USHAURI; Mambo Ya Kuzingatia Pale Kila Biashara Unayoanzisha Inakufa.

MUHIMU;
Tarehe 05/10/2015 itaanza semina muhimu na ya mwisho kwa mwaka huu kwa njia ya mtandao. Semina hii inakwenda kwa jina MIMI NI MSHINDI, na utajifunza mambo yote muhimu unayotakiwa kujua na kufanyia kazi ili uwe mshindi wa kweli kwenye maisha yako. Semina hii itaendeshwa kwa njia ya email, kundi la wasap na kutumiwa ujumbe wa simu. Usipange kabisa kukosa semina hii. Pia jiunge mapema kabla nafasi hazijajaa. Fungua hapa kupata taarifa na kujiunga; SEMINA; MIMI NI MSHINDI (Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu)

Karibu tena mpenzi msomaji kwenye kipengele chetu kizuri cha ushauri wa changamoto ambazo zinatuzuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yetu. Wote tunajua ya kwamba hakuna kinachokosa changamoto na hivyo lengo letu kubwa sio kuzikimbia bali kuweza kuzitatua. Na ndio maana kupitia hapa tunapeana mbinu hizi za kutatua changamoto.


KUPATA KITABU HIKI KIZURI BONYEZA MAANDISHI HAYA.

 
Leo katika kipengele hiki tutaangalia changamoto ya kuanzisha biashara na hatimaye zinakufa. Kuna watu wengi sana ambao wamekuwa wakikazana kuanzisha biashara lakini biashara hizo zinakufa. Wanajaribu kuanzisha nyingine tena nazo zinakufa.
Kabla hatujaangalia ni kitu gani cha kufanya, tupate maoni ya msomaji mwenzetu aliyetuandikia kuhusiana na changamoto hii;

Biashara Kila Nikianza Inakufa Baada Ya Miezi 6 Kwa Kukosa Wateja Hii Ni Changamoto Inayonisumbua Sana Nimefilisi Mara Kadha Na Kukosa Rejesho La Bank. M.O

Kama tulivyosoma maoni ya msomaji mwenzetu hapo juu, yeye na wengine wengi kama yeye wamekuwa wanakutana na changamoto hii ambayo inawarudisha nyuma.
Inaumiza sana pale ambapo unajinyima na kuanzisha biashara au hata unachukua mkopo benki na kuja kuweka kwenye biashara ukitegemea kupata faida ila mwisho wake unapata hasara na kufunga kabisa.
Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia pale unapoanzisha biashara halafu zinakufa.
1. Fanya utafiti wa kutosha kabla hujaingia kwenye biashara.
Usianze biashara kwa sababu watu wanakuambia biashara fulani inalipa. Usiingie kwenye biashara kwa sababu umeona watu wengine wanafanya biashara. Kaa chini na jua ni biashara gani unafanya kutokana na mazingira uliyopo, kisha fanya utafiti wa kutosha juu ya biashara hiyo.
Jua ni wateja kiasi gani wanapatikana, jua ni gharama kiasi gani utaingia kuendesha biashara, jua kuna watu wangapi wanaofanya biashara kama unayokwenda kufanya wewe. Na pia jua ni kitu gani cha ziada na cha tofauti ambacho unacho wewe ukilinganisha na wafanyabiashara wengine ambao wanafanya biashara hiyo.
2. Usianze biashara usiyoijua kwa mkopo wa benki.
kama tulivyoona kwa msomaji mwenzetu hapo, alitumia mkopo wa benki kuanzia biashara na mwishowe akashindwa kufanya marejesho. Ni hatari sana kuchukua mkopo benki na kwenda kuanza nao biashara, ambayo hata hujaifanyia utafiti wa kutosha.
Kama kuna biashara ambayo umeona unaweza kufanya, ijue vizuri kisha anza kidogo kwa mtaji ambao umejikusanyia wewe mwenyewe. Utakapoijua biashara hiyo vizuri na kujua ni eneo gani linaloleta faida ndio unaweza kuchukua mkopo na kuweka kwenye eneo hilo.
Kuanza biashara yeyote mpya ni majaribio ya kujifunza, mwanzoni utakutana na changamoto nyingi. Ni hatari kutumia fedha ya benki ambayo unailipia riba katika majaribio ya biashara.
3. Ifuatilie biashara kwa makini, ijue nje ndani.
Biashara huwa haifi siku moja, kabla biashara haijafa kuna dalili nyingi sana ambazo zinaonekana. Kama upo makini na biashara yako na unaijua vizuri utaona dalili hizo na kuchukua hatua mapema. Ila unapokuwa hujui biashara inaendaje, huwezi kuona dalili za biashara yako kufa mapema na hivyo utashangaa inafika siku biashara haiwezi kwenda tena.
Fuatilia kwa makini mwenendo wa biashara yako, na chukua hatua mapema pale unapoona mabadiliko.
Sasa hayo ni mambo ya kuzingatia ili biashara isife. Ila inapokufa ni hatua gani unachukua?
Pale biashara yako imekufa na unataka kuingia kwenye biashara nyingine, kabla ya kufanya hivyo kuna mambo muhimu sana ya kuzingatia.
Na mambo haya yameandikwa vizuri sana kwenye makala ya biashara inayopatikana kwenye mtandao wa NAPENDA BIASHARA. Kusoma makala hiyo nzuri bonyeza maandishi haya; Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Kabla Hujatoka Kwenye Biashara Iliyoshindwa Na Kuingia Kwenye Biashara Mpya.
Fanyia kazi mambo hayo uliyojifunza ili uweze kuendesha bishara yenye mafanikio.
Nakutakia kila la kheri kwenye mafanikio ya biashara yako.
TUPO PAMOJA.
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: