SEMINA; MIMI NI MSHINDI (Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu)

Habari za leo rafiki? Naamini uko vizuri na unaendelea kufanyia kazi yale unayojifunza na maisha yako yanaendelea kuwa bora. Hongera sana kwa hilo.
Na kama bado hujaanza kufanyia kazi, au unafanyia kazi lakini huoni mabadiliko, endelea kuweka juhudi, usikate tamaa. Maarifa unayopata kupitia AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA ni maarifa yanayofanya kazi kwa kila anayeyatumia sawasawa.
Leo nina habari njema sana kwako rafiki yangu wa karibu. Ni kwamba AMKA CONSULTANTS tunakuletea semina ya tatu na ya mwisho kwa mwaka huu 2015 kwa njia ya mtandao. Mpango wetu kwa mwaka huu ulikuwa kuendesha semina nne, tatu kwa njia ya mtandao na moja kwa njia ya mkutano, yaani live.
Tayari tumeshatoa semina mbili kwa njia ya mtandao ambazo zimekuwa na mafanikio makubwa sana kwa washiriki. Semina ya kwanza ilikuwa mwezi wa kwanza na ilikuwa ni SIKU 21 ZA MAFANIKIO. Semina ya pili ilikuwa mwezi wa tano na ilikuwa ni MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA na sasa tunakuletea semina ya tatu ambayo ni MIMI NI MSHINDI. Semina ya nne itakujia mwishoni mwa mwaka huu, endelea kuwepo hapa na utapata taarifa zote.

MIMI NI MSHINDI.

 
MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.
Hii ni semina kwa njia ya mtandao ambayo itakukumbusha kitu muhimu sana kwenye maisha yako. Kwamba wewe ni mshindi na una kila unachohitaji kushinda. Kinachokuzuia mpaka sasa ni kukosa maarifa sahihi na kuzungukwa na jamii ambayo inakulazimisha kwamba huwezi tena kushinda.
Huu ni uongo wa hali ya juu sana na umekufanya uishi maisha ambayo sio stahili kwako. Kupitia semina hii utaweka ahadi yako na nafsi yako ambayo itakuwezesha kushinda.
Nini kipya kwenye semina hii, si yale ambayo tunajifunza kila siku?
Semina hii ina mambo mengi sana mapya. Pamoja na haya unayojifunza kila siku, hapa kuna mbinu za tofauti za kuhakikisha kwamba unaishi ule ushindi uliopo ndani yako.
Kitu kikubwa sana ambacho hujawahi kupata kwenye semina nyingine ni kwamba mimi sitakufundisha, bali utakuwa unajipa ahadi wewe mwenyewe. Jinsi masomo ya semina hii yalivyoandaliwa ni kwamba utakuwa unajiambia ni kipi ambacho unafanya. Sio mimi nakwambia WEWE NI MSHINDI, bali wewe unajiambia mwenyewe MIMI NI MSHINDI. Na masomo yote kwenye semina hii yamekaa kwa muundo huo.
Kwa hiyo hii inakuwa ni ahadi ya kweli na nafsi yako, unajiambia mimi ni mshindi, hii ina nguvu zana kuliko kuambiwa wewe ni mshindi
MUUNDO WA SEMINA HII;
Semina hii itaendeshwa kwa mwezi mmoja, mwezi huu wa kumi.
Semina itaanza jumatatu ya tarehe 05/10/2015 na kumalizika ijumaa ya tarehe 30/10/2015.
Semina hii itakuwa na mafunzo 20 ambapo somo moja litatumwa kila siku kwa siku tano za wiki. Siku za mwisho wa wiki zitakuwa za kuuliza na kujibu maswali.
Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao, email, kundi la wasap na kutumiwa ujumbe mfupi.
Kwa kujiunga na semina hii;
Kila siku ya semina utatumiwa email yenye mafunzo ya semina ikiwa na hatua za kuchukua pia.
Utapata nafasi ya kuwepo kwenye kundi la wasap, ambapo utaweza kusoma masomo haya kwenye simu yako na pia kupata nafasi ya kushiriki mijadala inayoendana na hiki tunachojifunza.
Kila siku asubuhi utapata ujumbe mfupi kwenye simu yako ya mkononi ukikupa mbinu za ushindi na kukumbusha kwamba wewe ni mshindi.
Utaweza kuwasiliana nami, na hata kuuliza maswali na kujibiwa wakati wowote wa kipindi hiki cha semina.
Yafuatayo ni masomo yaliyopo kwenye semina hii;
SEMINA; MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.
1. Nilizaliwa kushinda.
2. Maisha yangu ni jukumu langu.
3. Ninaamini ninaweza kushinda.
4. Ninapima ushindi wangu kwa malengo.
5. Mimi kama mshindi ni mwaminifu.
6. Nimejitoa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.
7. Muda ni mali ya thamani kwangu.
8. Nimezishinda hofu zote.
9. Kujifunza kila siku ndiyo nguzo yangu.
10. Nimeacha kutafuta sababu.
11. Wakatishaji tamaa hawaniyumbishi.
12. Ninafanya kile nilichopanga kufanya leo.
13. Kukosea ni sehemu ya ushindi wangu.
14. Ninakazana kuwa bora na sio kuwashinda wengine.
15. Ninajua hakuna njia ya mkato.
16. Kulaumu na kulalamika ni mwiko kwangu.
17. Mimi ni king’ang’anizi, sikubali kukata tamaa.
18. Ninashukuru kwa maisha haya ya ushindi.
19. Ninashirikiana na washindi wenzangu.
20. Ninachukua hatua mara moja.
Masomo haya 20 yameandaliwa vizuri sana kiasi kwamba kadiri unavyokwenda unaendelea kuvunja minyororo yote ambayo inakuzuia kufikia mafanikio. Kumbuka mabadiliko ya kweli kwenye maisha yako yanaanza na wewe mwenyewe, na ndio maana mafunzo haya yameandaliwa ili kukuwezesha wewe mwenyewe kubadilika, kujiahidi kwamba utashinda na baadae utashinda kweli.
CHETI CHA AHADI.
Ili kuongeza na kuweka msisitizo zaidi kwenye ahadi hii, baada ya mafunzo haya tutaandaa vyeti maalumu vya wewe kujiahidi mambo haya muhimu. Utaweka sahihi kwenye cheti hiko na kukiweka mahali ambapo kila siku unaweza kukiona na kujikumbusha kwamba wewe ni mshindi na ni mambo gani unafanya kama mshindi.
Yaani nakuhakikishia, kama utajiunga na mafunzo haya, na kuyafanyia kazi, na ukapata cheti hiki ambacho kitakuwa kinakukumbusha kila siku, hakuna kitu chochote, narudia tena, HAKUNA KITU CHOCHOTE kinachoweza kukuzuia wewe kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
GHARAMA ZA SEMINA HII.
Kwa yote haya mazuri upo tayari kulipia kiasi gani cha fedha?
Hakuna thamani unayoweza kuweka kwenye mafunzo haya, yana thamani kubwa sana ambayo huwezi kuitathmini kwa viwango vya fedha. Lakini kwa sababu wewe ni rafiki yangu, na lengo langu ni kukuona wewe unafanikiwa, utachangia mchango mdogo wa kuhakikisha semina hii inaweza kuendeshwa.
Na mchango huo utakuwa tsh elfu 30(30,000/=) kwa mafunzo ya semina. Kwa wale watakaotaka kupata vyeti vya kumbukumbu ya ahadi yao wataongeza gharama kidogo za kupata cheti kile, tutajuzana baadae.
Hii ni gharama ndogo sana ambayo huwezi kuipata kwa mafunzo kama haya ambayo utayapata.
KUJIUNGA NA MAFUNZO HAYA.
Ili uweze kushiriki mafunzo haya, unahitaji kujiunga kwa kujaza taarifa zako na kisha kulipia ada ya mafunzo.
Kujiunga na kulipia kumefunguliwa leo tarehe 18/09/2015 na mwisho wa kujiunga na kulipia itakuwa tarehe 02/10/2015. Baada ya hapo hutakuwa tena na nafasi ya kujiunga.
Ili kuhakikisha washiriki wanapata mafunzo bora, nafasi za ushiriki huwa zinakuwa chache. Hivyo ni vyema ukachukua hatua haraka.
Kujaza taarifa zako bonyeza maandishi haya na malipo fanya kwa namba zifuatazo; M PESA 0755 953 887, TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253.
Chukua hatua haraka kabla nafasi hii ya kipekee haijakupita.
Nakukaribisha sana kwenye mafunzo haya ambayo ninaamini bila ya kusita kwamba yatabadili maisha yako. Nimejitoa kuweka kila ninachojua kwenye mafunzo haya ili yawe msaada mkubwa sana kwenye maisha yako, usijaribu kabisa kuyakosa.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
P.S Kama bado hujajaza fomu ya kujiunga bonyeza maandishi haya sasa na ujiunge na mafunzo haya mazuri.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: