Siri Kubwa Ya Kukutoa Kwenye Umaskini.

Kipo kitu kimoja tu chenye nguvu na uwezo mkubwa wa kukutoa kwenye umaskini endapo utakizingatia na kukitumia kwenye maisha yako kila siku kwa kumaanisha. Haijalishi upo kwenye umaskini au maisha mabaya kiasi gani hata yasiyoelezeka, ukikitumia kitu hiki ni lazima UFANIKIWE.
Kitu hiki si bahati wala muujiza kama unavyoweza kufikiria. Kitu pekee ambacho kinaweza kukutoa kwenye maisha yoyote mabaya au hali yoyote ngumu ambayo unaiona hata wakati mwingine haiwezi kuelezeka ni KUFANYA KAZI KWA BIDII. Hiki ndicho kitu chenye nguvu kubwa ya kukutoa kwenye umaskini.
Ukiweka juhudi na nguvu zako nyingi kwa kile unachokifanya ni lazima ufanikiwe hata iweje. Watu wengi weye mafanikio makubwa ni wafanyaji wakubwa wa kazi kwa bidii. Tatizo kubwa walilonalo watu wengi ni kutaka kujipatia pesa na mafanikio makubwa bila ya kufanya kazi kwa bidii kubwa. Kama hizo ndizo fikra zako ni lazima rafiki utakwama.
Siri na nguvu kubwa ya mafanikio unaipata kwa kufanya kazi kwa bidii zote na bila kuleta mchezo wowote. Ukitegemea upate pesa nyingi bila kujituma elewa hutafanikiwa sana na huo ndio ukweli halisi. Jaribu kuangalia maisha ya watu wengi ambao wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa, walichokifanya kikubwa ni kujitoa na kufanya kwa juhudi zote.

JITOE KUFANYA KAZI KWA JUHUDI ZOTE


Unaweza ukaliona hili vizuri kwa mgunduzi wa balbu Thomas Edson. Akiwa katika hali mbaya ya umaskini, akiishi kijijini kusiko na umeme Thomas Edson alijitoa na  kufanya kazi kwa masaa 18 kila siku bila kuchoka mpaka alipofanikisha ugunduzi wake wa balbu na hatimaye kuwa tajiri.

Lakini si huyo tu King Camp Gillette akiwa kijana mdogo wa miaka 17 alijikuta akiishi maisha magumu yasiyo na mbele wala nyuma mara baada ya kampuni ya baba yake kuungua moto. Hilo halikumtisha sana Gillete aliamua kujitoa kwa nguvu zake zote na kutafuta njia yake mwenyewe na hapo akafanikisha ugunduzi wa wembe aina ya Gillette.
Abraham Lincoln na Andrew Jackson kwa nyakati tofauti bila shaka unafahamu walikuwa Marais wa marekani. Lakini kufika huko haikuwa kazi nyepesi walijituma na kujitoa kweli mpaka kufanikisha azma yao hiyo. Kila walipokosea waliamka na kunyanyuka tena. Hakuna kilichokuwepo kichwani mwao zaidi ya kufanya kazi kwa bidii kupindukia huyo ndiyo alikuwa mkombozi wao.
Hiyo haitoshi Hellen Adams Keller akiwa katika hali ya upofu ambayo kila mtu aliamini hawezi kufanya kitu, lakini mwanamke huyu aliweza kuwa mtunzi wa vitabu na alipata pia kuandika vitabu vya mashairi 300. Pia ndiye mwanamke wa kwanza kipofu kuchukua digirii ya sanaa.
Ni nini kilichomfikisha hapo Hellen si bahati wala akili nyingi alizokuwa nazo bali ni kufanya kazi kwa bidii. Hakuna kitu kinachoweza kukuzuia kuwa na mafanikio makubwa ikiwa utajitoa kwa nguvu zako zote kufanya kazi kwa bidii. Unataka mafanikio makubwa? Pesa za kutosha, jiwekee falsafa ya kufanya kazi kwa bidii.
Hii ndiyo siri kubwa ya kukutoa kwenye umaskini. Uwe unataka hutaki ukijitoa kufanya kazi kwa bidii huku ukijiwekea malengo yako vizuri, amini utafika mbali kwenye kilele kikubwa cha mafanikio. Mafanikio ni haki ya kila mtu.Anza kufanyia kazi hili leo uone mabadiliko makubwa yatakayotokea kwenye maisha yako.
Nikutakie siku njema sana na endelea kujifunza kupitia mtandao huu wa AMKA MTANZANIA kila wakati.
Kwa makala nyingine nzuri za mafanikio tembelea pia DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kujifunza zaidi.


Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
0713 048035,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s