MUHIMU; Likizo Ya Wiki Moja.

Habari zako rafiki yangu?
Naamini kwamba unaendelea vizuri sana.
Na pia naamini mwaka 2015 umekuwa mwaka bora sana kwako, na 2016 ndio unataka uwe bora zaidi. Na hata kama kuna mambo uliyopanga kukamilisha kwa mwaka 2015 ila hukuweza kukamilisha, usijiumize sana moyo, nina hakika kuna mengi umejifunza na kama utayatumia mwaka 2016 basi maisha yako yatakuwa bora sana.
Je mwaka 2015 AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA vimekuwa na mchango kwenye ukuaji na mafanikio yako? kama jibu ni ndio basi tushirikishe kwa kutuma email yenye maelezo kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Leo nataka nikupe taarifa muhimu sana wewe kama msomaji wangu na rafiki yangu. Kila mwaka nimekuwa na utaratibu wa kujipa wiki moja ya likizo. Hii ni wiki moja ambayo najipa likizo ya kufanya shughuli zangu mbalimbali. Kwa wiki hii moja napata muda mzuri wa kutafakari kile ninachofanya, nimekifanyaje na ni vitu gani bora zaidi ninavyoweza kufanya.
Kwa mwaka huu wiki hii ya likizo itaanza jumamosi ya tarehe 19/12/2015 na itakwisha jumamosi ya tarehe 26/12/2015.
Katika wiki hii sitapatikana kabisa kwenye mtandao wa intaneti, na nitapata muda mzuri wa kuondokana na kelele za kila siku na kupata muda wa kwenda ndani zaidi, ndani yangu na ndani ya kila ninachofanya ili niweze kuona ni yapi mazuri zaidi kufanya na kuboresha.
Kitu pekee kitakachoendelea kupatikana.
Ninaposema ninakuwa likizo ya wiki moja, simaanishi kwamba nitakuwa nimelala kwa wiki nzima, bali nitapata muda wa kuchukulia kile ninachofanya kama mtu wa nje, kwa sababu kwa kipindi hiki nitakuwa sifanyi.
Lakini kuna kitu kimoja kitaendelea kupatikana kwenye wakati huu wa likizo, na kitu hiko ni MAKALA ZA KURASA kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi zitaendelea kupatikana kila siku.
Makala hizi za kurasa ni changamoto ambayo nimejipa ya kuandika kila siku kwa siku zote za maisha yangu zilizobakia. Na tangu nimeanza ukurasa wa kwanza, mpaka leo ambapo nimefika ukurasa wa 352, hakuna siku hata moja ambayo nimeacha kuandika, hata sababu iwe kubwa kiasi gani, nimekuwa nahakikisha lazima naandika. Nategemea kuendelea kufanya hivi kila siku, kwa maisha yangu yote. Hivyo makala hizo zitaendelea kupatikana kila siku.
Ufanye nini kwenye wiki hii moja?
Kwenye wiki hii moja akushauri ufanye mambo yafuatayo.
Soma sana kuhusu makala za malengo kwenye AMKA MTANZANIA, kwa kipindi hiki ni rahisi sana kuvutwa vibaya na kujikuta unaweka malengo ambayo sio muhimu kwako. Kusoma makala hizo bonyeza maandishi haya.
Soma makala mbalimbali kwenye KISIMA CHA MAARIFA, kuna makala nzuri sana za uchambuzi wa vitabu, kujijengea tabia za mafanikio na makala za biashara na ujasiriamali.
Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, pia nakushauri sana ufanye hivyo sasa, kwa sababu kuna mengi mazuri sana yaliyopo na yanayokuja kwenye KISIMA.
Na kama bado hujajiunga na SEMINA YA MWAKA 2016 basi fanya hivyo sasa, kwa kubonyeza hapa na kujaza taarifa zako.
Heri ya sikukuu ya Krismasi.
Kwa sababu Krismasi hatutakuwa pamoja hapa, nitumie nafasi hii kukutakia heri ya sikukuu ya krismasi. Iwe bora sana kwako na usherekee kwa amani.
Nakutakia kila la kheri katika kuyaboresha maisha yako zaidi. Tuendelee kuwa pamoja kwa sababu bado kuna mengi mazuri sana yanakuja.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s