimoja tu ambacho ni ufahamu ulionao tena wa kawaida tu na kuamua kukubali na kuufuata ukweli halisi bila ya kuukwepa. 
Ni rahisi sana kwako kuhoji ‘Aaah Imani hili linawezakana vipi’? ninachotaka kukwambia  linawezeka tena sana tu, ikiwa wewe  leo hii utaamua kuwa makini na mipango endelevu  uliyojiwekea katika maisha yako. Hii ikiwa na maana kuwa nguvu na mawazo yako ni lazima kwanza yaelekezwe kwenye mipango yako endelevu ili kujihakikishia mafanikio ya kudumu  katika maisha yako.
Hiki ni kitu muhimu sana kutambua kwani bila kuwa makini na mipango endelevu uliyojiwekea hiyo itakuwa ni ngumu sana kwako kufanikiwa hata uwe na kipaji au pesa nyingi hivyo vyote haviwezi kukusaidia zaidi ya umakini wako katika mipango endelevu uliyojiwekea bila kukosa.
Watu wote wenye mafanikio makubwa na mataifa yote yaliyoendelea huwa ni makini katika hili. Huwa hawachezi na mipango endelevu kwa namna yoyote ile. Ni watu ambao huwa ni ving’an’anizi, wabishi ambao kwa vyovyote vile huwa na shauku ya kutaka kuona ndoto zao zinatumia na si kuishia hewani. Hiki pia ndicho kitu ambacho unatakiwa kuwa nacho hata wewe ili kujihakikishia mafanikio ya kudumu katika maisha yako.
Kuwa makini katika mipango endelevu katika maisha yako ni kitu cha msingi sana kwako. Bila mipango hiyo hakuna utakachoweza kukiendeleza au kukibadilisha kwa sehemu kubwa. Unapokuwa na mipango hiyo hata pale unaposhindwa kwa namna moja au nyingine inakuwa ni rahisi sana kwako kuweza kujipanga upya tena kwa sababu una mipango endelevu ya kimafanikio isiyo na kikomo.
Amua kubadilisha maisha yako leo kwa kuwa na mipango endelevu ya kimafanikio ambayo utahakikisha ni lazima ikufikishe kwenye kilele cha mafanikio. Inawezekana ukawa huna pesa, maisha yako ni magumu na huna uhakika wa kufanikiwa hilo lisikutishe sana kikubwa jiwekee mipango endelevu kwa kuamua kuwa ni lazima nitabadilisha maisha yangu hatua kwa hatua hata iweje, hicho ndicho kitu kitakachokuokoa na ugumu huo wa maisha.
Utakapojiamisha wewe mwenyewe na kuamua kubadili maisha yako hatua kwa hatua,  hapo ndipo utakuwa umejiwekea mipango endelevu ya kubadilisha maisha yako bila kujua na isitoshe uwe na uhakika kuna nguvu fulani ambayo utaipata ndani yako ambayo itakuwa inakupa msukumo na hamasa ya kutenda zaidi kuliko kawaida.
Kiuhalisia, kama nilivyoanza kusema awali unahitaji kwanza mipango endelevu ya kimaisha ili kujihakikishia mafanikio ya kudumu katika maisha yako. Hata pale tunapochoka kwa kukosa hamasa, kukatishwa tamaa, au kukosolewa sana haina haja ya kusimama ni lazima tusonge mbele hadi kufanikiwa hata iwe hali ngumu vipi, kwa sababu ndani yetu tuna mipango endelevu.
Huna haja ya kulalamika tena kuwa maisha yako ni magumu ama hujiwezi. Ili kutoka katika hali hiyo fanya uamuzi wa kuwa na mipango endelevu ya kubadilisha maisha yako hatua kwa hatua bila kuchoka. Hicho ndicho kitu unachotakiwa kukizingatia sana na kukifuata mpaka ndoto zako zitimie.
Tunakutakia ushindi mkubwa katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kujifunza kila siku.
Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kuboresha na kubadilisha maisha yako.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048 035,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: