Sheria 6 Za Mafanikio Na Jinsi Zinavyoweza Kukuongoza Kufikia Mafanikio Makubwa.

Wakati mwingine katika maisha huwa tujikuta ni watu wa kukosa mwelekeo wa kule tunakotaka kufika  pengine kwa sababu ya kutokuwa na mwongozo au sheria sahihi za kutufikisha huko. Ni sheria hizihizi ambazo kila mmoja wetu hulazimika kuzijua ili kufikia viwango vya juu vya mafanikio. Sheria hizi huwa zipo hata kama hujui na zinafanya kazi kwa saa zote ishirini na nne kila siku.
Kwa wale wanaomudu kutumia sheria au kanuni hizi hujikuta ni watu wa mafanikio zaidi, kuliko wanaoshindwa kuzitumia kabisa. Katika makala hii utajifunza kwa uchache baadhi ya sheria ambazo zinaweza kukuongoza kufikia mafanikio makubwa  ikiwa utazitumia kwa sahihi. Je, unajua ni sheria zipi ziazoweza kukuongoza kufikia mafanikio makubwa katika maisha yako?
Hizi Ndizo Sheria 6 Za Mafanikio Na Jinsi Zinavyoweza Kukuongoza Kufikia Mafanikio Makubwa.
1. Sheria ya uwajibikaji.
Maisha yako yatakuwa bora zaidi, pale utakapotambua kuwa wewe ndiye unayewajibika katika maisha yako kwa kila kitu. Hutakiwi kulaumu mtu, serikali, wazazi, bosi wako au kitu chochote kuwa ndicho kimekukwamisha.  Tambua wewe ndiye kiongozi pekee wa maisha yako unayewajibika kwa kila kitu. Wewe ndiye unayetakiwa kuitawala kesho yako kwa kufanya mambo yako kwa usahihi hadi kufikia mafanikio makubwa. Kwa kutumia sheria hii ya uwajibikaji uwe na uhakika na mafanikio yako.

2. Sheria ya vitendo.
Hakuna utakachoweza kukifanikisha vizuri katika maisha yako ikiwa utashindwa kutumia sheria hii vizuri. Hii ni sheria inayokutaka ni lazima uwe utakuwa mtu vitendo ili kufaniwa. Mafanikio yote makubwa yanapatikana kwa kwa wale ambao ni watu wa vitendo. Kama utakuwa ni mtu wa kuahirisha mambo yako kila mara mafanikio kwako ni rahisi kubaki kuwa hadithi. Ili uweze kufanikiwa ni muhimu kuitambua sheria hii na kuifanyia kazi kila siku na maisha yako yatabadilika.
3. Sheria ya ung’ang’anizi.
Mafanikio makubwa utayapata tu ikiwa wewe ni king’ang’azi wa mipango na malengo yako mpaka kuyatimiza. Katika maisha kuna mambo mengi ambayo huwa yanatokea na kutukatisha tamaa sana. Bila kutumia sheria hii ya kung’ang’ania ni rahisi sana kurudi nyuma na kukata tamaa na kuachana na ndoto zako. Kitu unachotakiwa kujua ni kutambua umuhimu wa kung’ang’ania mafanikio yako mpaka yatimie na siyo vinginevyo.
4. Sheria ya uzingativu.
Ili uweze kufanikiwa katika jambo lolote kwa asilimia mia moja, unalazimika kuweka nguvu zako za uzingativu katika jambo moja unalolifanya kwa sehemu kubwa. Unapoweka nguvu za uzingativu, hapo ndipo unajikuta wewe mwenyewe unakuwa unatumia sheria hii ya nguvu ya uzingativu kukusaidia kufanikiwa. Mara nyingi matokeo chanya hutokea pale nguvu ya uzingativu inapotumika. Mawazo kama mawazo yanakuwa yana nguvu kubwa sana ya kuumba au kukupa kile unachokitaka pale yanapotumika pamoja kuliko unavyofikiri.
5. Sheria ya kuamini inawezekana.
Kujiamini ni moja ya nguzo kubwa sana ya mafanikio kwa binadamu yoyote yule. Kama unataka kufanikiwa jenga uwezo mkubwa sana wa kujiamini ndani mwako na amini hilo linawezekana. Kwa kadri unavyoitumia sheria hii ya kuamini inawezekana katika kile unachokifanya, utaona mwenyewe jinsi ambavyo mambo yako mengi utakuwa ukiyafanikisha. Jipe moyo na muda kila kitu kinawezekana kwako kwa kutumia sheria hii muhimu kwako.
6. Sheria ya mtazamo.
Maisha uliyonayo yawe ya mafanikio au kushindwa yanategemea sana juu ya mtazamo ulionao. Tunapotumia sheri hii ya mtazamo inatufundisha kuwa ili tuweze kufanikiwa ni lazima kwetu sisi tuwe na mitazamo sahihi ya kimafanikio. Mafanikio yatakuwa upande wetu kama fikra zetu tumezijaza mambo mengi ya kimafanikio na kuwa na mitazamo sahihi inayoendana na kile tunachokitaka katika maisha yetu. Hii ndiyo siri iliyopo kwenye sheria hii ya mtazamo.
Kumbuka maisha yanaongozwa na kanuni au sheria, kwa kuzijua sheria hizo inakuwa ni rahisi kwako kukuwezesha kufikia mipango na malengo makubwa uliyojiwekea, ikiwa utazifanyia kazi katika maisha yako.
Tunakutakia maisha mema yawe ya mafanikio makubwa kwako.
Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza zaidi kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048 035,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: