Habari za leo rafiki?
Karibu tena kwenye makala zetu hizi za kujifunza na kuhamasika ili kuweza kuboresha maisha yetu zaidi. Kupitia makala hizi tumekuwa tunapeana mbinu muhimu sana za kuweza kuwa na maisha bora, kuanzia kwenye kipato, utendaji wetu, mahusiano yetu na wengine na hata mipango yetu ya baadae.
Lakini kujifunza pekee hakuwezi kuleta mabadiliko makubwa kwenye maisha yako. hata ungejifunza kiasi gani, kama wewe mwenyewe hutachukua hatua, basi hakuna kitu kitakachobadilika kwenye maisha yako. hivyo kuchukua hatua ni muhimu sana.
Lakini pia kuchukua hatua sio kitu rahisi kama ilivyo kwenye kusema kwamba nitachukua hatua, kuna changamoto zake nyingi na huenda ulishachukua hatua huko nyuma na ukaishia kuumia. Kuchukua hatua peke yako ni vigumu na inahitaji moyo sana.
Mwaka 2014 nilianzisha KISIMA CHA MAARIFA kama blog ya kulipia ambapo kwa wale wasomaji wa AMKA MTANZANIA ambao wanataka kupata maarifa ya ziada basi waliweza kujiunga kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Wasomaji wengi sana wamekuwa wakijiunga kwenye KISIMA, asanteni sana.
Mwanzoni mwa mwaka 2015 tulikuwa na mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA kupitia mtandao wa wasap, na kwa pamoja tukaazimia kuanzisha kitu ambacho kitakuwa ni kufanyia kazi haya ambayo tunajifunza kila siku.
Hivyo baada ya hapo tulianzisha kampuni ambayo imeshasajiliwa hapa Tanzania na inajulikana kwa jina KISIMA CHA MAARIFA TANZANIA (KICHAMATA) INVESTMENT COMPANY LIMITED au kwa kifupi KICOL. Hii ni kampuni ya uwekezaji ambapo mtaji unatoka kwetu sisi wanachama.

CHETI CHA HISA ZA KICHAMATA

 
Kupitia kampuni hii kila mwanachama aliahidi kiasi cha mtaji anachoweza kuchangia kila mwezi na tulikubaliana kila mmoja wetu kuchangia kwa miaka miwili. Lengo ni kuwa na mtaji usiopungua milioni 100 ndani ya miaka hii miwili.
Hii ni kampuni ya uwekezaji ambapo tuna mipango mikubwa sana ya uwekezaji kwa hapa Tanzania na hata nje baadae. Kwa sasa tumeshaanza na uwekezaji kwa kununua hisa, na tunaendelea na uwekezaji ambapo tumepanga kuwekeza kwenye kilimo pamoja na kuwekeza kwenye biashara ambazo zinaweza kunufaika na sisi kunufaika pia.
Hii ni kampuni ya kipekee sana kwa hapa Tanzania, na kwa bahati nzuri sana hata wewe unaweza kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hii.
Pata nafasi ya kuwa mwekezaji.
Sasa kama umekuwa mfuatiliaji wa mafunzo haya kwa kipindi kirefu, ni lazima uwe umeshaanza kuchukua hatua. Na kama bado hujaanza kuchukua hatua, au hata kama umeshaanza kuchukua hatua, basi kampuni hii ya uwekezaji ni sehemu nzuri sana kwako kuchukua hatua.
Kwa mfano kama ulielewa vizuri kuhusu kujilipa wewe kwanza, kwa kuweka pembeni asilimia 10 ya kipato chako, baada ya muda unahitaji kuwekeza asilimia hiyo kumi. Sasa kama kipato chako ni laki tano kwa mwezi, asilimia 10 ni elfu 50. Na ukiweka pembeni elfu 50 kwa miaka miwili ni milioni moja na laki mbili. Kwa mtu mmoja huwezi kuwekeza milioni moja, lakini kama mpo watu hamsini, hiyo ni milioni hamsini. Mkiwekeza milioni 50 kwenye maeneo yenye kurejesha vizuri na ambayo sio hatari sana, mnapata faida kubwa kwa pamoja.
Unaweza kupata nafasi hiyo ya kuwa mwekezaji kwa kujiunga na kampuni hii ya KICHAMATA.
Vigezo vya kujiunga na KICHAMATA.
Ili uweze kujiunga na kampuni hii ya KICHAMATA, kwanza kabisa ni LAZIMA uwe mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Hii ni muhimu kwa sababu tunataka tunavyoendesha kampuni hii twende na falsafa moja. Tunataka kwa pamoja tuwe tunajua ni maeneo gani tunawekeza, hatari na faida zikoje na jinsi gani ya kupunguza hatari na kuongeza faida. Tunataka kwa pamoja tujue hakuna kitu ambacho hakina hatari na pia changamoto. Na pia kwa pamoja tunataka tujue sehemu yoyote inayoshawishi faida kubwa sana kwa uwekezaji kidogo ni hatari. Na hivyo kwenda taratibu ili kuhakikisha tunafanya mamauzi ambayo ni bora kwetu.
Unaweza kutengeneza falsafa hii taratibu kutokana na makala na mijadala inayokuwa inaendelea kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo ni lazima uwe kwenye KISIMA CHA MAARIFA ili kufaidi hili.
Kama ungependa kuwa sehemu ya kampuni hii na bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, basi jiunge leo. leo hii chukua hatua ya kujiunga ili upate nafasi hii nzuri ya kuwa sehemu ya uwekezaji mkubwa sana kwenye nchi yetu.
Ili kujiunga tuma ada ya mwaka ambayo ni tsh elfu 50 kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 na kisha tuma ujumbe wa wasap kwenye 0717396253 kisha utapatiwa maelekezo zaidi.
Muda ni mfupi nafasi ni chache.
Muda wa kujiunga ni mfupi, tutachukua wanahisa wapya kwa mwezi huu wa kwanza, hivyo kama ungependa kuwa mmoja wao hakikisha unajiunga na KISIMA CHA MAARIFA mapema sana, yaani leo hii.
Pia nafasi za kuingia kwenye kampuni hii ni chache. Kulingana na sheria za nchi yetu, idadi ya wamiliki wa kampuni binafsi ni watu wawili mpaka 50. Hivyo tukishafika 50 nafasi zinakuwa zimejaa. Hivyo unahitaji kuwa tayari kuchukua hatua kama kweli unaitaka nafasi hii nzuri sana.
Kama utakuwa na swali lolote la ziada tuwasiliane kwa namba 0717396253.
Nakukaribisha sana katika kufanyia kazi kwa pamoja haya tunayojifunza.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.
makirita@kisimachamaarifa.co.tz