Majibu Ya Maswali Na Maoni Kuhusu Kujiunga Na KISIMA CHA MAARIFA, Kama Bado Hujajiunga Usiache Kusoma Hapa.

Habari za leo rafiki yangu?
Naamini uko vizuri na unaendelea kufanyia kazi yale ambayo unajifunza kupitia AMKA CONSULTANTS. Ninaamini kama tumekuwa pamoja kwa muda sasa umeshaanza kuona mabadiliko fulani kwenye maisha yako, na ndio maana bado tupo pamoja, vinginevyo ungeshaacha na kutumia muda wako huu adimu kwenye mambo mengine muhimu zaidi.
Ni kwa sababu hii nakuheshimu sana wewe kama msomaji wangu na kama rafiki yangu wa kweli. Kwa sababu uwepo wako, na kusoma kwako makala, na pale unaponipa mrejesho kwamba yale unayojifunza yanakusaidia kunanisukuma mimi kuendelea kuandika makala nzuri sana kwa ajili yako. niseme tena asante sana kwa uwepo wako rafiki yangu, nauthamini sana.
Leo nataka nitoe ufafanuzi kidogo kwa baadhi ya maswali na maoni ambayo ninyi marafiki zangu mmekuwa mnanitumia kila siku kuhusu KISIMA CHA MAARIFA. Mmekuwa mnatoa maoni mazuri sana ili kuhakikisha KISIMA kinakuwa bora sana. Asanteni pia kwa hilo, nathamini sana maoni yenu. Kabla hatujaingia kwenye ufafanuzi, kwanza tujue KISIMA CHA MAARIFA ni nini, maana huenda kuna rafiki yetu anasikia tu na hajawahi kujua vizuri.
KISIMA CHA MAARIFA ni blog ambayo inakupatia maarifa ya kina sana kuhusu kuishi maisha bora na yenye mafanikio. Na hili lipo kwenye kauli mbiu ya kisima ambayo ni CHOTA MAARIFA MBALIMBALI UBORESHE MAISHA YAKO. Kama ambavyo huwa tunaenda kwenye kisima kuchota maji, na kama ambavyo tunajua maji ni uhai, basi tunakuja kwenye KISIMA CHA MAARIFA kuchota maarifa, na maarifa ndio uhai wa maisha bora na ya mafanikio.
Ili uweze kuchota maarifa haya, unahitaji kuwa mwanachama kwa kujiunga na kulipa ada ya mwaka. Na kwa sasa ada ya KISIMA CHA MAARIFA ni tsh elfu 50 na unalipa kabla hujaanza kupata nafasi ya kusoma makala. Lakini pia kama hutalipia ada bado hutatoka mikono mitupu, kuna makala za KURASA ambazo ni makala fupi zenye kitu muhimu cha kujifunza ambazo zinawekwa kila siku. NDIO, KILA SIKU, bila ya kujali kuna nini kinaendelea.
Sasa karibu kupata ufafanuzi wa maswali ambayo yanaulizwa sana kuhusu KISIMA CHA MAARIFA.
1. Nikilipa hiyo elfu 50 napata nini?
Unapolipa ada ya kisima cha maarifa na kuwa GOLD MEMBER unapata yafuatayo;
Makala bora sana za biashara.
Makala bora sana za mbinu za kufikia mafanikio makubwa.
Makala bora sana za uchambuzi wa vitabu.
Makala za kujijengea tabia za mafanikio.
Na pia unapata nafasi ya kuwa kwenye kundi la wasap. Kupitia kundi hili unakutana na watu wenye mtazamo wa mafanikio kama wewe. Na kila siku asubuhi unaamshwa na tafakari nzuri itakayoifanya siku yako kuwa chanya. Utaweza kuianza siku vizuri na sio kwa kisirani.
2. Naweza kulipa ada hiyo kwa awamu?
Hapana, huwezi kulipa hivyo. Tulijaribu hili mwanzoni lakini lilileta usumbufu, watu walilipa kwa awamu na baadae kuacha kuendelea kulipa. Na walipotolewa walileta malalamiko makubwa sana. Hivyo jitahidi kufanya vyovyote ili kuipata ada kamili na kulipa na upate nafasi ya kujifunza zaidi.
3. Kwa nini ada isingekuwa inalipwa kwa mwezi badala ya mwaka?
Kulipa kila mwezi pia ni changamoto kubwa kwako msomaji na kwangu mimi mwendeshaji. Kulipa kwa mwaka kunatoa nafasi kwetu sote kukazana na kile ambacho ni muhimu, kujifunza.
4. Elfu hamsini ni kubwa sana, kwa nini usipunguze.
Ni kweli elfu hamsini ni fedha kubwa, lakini pia thamani unayoipata kwenye KISIMA ni kubwa kuliko ada hii. Na kama ukigawa elfu 50 kwa miezi inakuwa elfu nne kwa mwezi na ukigawa kwa siku ni kama shilingi 150 kwa siku. Kama unaweza kupata nafasi ya kujifunza kila siku, kwa siku 365 kwa mwaka kwa kuchangia shilingi 150/= tu, je ni ghali?
5. Nitaaminije kwamba napata thamani ya fedha zangu, nipe nafasi ya kuingia na nikiona ni pazuri nilipe ada.
Ninakuhakikishia utapata thamani kubwa sana ya kile ambacho umelipia. Na kama utaona hupati thamani hiyo, ndani ya mwezi mmoja tangu umejiunga, unaweza kuniambia sioni thamani na nikakurudishia fedha yako yote, bila ya swali la ziada. Hivyo unaweza kujiunga sasa na usipoteze chochote.
6. Nitajuaje kama sio utapeli.
Kama mpaka sasa unahofu kujiunga kwa kutuma ada yako ukifikiri ni utapeli wa mtandao basi ninachoweza kukushauri ni kwenda kwenye AMKA MTANZANIA, www.amkamtanzania.com kule kuna makala zaidi ya 1000, soma zote, au soma makala kama 100 hivi, halafu jiulize je mtu aliyeweka makala zote hizi anaweza kuwa tapeli? Ukishapata jibu chukua hatua.
Kwa kuhitimisha niseme haya machache.
Kama kweli unapenda kujifunza kila siku, na ungependa maisha yako yawe bora, basi jiunge na KISIMA CHA MAARIFA ni sehemu bora sana ya wewe kuwepo.
Na pia nikuhakikishie kwamba utapata thamani kubwa kulingana na ada unayolipa. Hiki ni kitu ambacho nimechagua kukifanya kwa miaka 50 ijayo, hivyo siwezi kufanya kitu chochote ambacho kitaniondolea fursa zangu za miaka yote 50 ijayo.
Najitahidi kujenga biashara yangu hii ya utoaji wa maarifa katika uaminifu mkubwa sana, kwa sababu hiki ni kitu kikubwa sana kwa baadae. Na ndio maana nipo tayari kuingia gharama yoyote kuhakikisha kila anayestahili kupata maarifa anayapata. Na kama kwa namna yoyote ile unaona huridhishwi unaweza kuniambia wakati wowote na tukatatua lile linalokusumbua.
Mara nyingi nimekuwa nikifanya mabadiliko kutokana na watu wanavyokwenda. Kwa mfano wengi waliokuwa wamejiunga kwa silver member walikuwa hawafungui makala, kwa mfumo ninaotumia najua mtu kafungua makala mara ngapi, kaingia mara ngapi na hata tarehe ya mwisho kuingia kwenye KISIMA ni lini. Wengi ambao hawakuwa GOLD MEMBERS walikuwa hawafungui makala. Na gold members karibu wote wanafungua makala, na hii inatokana na wao kuwa kwenye kundi la wasap ambapo nawakumbusha kila siku. Kwa njia hii naona hawa wanaolipa na hawasomi, siwatendei haki.
Na ndio maana yamekuja mabadiliko ya kuwa na uanachama wa aina moja tu, AMBAO NI GOLD MEMBER. Kwa wote kuwa kwenye kundi la wasap itakuwa rahisi kujifunza zaidi na kuchukua hatua.
JIUNGE NA KISIMA CHA MAARIFA.
Kama bado hujajiunga, jiunge leo hii ili usiendelee kuchelewa. Kujiunga tuma ada ya mwaka ambayo ni tsh elfu 50, (50,000/=) kwa namba zifuatazo, mpesa 0755 953 887 au tigo pesa 0717 396 253, jina litakuja AMANI MAKIRITA.
Ukishatuma ada tuma taarifa zako, jina kamili, email na namba ya simu kwa meseji au wasap kwenye namba 0717396253, na utapewa taratibu za kuwa mwanachama kamili. Karibu sana.
MUHIMU; Kwa wale wanachama wa zamani kumbuka kulipa ada yako ya kuendelea kuwepo kwenye kisima kabla ya mwisho wa wiki hii tarehe 04/12/2015.
Nafurahi sana kwa kuwa tunaendelea kuwa pamoja kwenye safari hii ya kuboresha maisha yetu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
AMKA CONSULTANTS.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: