Mambo Matano Muhimu Kuhusu Mafanikio Niliyojifunza Kutoka Kwa Mwalimu Mstaafu.

Habari mpenzi msomaji wa mtandao huu wa Amka Mtanzania?
Karibu tena tujifunze katika makala yetu ya leo. Katika mwezi huu wa tisa nilipata nafasi ya kumtembelea mwalimu mstaafu wa shule ya msingi. Mwalimu huyu alinivutia kwa mambo aliyoyafanya na mimi nikapata hamasa kutoka kwake nikaona ni vema nikushirikishe na wewe ndugu mpenzi msomaji. Mwalimu huyu alistaafu rasmi kazi yake ya ualimu mwaka 2014 alinieleza kwamba baadhi ya walimu wastaafu wenzake anaowafahamu wengi sasa wamepoteza dira ya maisha hii ni kwa sababu walishazoea maisha ya kupokea kila mwisho wa mwezi sasa hawapati na hawana kitu cha kuwaingizia.
Kweli maisha yanatengenezwa angali uko kazini au kijana na maisha hayatengenezwi baada ya kustaafu unatakiwa kuyaandaa sasa hivi. Kila mfanyakazi inampasa atengeneze maisha yake ya kustaafu leo, atengeneze falsafa yake ya tatu katika maisha yake yaani maisha yake yatakuwaje hapo baadae wakati huna nguvu tena ya kufanya kazi.
Mazoea ni mabaya sana kama ulikuwa umezoea kupata kila mwisho wa mwezi na sasa hupati tena utachanganyikiwa kisaikolojia na kudhoofika kiafya. Kwa hiyo usiridhike na kipato unachopata sasa kuna kipindi kitafika huna budi kupumzika na kama ulikuwa ni mtu wa kutumia tu bila kuwekeza ndio matatizo yanapoanzia hapo. Wengi wanajisahau wanapokuwa kazini na akili inakuja kuamka tayari wakati muda umewaacha hawana nguvu tena ya kuzalisha.

 
Kila mtu ana uwezo wa kutengeneza maisha yake sasa hivi na siyo baadae. Uhuru wa kifedha unaanza kutengenezwa leo na siyo kesho na kumbuka mafanikio ni safari usitegemee hela utakayolipwa baada ya kustaafu ndio itakuletea mafanikio na kufuta shida zako zote.
Mambo niliyojifunza kwa mwalimu mstaafu wa shule ya msingi;
1. Alikuwa Mtu Anayeweka Akiba; kutokana na mazungumzo yetu mwalimu huyu aliniambia kuwa yeye alikuwa ni mtu wa kuweka akiba ndio maana maisha yake ya sasa anayafurahia ukilinganisha na walimu wenzake aliokuwa anafanya nao kazi. Akiba ni tairi la ziada katika safari yako ya mafanikio hivyo kila mtu anatakiwa kuweka akiba bila kujali kipato, anza na kuweka elfu moja kila siku utakuwa mbali sana tofauti na mtu ambaye haweki akiba nimetolea mfano elfu moja lakini weka kadiri ya kipato chako.
SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutajirika Kwa Kuanza Na Shilingi Elfu Moja.
2. Alikuwa Ana Wekeza (vyanzo vya mapato);
Mwalimu huyu ana vyanzo vya mapato zaidi ya kimoja na alianza kufanya hivi tokea yuko anafanya kazi yake ya ualimu kwa sasa mwalimu huyu ana uhuru wa kifedha. Kwa hiyo ili ufikie mafanikio ya kifedha kuwa na vyanzo vingi vya mapato ndio utaweza kufikia uhuru wa kifedha usitegemee mshahara tu kuwa na kitu kingine pembeni tofauti na mshahara.
3. Anaishi Chini ya Kipato Chake;
Kulingana na maelezo yake mwalimu huyu mstaafu alikuwa anaishi chini ya kipato chake ndio maana ameweza kuwekeza sehemu mbalimbali. Kama unaishi maisha juu ya kipato chako ni ngumu kufikia mafanikio utakuwa unavutwa na matatizo mbalimbali haijalishi unapata kipato kikubwa kiasi gani lakini ishi chini ya kipato chako ili upate fursa ya kuwekeza zaidi.
4. Ana Nidhamu ya Maisha;
Mwalimu huyu anajituma mpaka sasa katika shughuli zake za ujasiriamali, shughuli nyingine za ujasiriamali watu wanamfanyia. Huwezi kufanikiwa bila watu ndio maana shughuli zake zingine watu wanamfanyia. Licha ya mwalimu huyo kustaafu bado anajituma kila siku hajaridhika na maisha. Kwa hiyo tunatakiwa kujituma kila siku bila kukata tama.
5. Ni Mjasiriamali Mzuri;
Sifa moja wapo ya mjasiriamali ni mtu ambaye haogopi changamoto. Kama unaogopa changamoto huwezi kufanikwa kwa sababu kila siku utaogopa kufanya jambo kubwa litakalokusaidia, tunatakiwa kujaribu bila kuogopa changamoto na ni muhimu kuona changamoto ni sehemu ya maisha ya kila siku kwa kufanya hivi utakuwa unathubutu kila siku bila kujali kukatishwa tamaa.
SOMA; Kama Una Tabia Hizi 30 Tayari Wewe Ni Mjasiriamali, Chukua Hatua.
Mwisho, tunapaswa kuandaa maisha yetu leo na siyo baada ya kustaafu na uhuru wa kifedha unaanza kutafutwa leo na mafanikio ni kama safari kwa hiyo anza safari yako leo ya kuelekea kufikia kwenye mafanikio. Tujifunze kila siku maarifa ndio kila kitu kwenye safari ya mafanikio.
Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: