Sababu 6 Zinazokufanya Ushindwe Kuchukua Hatua Mapema Za Kubadili Maisha Yako.

Kuna wakati unaweza ukajikuta unashindwa kubadili maisha yako sio kwa sababu huna malengo na mipango, bali ni kwa sababu ya kushindwa kwako kuchukua  hatua mapema za kubadili maisha yako. Kutokuchukua hatua mapema ni moja ya tatizo kubwa linalopelekea malengo yako mengi kutofanikiwa.
Ili uweze kufanikiwa na kufikia mafanikio makubwa ni lazima kujifunza kuchukua hatua mapema za kubadili maisha yako. Lakini hata hivyo pamoja na umuhimu huo, hili bado ni tatizo si kwako tu bali linawakabili wengi kushindwa kuchukua  hatua mapema. Kwa sababu hiyo malengo mengi yanakuwa yanashindwa kutumia.
 Je, unajua ni kitu gani au sababu zipi hasa zinakufanya ushindwe kuchukua hatua mapema za kubadili maisha yako?
1. Unafikiria kushindwa sana.
Kila unapowaza kufanya kitu kizuri cha kubadili maisha yako, ndani mwako unajijengea fikra za kushindwa. Unawaza sasa nikifanya hivi na nikishindwa itakuwaje? Kwa kifupi unakuwa mwoga wa kuchukua hatua za kubadili maisha yako sababu tu unaona utashindwa.
Ili uweze kuondokana na hali hiyo unalazimika kuwa na fikra chanya ambazo zitakupelekea wewe kutambua kuwa unatakiwa kuachana na fikra zako hizo ili kuweza kutimiza ndoto zako na kuachana na mawazo hayo ya kushindwa .
2. Unakosa sana kujiamini.
Hiki ni kitu kingine kinachokugharimu na unajikuta unashindwa kuchukua hatua mapema. Nia ya kutaka kufanikiwa unakuwa nayo kweli, lakini unakuwa una sitasita sana kuchukua hatua kutokana na kukosa kujiamini. Kwa kutokujiamini tu ni sababu tosha inayokufanya ushindwe kuchukua hatua mapema juu ya maisha yako.
Kumbuka hakuna mafanikio  utakayoyaweza kuyapata kama hujiamini. Hivyo basi nguzo kubwa itakayokufanya wewe uweze kumudu kuchukua hatua mapema za kubadili maisha yako ni kujiamini. Hicho ndicho  kitu cha kwanza kuliko kitu chochote unachotakiwa ukielewe vizuri ili kukupa mafanikio.
3. Hutaki kujitoa mhanga.
Ili uweze kuishi maisha ya ushindi na mafanikio, kitu kikubwa unachotakiwa kukifanya katika maisha yako ni kuhakikisha unajitoa mhanga mpaka kutimiza mipango ya malengo yako. Tatizo kubwa linalosababisha unachelewa kuchukua hatua juu ya maisha yako ni kuogopa kujitoa mhanga au kulipia gharama za mafanikio hayo.
Kwa jinsi unavyochelewa kujitoa ili kujenga mafanikio unayoyataka, ndivyo ambavyo maisha yako yanazidi kuwa magumu. Hiyo yote ni kwa sababu hakuna hatua unayoichukua, kwani unakuwa unaishi maisha yaleyale siku zote.
4. Kufikiria umechelewa.
Inawezekana unakuwa mzito kuchukua hatua moja kwa moja za kubadili maisha yako pengine kwa kufikiri kuwa umechelewa kufanya hivyo. Ni mawazo yanayokujia pengine kutokana na kujiona kuwa tayari una majukumu mengi kama ya kifamilia na kuhisi kila kitu kimeharibika kumbe sivyo ndivyo.
Lakini ukweli wa mambo ni kwamba hujachelewa kama unavyofikiri. Unao uwezo wa kufanya madiliko ya maisha yako ukiamua. Tekeleza mipango yako kila siku na mwisho wa siku mafanikio unayoyatafuta utayaona. Acha kujijengea fikra hasi kama hizi  zitakukwamisha.
5. Kufikiria  mawazo mazuri tayari yameshafanyiwa kazi.
Hili linaweza likawa tatizo lingine linalokufanya ushindwe kuchukua hatua mapema za kubadili maisha yako. Kila wazo unalotaka kulifikiria unahisi tayari limeshafanyiwa kazi. Matokeo yake unajikuta unakuwa na mawzo mengi sana ambayo unakuwa unayachagua na kuyaacha  na kujikuta hufanyi kitu.
Kama kweli una nia ya kubadili maisha yako achana na hizo fikra zako. Mawazo hayohayo hata kama unaona yamefanyiwa kazi na wewe yaweke kwenye utendaji kwa upande wako. Hiyo itakupelekea malengo yako kuweza kutimia kuliko kuacha kila kitu.
6. Kuishi kwa mazoea.
Ni rahisi kushindwa kuchukua hatua mapema kutokana na kupenda kuishi kwa mazoea. Mazoea yako hayo yanakulazimisha sana kufanya mambo yaleyale siku zote na kushindwa kutumia fursa zingine kukufanikisha. Kw a sababu hiyo ndiyo inayokufanya ushindwe kuchukua hatua katika maisha yako mapema.
Kwa namna moja au nyingine hizo ndizo sababu zinapolekea mara nyingi ushindwe kuchukua hatua mapema za kubadilisha maisha yako.
Naomba nikutakie siku njema iwe ya mafanikio kwako na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kujifunza kila siku.
Kwa makala nyingine nzuri karibu pia katika DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na uhamasika.
 Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: