Karibu Kwenye Semina; 2016 NI MWAKA WANGU WA UBORA WA HALI YA JUU.

Habari za wakati huu rafiki?
Naamini uko vizuri na unaendelea kufanyia kazi yale unayojifunza ili kuboresha maisha yako. hongera sana kwa hilo.
Rafiki sasa tumekaribia ule muda ambao watu wengi huwa wanafanya vitu ambavyo hawajui ni kwa nini wanafanya. Watu wamekuwa wakisukumwa kufanya vitu fulani kwa sababu kila mtu anafanya. Na hili limekuwa linaleta matatizo makubwa sana kwenye maisha ya wengi.
Wakati huo ambao tumeukaribia ni ule wakati wa kuweka malengo, ambao wengi huwa wanayaweka mwanzoni mwa mwaka. Kwa sababu kila mmoja anafanya hivyo.
Jambo kubwa la kushangaza ni kwamba pamoja na kila mtu kuweka malengo, tena mazuri sana ya mwaka, miezi miwili baadaye asilimia 95 ya watu wanakuwa wameshaachana na malengo yao, na kurudi kwenye maisha yao ya kawaida. 

 
Na jambo jingine la kushangaza ni kwamba mtu mmoja anaweza kuweka malengo yale yale kila mwaka kwa miaka kumi na anashindwa kuyatimiza. Kila mwaka mpya anaamka na kusema MWAKA MPYA MAMBO MAPYA, anapanga mambo atakayofanya lakini baada ya muda anaachana nayo, anasema nitajaribu tena mwakani. Na anafanya hivi kwa miaka mingi, bila ya mafanikio.
Je unawajua watu wa aina hii? Je na wewe umewahi kujikuta kwenye mkumbo huu? Basi usijilaumu kwa sababu unakwenda kupata suluhisho la kudumu la matatizo haya, endelea kusoma hapa.
Wanamafanikio wengi, yaani wale ambao ni wasomaji wa AMKA MTANZANIA na wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, tayari wameshauanza mwaka 2016 na tayari wameshaanza kupanga na kufanyia kazi malengo yao. Kwa hatua hii tu wanajiweka pembeni na ule mhemko wa kuweka malengo kwa sababu kila mtu anafanya hivi. Na kwa wakati huu inakuwa rahisi sana kufanyia kazi malengo yako, kwa sababu hakuna kelele nyingi.
Kama wewe hukupata nafasi hii ya kuweka malengo yako na kuuanza mwaka 2016 mapema, usihofu, kwani pia utakwenda kupata nafasi ya kuweka malengo bora sana kwako ambayo utaweza kuyafikia.
Karibu kwenye semina muhimu kwa mwaka 2016.
AMKA CONSULTANTS tumekuandalia semina muhimu sana kwako kwa mwaka huu 2016. Semina hii ni muhimu sana kwa sababu inakuandaa kuweza kuufanya mwaka 2016 kuwa mwaka wa kipekee kwako, kuwa mwaka wako wa kuweka ubora wa hali ya juu na kufikia mafanikio makubwa zaidi ya uliyonayo sasa.
Hii ni semina ambayo huwezi kumudu kuikosa kwa sababu kufanya hivyo ni kuamua kwamba hutaki kuboresha maisha yako zaidi. Ni sawa na kuamua kwamba utaendelea kuwa kawaida kwa pale ulipo sasa.
Kupitia semina hii utapata nafasi ya kujifunza mambo haya muhimu sana kwenye maisha yako;
1. Kauli mbiu ya 2016 na Jinsi ya kufanya 2016 kuwa mwaka wa kipekee kwako.
2. Umuhimu wa kuweka malengo makubwa kwenye maisha yako.
3. Hatua saba za kuweka malengo ambayo utayafikia na aina kuu tano za malengo unayotakiwa kuweka.
4. Jinsi ya kuweka malengo binafsi.
5. Jinsi ya kuweka malengo makubwa ya kifedha.
6. Jinsi ya kuweka malengo makubwa ya kazi na biashara.
7. Jinsi ya kuweka malengo ya familia na mahusiano.
8. Jinsi ya kuweka malengo ya kiafya.
9. Jinsi ya kuepuka changamoto zinazoweza kukurudisha nyuma kwenye malengo.
10. Maisha mapya kwa mwaka 2016 na kuendelea.
Mambo hayo kumi, utajifunza kwa undani, na utafanya kwa vitendo ili mwisho wa semina uwe na mpango bora sana wa maisha yako ambao utaufanyia kazi kwa mwaka 2016.
Kila mwaka tumekuwa na kauli mbiu yetu kama wanamafanikio, mwaka 2015 tumekuwa na kauli JUST DO IT, yaani ANZA KUFANYA. Kauli mbiu hii ilikuwa ikitupa nguvu ya kuweza kuanza kufanya kitu hata kama bado hatujawa na maandalizi ya kutosha. Kama uliifanyia kazi nina hakika unajua ni jinsi gani imekuwezesha kufanya makubwa.
Sasa mwaka 2016 tunakuja na kauli mbiu nyingine nzuri na muhimu sana kwako. Kwa kutumia kauli mbiu hii itakusukuma kufanya hata pale unapokuwa unakaribia kukata tamaa. Utapata nafasi ya kuijua kauli mbiu hii na jinsi ya kuitumia kupitia semina hii.
Kupitia semina hii utajifunza mchakato mzima wa kuweka malengo, hatua kwa hatua, na utafanya hivyo wewe mwenyewe kwenye malengo yako. Mpaka mwisho wa semina utakuwa na malengo ambayo yanajitosheleza na kazi inabaki kwako kuyafanyia kazi.
Hutakuwa tena na yale malengo yasiyoeleweka, ambayo ni magumu kutekeleza na yanakushawishi kukata tamaa. Utakuwa unajua kabisa ni kipi cha kufanya na kwa wakati gani. Pia utajua ni changamoto zipi unakwenda kukutana nazo na jinsi ya kuzivuka ili zisiwe sumu kwako kufikia malengo yako makubwa.
Semina hii inatolewa kwa njia ya mtandao na mafunzo yatatumwa kwa njia ya email. Pia kama mshiriki utapata nafasi ya kuwepo kwenye kundi la wasap na hivyo kupata nafasi ya kujifunza zaidi.
Semina hii itaanza tarehe 04/01/2016 na itaendeshwa kwa wiki mbili.
Ili kuhakikisha unapata nafasi ya kushiriki semina hii jiunge kwa kubonyeza maandishi haya nakuweka taarifa zako.
Kujiunga na semina hii ni kuanzia leo na mwisho wa kujiunga ni tarehe 02/01/2016.
Gharama ya kushiriki semina hii ni tsh elfu 20 (20,000/=). Kwa wale ambao ni wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA GOLD waliolipia ada zao watashiriki semina hii bila kulipa ada hiyo. Hii ni kwa semina hii ya mwanzo wa mwaka, na itakuwa hivi kwa kila semina ya mwanzo wa mwaka.
Hakikisha hukosi nafasi hii ya kipekee ya kuufanya mwaka 2016 kuwa mwaka wa kipekee kwako.
Angalizo;
Naomba kutoa angalizo hili muhimu sana;
Kama hupo tayari kufanya kazi, kama hupo tayari kujituma, usijiunge na semina hii. Semina hii itakuhitaji utenge angalau nusu saa kila siku kwa siku hizo kumi ili kufanyia kazi yale ambayo utakuwa umeelekezwa. Na utahitajika kufanya hivyo, sio kuchagua kama utafanya au la.
Kama ambavyo wote tunaona mabadiliko yanayoendelea kwenye nchi yetu, basi kila mmoja wetu ayaweke mabadiliko haya kwenye maisha yake. Hivyo unahitaji kuvuka visingizio vyote na kufanya, kile ambacho unahitajika kufanya, kila siku. Kila siku utahitajika kutoa ripoti ya kile ulichofanyia kazi.
Kwa njia hii utafaidika sana na semina hii na utakapoimaliza, utakuwa mtu tofauti kabisa na kuwa tayari kwenda kufanyia kazi yale ambayo umejifunza.
Karibu sana kwenye semina hii itakayoendelea kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Kuhakikisha unapata nafasi ya kushiriki semina hii fungua hapa na uweke taarifa zako, na hakikisha unafanya malipo kabla ya tarehe 02/01/2016.
Ili kuweza kumfuatilia kila mshiriki vizuri, nafasi za kushiriki semina hii zitakuwa chache sana, hivyo chukua hatua haraka ya kujiunga ili kujihakikishia unapata mafunzo haya mazuri sana.
Nakukaribisha sana kwenye semina hii kubwa na nakutakia kila la kheri katika mwaka huu 2016.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: