Kwa Nini Huwa Siandiki Makala Za Watu Wenye Mafanikio Makubwa Duniani, Na Ninachofanya Badala Yake.

Habari za wakati huu rafiki?
Ni imani yangu kwamba unaendelea vyema na harakati zako za kuwa na maisha bora zaidi kadiri siku zinavyokwenda. Hilo ndio jambo la msingi sana kwa sababu maisha ni kwenda mbele au kurudi nyuma. Hakuna katikati, ni iwe unayafanya maisha yako kuwa bora, au unayafanya kuwa hovyo. Na yote hayo yanatokana na juhudi zako wewe binafsi, sio jukumu la mtu mwingine yeyote, sio serikali, wazazi, ndugu au yeyote unayeweza kudhani anahusika. Ni wewe.
Marafiki na wasomaji wengi wamekuwa wakitoa maoni mazuri sana na ushauri juu ya makala ninazoandika. Na wengi sana wamekuwa wakipendekeza niwe naandika makala za watu waliofikia mafanikio makubwa duniani. Kwa kuwa kupitia makala hizi watu wanahamasika zaidi na kuona kwamba inawezekana. Ni kweli kabisa ya kwamba kupitia hadithi za wengine, kupitia watu ambao walianzia chini sana na kuweka juhudi hatimaye kufika juu kabisa, unaweza kuhamasika sana na wewe kuchukua hatua kubwa.
Ila tatizo linakuja moja….
Hadithi nyingi za watu waliofanikiwa ni wa nchi za nje, nchi za amerika na ulaya. Kwa hapa kwetu Tanzania kuna watu wengi ambao wana mafanikio makubwa ila taarifa zao hazipatikani kirahisi. Ni vigumu sana kupata taarifa za watanzania wenzetu ambao wameweza kujikomboa kutoka kwenye hali ngumu na kufikia mafanikio makubwa.
Kuandika makala za watu wenye mafanikio makubwa, ambao hawapo kwenye amzingira yetu inaleta hamasa, lakini inaweza kuwa na kikwazo kimoja, mtu anaweza kufikiri lakini hii ni ulaya, lakini hii ni marekani, imewezekana kwao ambao wana mazingira bora, na sababu nyingine nyingi.
Mimi binafsi najifunza sana kupitia watu ambao wamefanya mambo makubwa duniani, watu kama kina Bill Gates, Steve Jobs, Jack Ma, na wengine wengi. Na najua kabisa ya kwamba mbinu walizotumia wao kufikia makubwa waliyofikia zinaweza kutumika popote duniani na zikaleta majibu kama waliyopata wao. Najua kabisa tofauti ya kimazingira haifanyi mbinu hizi zisifanye kazi, badala yake ni kuzifanya ziendane na mazingira ambayo mtu upo.
Lakini mimi naandika makala ambazo wewe msomaji unaweza kuondoka na kitu ambacho ukienda kukifanyia kazi kitabadili maisha yako. na ninavyoandika huwa natumia msingi mmoja muhimu, kuhakikisha mwanafunzi wa darasa la tano anaelewa makala hiyo vizuri kama akiisoma. Na ndio maana umekuwa unaona makala hizi zinatumia lugha rahisi sana na mifano ambayo inaeleweka.
Inakuwa vigumu sana kuandika makala nzima kwa mtu aliyefanikiwa nchini marekani. Msomaji anaweza kusoma na akifika mwisho akajishawishi kwamba hii ni kwa marekani, hapa kwetu haiwezekani, kitu ambacho sio kweli. Sipendi nitumie rasilimali zangu kubwa kuandika makala halafu mwisho msomaji ajishawishi kwamba kwake haiwezekani, napenda kutoa kila ninachojua na ninachofanya na ibaki kwa mtu mwenyewe kuchukua hatua, huku akijua ni kitu ambacho kinawezekana kama akiweka juhudi.
Nafanya nini sasa, kama hadithi za wengine haziwezekani?
Kutokana na kwamba hadithi nyingi za mafanikio zinazopatikana ni za watu wa nje ya nchi, nilipata wazo la kuanzisha KISIMA CHA MAARIFA, kupitia KISIMA, tunatengeneza hadithi mpya za mafanikio baina yetu wenyewe.
Kwenye KISIMA CHA MAARIFA, tunatengeneza wana mafanikio wa hapa kwetu wenyewe ambao wapo tayari kushirikisha wengine safari yao ya mafanikio. Kupitia kisima, watu wanajifunza na kufanyia kazi yale wanayojifunza, pamoja na kushirikishana safari yao ya mafanikio. Haya yanafanyika kupitia blog ya KISIMA CHA MAARIFA, ambapo unahitaji kujiunga ili uweze kuzisoma makala nzuri na pia kupitia kundi la wasap ambapo kunakuwa na mijadala mbalimbali ya kushirikishana mambo muhimu kuhusu mafanikio.
Je unataka kuwa sehemu ya kizazi kipya cha mafanikio?
Kama na wewe unataka kuwa sehemu ya kizazi kipya cha mafanikio, kuwa sehemu ya watu tunaotengeneza historia mpya ya mafanikio kwenye nchi yetu, basi chukua hatua sasa kabla hujachelewa. Jiunge leo na KISIMA CHA MAARIFA na uwe sehemu ya wanamafanikio. Kupitia kisima hutapata muda wa kulalamika kwamba haiwezekani au kwa nini wewe tu, bali utajifunza na kupitia ushindi na changamoto za wengine, utapata njia bora ya wewe kufikia mafanikio makubwa. Na wewe ukishapata mafanikio hayo unawashirikisha wengine pia. Ni nafasi bora kiasi gani hii ambayo bado hujaichangamkia?
Unajiungaje na KISIMA CHA MAARIFA?
Unajiunga kwa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh elfu 50 (50,000/=) na unatuma ada hiyo kwenye namba 0755 953 887 au 0717 396 253 katika kutuma jina litakuja AMANI MAKIRITA. Ukishatuma ada hiyo, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenye namba 0717396253 na hapo utapewa maelekezo mengine pamoja na kuingia kwenye kundi la wasap. Pia unaweza kutembelea KISIMA CHA MAARIFA kwenye www.kisimachamaarifa.co.tz ili ujiridhishe na makala zilizopo pale.
SOMA; Malengo Matano (5) Muhimu Kwako Kuweka Mwaka 2016 Ili Uwe Na Maisha Bora Sana.
Karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, karibu tujenge historia mpya ya mafanikio kwenye taifa letu kwa manufaa yetu na ya wanaotuzunguka.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
AMKA CONSULTANTS.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s