Mabadiliko Madogo Kwenye Kisima Cha Maarifa Ili Kuboresha Zaidi.

Habari za wakati huu rafiki?
Napenda kuchukua nafasi hii kukutaarifu ya kwamba kutakuwa na mabadiliko madogo kwenye KISIMA CHA MAARIFA ili kukifanya kuwa bora zaidi. Mabadiliko haya yatahusisha ruhusa ya kuzisoma makala zilizopo kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Kuanzia tarehe 01/06/2016 makala zote kwenye KISIMA CHA MAARIFA zitaweza kusomwa na wale ambao ni wanachama pekee. Yaani ili uweze kusoma makala yoyote kwenye KISIMA unahitaji kuwa umejiunga na umelipia ada ya uanachama.
Kwa sasa makala za KURASA ZA MAISHA zimekuwa zinapatikana kwa wote, iwe umejiunga au la. Hili linakwenda kubadilika na hivyo hutaweza kusoma makala yoyote, ikiwepo ya kurasa kama hujajiunga na kulipa ada.

Kwa nini mabadiliko haya?
Mabadiliko haya yamekuja ili kuboresha zaidi makala ninazoandika kupitia kipengele cha kurasa. Badala ya kuandika makala nyingi za kawaida, nataka kuandika makala chache ambazo ni bora sana. Hivyo kipengele cha kurasa za maisha kitabeba makala ambazo ni bora zaidi ya sasa, huku tukiangalizia maeneo yote muhimu ya maisha yetu, kuanzia kazi, biashara, mahusiano, imani, afya na hata maisha ya kawaida. Kwa kusoma makala hizi za kurasa kila siku unakuwa unapata maarifa bora na hatua za kuchukua ili kuboresha maisha yako kila siku.

Pia mabadiliko haya yamechochewa na tathmini ambayo nimekuwa nafanya kila siku kupitia makala hizi. Kila kitu ninachofanya huwa napima, na ninaona malengo ya awali ya kufanya makala za kurasa kuwa bure hayaendi vile nilivyopanga yaende. Makala hizi za kurasa ndiyo zimekuwa zinaongoza kwa kuibiwa na watu wengine. Kwa kuwa watu wana uhakika ya kwamba kila siku makala ipo, wanasubiri makala iende hewani na kisha kuinakili kama ilivyo na kuzitumia kama vile ni makala zao binafsi. kwa kuziondoa kwenye kuwa bure nitapunguza nafasi ya watu kuziiba na kuzitumia kama wanavyotaka wao wenyewe.
Nataka KISIMA CHA MAARIFA kiwe kisima kweli kweli na kiwe sehemu kuu ya wale walio makini na kutaka kujifunza mambo mengi zaidi kufanya hivyo. Mara kwa mara nitakuwa naandaa makala kuhusu mambo tofauti ambayo unapaswa kuyajua ikiwemo tafiti mbalimbali za kisayansi na kijamii kuhusu mafanikio na maendeleo.

Karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA.
Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA karibu ujiunge sasa ili uweze kuendelea kusoma makala za kurasa za maisha.
Kujiunga tuma ada ya mwaka ambayo ni tsh elfu 50, kwenye namba zifuatazo; TIGO PESA AU AIRTEL MONEY 0717396253 au MPESA 0755953887, majina yatakuja Amani Makirita. Baada ya kutuma ada tuma ujumbe kwenye wasap kwenda namba 0717396253 kisha utapatiwa utaratibu wa kujiunga.
Kumbuka username na password yako.
Kwa wale ambao tayari ni wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, kumbuka username na password yako ili uweze kuzisoma makala zote zilizopo kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Mabadiliko haya hayahusu makala zilizopo kwenye AMKA MTANZANIA.
Karibu sana rafiki tuendelee kujifunza kwa pamoja ili kuyafanya maisha yetu kuwa bora zaidi.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s