Siri Kubwa Ya Mafanikio: Fanya Kile Unachopenda Sana Na Sio Kinacholipa Sana

Habari za Jumapili msomaji wa Amka Mtanzania, ni siku nyingine tena tunaendelea kukumbushana mambo muhimu na kuzidi kufichua baadhi ya vitu ambavyo vimo ndani mwetu lakini hatujui kama vipo au hata kama tunajua tunaogopa kuchukua hatua sahihi.
Wengi wetu tunafanya kazi au shughuli mbalimbali ili kuwezea kujiongezea vipato ili kuweza kufurahia wakati wetu hapa duniani. Mara nyingi kigezo kikubwa ambacho tunatumia ni kuwa labda hiki ninachofanya kinaniingizia kipato kikubwa, pengine labda kwa kuwa hii kazi inanilipa vizuri ndio maana naifanya, na kwa kuwa mara nyingi tunakuwa tunafanya kwa ajili ya pesa nyingi basi unakuta mtu anatumai nguvu nyingi sana kuweza kufanya hicho kitu na wakati mwingine inaweza hata kutugharimu muda wa kufanya mambo mengine, kuna watu wanakosa hata muda wa kukaa na familia au hata kushiriki mambo mengine ya kijamii kwa kuwa tu inabidi uhakikishe unatumia akili na nguvu zako kufanya hiyo kazi kwa ufanisi ili kuendelea kulinda kile unapata.

 
Lakini kitu cha hatari zaidi, kwa kuwa tu ninachofanya kinanilipa vizuri basi najikuta natamani kila mtu afanye hiki , hapa kwa baadhi ya wazazi au walezi wamejikuta wanalazimisha watoto wao kusomea hata baadhi ya fani si kwa kuwa wanazipenda bali kwa kuwa wazazi wameona hizo ndio zinalipa kwa wakati huo bila kujali hata kama ndicho kitu mtoto anataka na anafurahia kufanya, naweza sema wazazi kuna wakati waweza tumika kumpoteza au kumchelewesha mtoto wako kufika pale anataka/takiwa kufika kwa wakati kwa kumfanya apite kule unataka wewe kwa faida yako. Lakini njia hii naweza sema imechangia sana kuleta aina ya watu/watumishi maofisini waliopo, hawapendi kazi wanazofanya, hawafurahii, wanaangalia pesa tu, hata kabla hajafanya kazi anataka alipwe kwanza, na hata akilipwa hafanyi kazi ile kwa ufanisi, ukweli ni kwamba hafurahii kufanya ile kazi, hafurahii kazi anafurahia zile hela anapata kutokana na ile kazi, anafurahia yale malipo anapata na anaamka kila siku kuja ofisini kwa kuwa tu mwisho wa siku anajua atalipwa anachopenda na kukifurahia, ina maana hapo siku hayo malipo yakichelewa au kukosekana itakuwa hatari, hatakuwa ni kitu cha kumpa moyo wa kuendelea kufanya kazi hiyo.
SOMA; Je Unachokifanya Kimeshikamana Na Moyo Na Mwili wako?
Watu wengi leo hii wanateseka sana kwa sababu ya pesa, wengi wanafanya vitu ambavyo vinaishia kuwapa hata msongo wa mawazo, maana wanafanya vitu wasivyovipenda, wasivyofurahia kufanya ni kile wanapata kutokana na kazi hizo kinawafanya waendelee kufanya, na wanahakikisha wanatumia nguvu na uwezo wao wote kufanikisha hilo. Lakini pamoja na hayo yote kipo kitu ambacho kila mtu anapenda kufanya, kile ambacho unaweza fanya hata bila kulipwa na mtu yeyote lakini unapata ile furaha ya ndani, ukifanya hicho unajiona umekamilika sasa. Ni kitu ambacho hata ukienda kwenye mihangaiko yako, hata uwe umechoka namna gani ni lazima ufanye kitu hicho hata kwa muda mfupi, ni kitu ambacho huhitaji mtu wa nje au chochote kukusukuma ili uweze kukufanya, yaani hicho kitu unakifanya kwa kuwa unasukumwa toka ndani kufanya hivyo, bila hicho unaona bado haujaishi au kutimiza wajibu wako hapa duniani, naweza sema hicho kitu ndio kinakufanya uwe wewe, kinakukamilisha , ndio kilichokufanya uje hapo duniani. Ni kwambie hicho ndicho kitu unatakiwa kufanya kwa bidii na ikibidi muda wako mwingi uutumie hapo maana hicho ndio unakifanya kwa moyo wako wote, akili zako zote na nguvu zako zote. Unaweza kuona kama hakieleweki leo lakini naomba utambue kuwa ukiendelea kufanya kile unapenda na kufurahia kinaweza kisikulipe leo, unaweza usione matunda leo lakini uwe na hakika ipo siku lazima utafurahia matunda ya hicho kitu au hata kwa kufanya hicho yupo mtu mwingine utamfanya naye aweze kupiga hatua fulani maishani mwake.
SOMA; Hivi Ndivyo Unavyodhulumu Maisha Yako Wewe Mwenyewe.
Faida ya kufanya kitu ambacho hauhitaji nguvu ya nje kuendelea kufanya ni kwamba kwanza utakuwa na furaha muda wote, maana unafurahia kuifanya hivyo hata kiafya ni nzuri huwezi kupata baadhi ya matatizo ya kiafya. Hautasumbuana na mtu kuja kuuliza kwa nini haujafanya hiki au kile, furaha yako ni kuona unafanya kila kitu kwa usahihi maana kuonekana kimefanyika sawa , wewe ni furaha yako. Na kwa namna hii ni lazima ufanikiwe tu.
Makala imeandikwa na Beatrice Mwaijengo
+255 755 350 772

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: