Mambo Mazuri Kutoka AMKA MTANZANIA Mwaka Huu 2016.

Habari za leo rafiki?
Naamini unaendelea vyema sana na maisha yako yanazidi kuwa bora kadiri siku zinavyokwenda. Na hii yote ni matokeo ya wewe kuamua kuchukua hatua kutokana na mambo mbalimbali unayojifunza. Hongera sana rafiki yangu kama hiki ndio kinachoendelea kwenye maisha yako.
Leo napenda kuchukua nafasi hii kukushirikisha wewe rafiki yangu mambo mazuri sana utakayoyapata kupitia AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA kwa mwaka huu 2016. Marafiki na wasomaji wengi mmekuwa mkiuliza mbona hatujapeana mikakati ya mwaka huu 2016. Sasa umefika wakati w akupeana mikakati hii muhimu ili kuhakikisha kila mmoja wetu anakuwa na maisha bora sana.
Kabla hatujaingia kwenye mikakati hii bora kwa mwaka 2016 kwanza tuangalie mwaka 2015 umekwendaje kwetu sisi wote kupitia AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA. Kwangu binafsi nimeweza kuona ukuaji mkubwa kifikra na hata kiroho kupitia makala mbalimbali ambazo nimekuwa ninaandika. Pia kupitia KISIMA CHA MAARIFA nimeweza kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwenu ninyi marafiki, tumeweza kuanzisha kampuni ya uwekezaji kupitia mtandao wa KISIMA CHA MAARIFA. Kupitia AMKA MTANZANIA mwaka 2015 tuliweza kuendesha semina tatu kwa njia ya mtandao na pia kutoa program ya ukocha kwa watu wengi waliokuwa wanahitaji kuongozwa kwenye mambo waliyokuwa wakifanya. Pia kwa mwaka 2015 nimeweza kusoma vitabu vingi zaidi, angalau vitabu viwili kila wiki na vitabu zaidi ya 100 kwa mwaka mzima kupitia kikundi chetu cha usomaji vitabu kinachoitwa TANZANIA VORACIOUS READERS . Hayo ni machache kati ya mengi ambayo nimeweza kufanya mwaka 2015 kuboresha zaidi maisha yangu na kazi yangu hii ninayofanya.
Tushirikishe mwaka wako 2015.
Tafadhali tushirikishe mwaka wako 2015, ni kwa jinsi gani AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA vimeweza kukusaidia kuboresha maisha yako zaidi? Ni kwa jinsi gani maisha yako yameimarika kwenye mwaka 2015? Tushirikishe kwa kujibu email hii, kama umepokea kwa email au kwa kutuma email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz chukua dakika chache kuniambia mwaka 2015 umekwendaje kwako na AMKA MTANZANIA pamoja na KISIMA CHA MAARIFA vimekuwa na msaada gani kwako kwa mwaka huo 2015.

http://www.amkamtanzania.com/p/kuwa-tajiri.html

 
Mikakati ya mwaka 2016.
Kama ambavyo nimekuwa nikisisitiza kwenye makala ninazoandika, maisha ni kwenda mbele au kurudi nyuma, hakuna kusimama, hakuna kati kati. Ni unaenda mbele au unarudi nyuma, hata kama unasema unasimama, unajidanganya, maana yake unarudi nyuma, kwa sababu dunia inakwenda kwa kasi kubwa sana.
Kasi hii imewaacha wengi ambao hawajaweza kwenda nayo. Kwa mwaka huu 2016 tumejipanga kwenda na kasi hii ya mabadiliko ya dunia na hivyo tutaboresha zaidi huduma ambazo tunatoa kupitia AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA.
AMKA MTANZANIA.
Kwenye AMKA MTANZANIA, utaendelea kupata makala nzuri na bora sana kuhusu USHAURI WA CHANGAMOTO, MBINU ZA MAISHA NA MAFANIKIO, UCHAMBUZI WA VITABU na pia tutaanza kwenda ndani zaidi kuhusu mbinu za MAFANIKIO KWENYE KAZI na hata KUJIJENGEA NIDHAMU YA MUDA NA FEDHA. Haya ni maeneo muhimu sana kwa kila mmoja wetu ili aweze kuwa na maisha bora.
Pia makala zitazidi kuwa na maarifa mazuri sana yanayokuwezesha wewe kuchukua hatua ya kuboresha maisha yako.
KISIMA CHA MAARIFA.
Kwenye KISIMA CHA MAARIFA utaendelea kupata makala bora sana za BIASHARA NA UJASIRIAMALI, MBINU ZA MAFANIKIO, UCHAMBUZI WA VITABU NA FALSAFA MPYA YA MAISHA. Bila ya kusahau makala za KURASA ZA MAISHA ambazo ni makala zinazokujia kila siku.
Kama unavyojua KISIMA CHA MAARIFA unahitaji ujiunge ndio uweze kusoma makala hizo, ukiondoa makala za KURASA ZA MAISHA . Pia kwa kujiunga unapata nafasi ya kuwa kwenye kundi la wasap ambapo humo unajifunza mambo mengi zaidi yanayokufanya uwe chanya na uweze kuchukua hatua kila siku ya kuboresha maisha yako. kila siku unaianza siku yako chanya, unapata tafakari ya siku, inayokufanya uwe chanya zaidi na pia unapata nafasi ya kushauriwa kwa changamoto mbalimbali unazopitia.
Kama bado hujajiunga na KISIMA, jiunge leo kwa sababu nafasi za kuingia kwenye kundi la wasap zimebaki nne tu.
Kujiunga tuma ada ya mwaka ambayo ni tsh elfu 50 kwenye namba 0755953887 au 0717396253 kisha tuma ujumbe wenye majina yako na email kwa wasap kwenda kwenye namba 0717396253. Karibu sana ujiunge na wanamafanikio wenzako na ujihakikishie kufikia mafanikio makubwa.
Mambo mengine mazuri kwa mwaka huu 2016.
1. Mafunzo kwa njia ya video.
Mwaka huu 2016 nitaanza kutoa mafunzo haya kwa njia ya video pia na tutaanza na video fupi fupi kwenye mtandao wa YOUTUBE, tutaendelea kupeana taarifa kadiri video mpya inavyotoka.
2. Kuchapa vitabu.
Mwaka huu 2016 nitachapa vitabu viwili na hivyo mafunzo haya yataanza kupatikana kwenye vitabu vya kawaida. Nimekuwa natoa vitabu ambavyo ni softcopy tu, najua kuna wengi hawawezi kusoma vitabu kwa njia hii ya softcopy, hivyo vitabu vya kawaida vinakuja.
3. Semina kwa njia ya mtandao.
Kwa mwaka huu 2016 nitaendesha semina nne kwa njia ya mtandao, ya kwanza tayari imemalizika, sasa zimebaki semina tatu ambazo zitaendeshwa kwa njia ya mtandao. Kila moja itakuwa baada ya miezi mitatu. Na semina zote zinalenga kuboresha maisha yetu zaidi.
4. Workshop (warsha).
Kwa mwaka huu 2016 nitaandaa workshop mbili ambapo tutakutana pamoja kwa wale ambao tunataka kuboresha maisha yetu, kazi zetu na hata biashara zetu, kila workshop itakuwa ya siku moja na tutajadili mengi na kuwekeana mikakati ya kwenda kufanyia kazi ili kuona mabadiliko ya kweli kwenye maisha yetu. Endelea kutembelea mitandao hii na utapata taarifa zaidi kuhusu workshop hizi.
5. Huduma za ukocha.
Pia kwa mwaka huu 2016 nitaendelea kutoa huduma za ukocha kwa wale ambao wanataka kupata mwongozo kwenye jambo lolote wanalotaka kuwa bora sana kwenye mwaka 2016. Inaweza kuwa ni biashara, kazi, kubadili tabia, kujijenga kujiamini, kuandika, kuondokana na madeni, kujenga nidhamu ya fedha na muda, kuongea mbele za watu na mengine mengi ambayo unahitaji kufanya ili maisha yako yawe bora. Karibu sana tufanye kazi pamoja kama kuna kitu kikubwa unataka kufanya kwa mwaka 2016.
Hiyo ndiyo mikakati ya mwaka 2016 kupitia AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA. Nachukua nafasi hii kukukaribisha sana tuendelee kuwa pamoja ili kuhakikisha maisha yetu yanakuwa bora zaidi kila siku.
Tafadhali usisahau kunijulisha ni kwa jinsi gani AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA vimekusaidia kwa mwaka 2015 kuweza kufanya mambo makubwa. Pia nijulishe ni mambo gani makubwa uliweza kufanya. Jibu email hii kama umepokea kwa email au tuma mrejesho wako kwenye email makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Nakutakia kila la kheri kwa mwaka 2016 ukafanye makubwa zaidi.
TUPO PAMOJA.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.
0717396253.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: