Kosa Moja Kubwa Ambalo Wasomaji Wa AMKA MTANZANIA Wanalifanya Na Linawazuia Kuwa Na Mafanikio Makubwa.

Rafiki, karibu tena kwenye makala yetu ya leo kupitia mtandao huu wa AMKA MTANZANIA. Amka mtanzania tumekuwa na wewe bega kwa bega kuhakikisha ya kwamba unepata maarifa sahihi yatakayokuwezesha kufanya maamuzi sahihi kwenye maisha yako. kupitia mtandao wa AMKA MTANZANIA, na KISIMA CHA MAARIFA umekuwa unajifunza na kuhamasika kila siku, na kuweza kuchukua hatua ya kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.

Kuna kosa moja ambalo nimekuwa naona wasomaji wengi wa AMKA MTANZANIA wanalifanya, kosa hili linawagharimu sana mafanikio yao. Nimekuwa nawafuatilia wasomaji wa makala zangu kwa karibu. Nimekuwa naona mtu ambaye amekutana na makala zangu kwa siku za mwanzo anakuwa mfuatiliaji mzuri, anatoa ushuhuda wa namna anavyoyafanya maisha yake kuwa bora. Baada ya muda humwoni tena mtu huyu, akija kutokea baadaye anakuja na changamoto nyingi kuliko alizokuwa nazo mwanzo.
Hiki ni kitu ambacho nakiona kwa wengi, na sitaki kikukute na wewe rafiki yangu, ambaye bado hujafanya kosa hili.

Kosa kubwa ambalo baadhi ya wasomaji wa AMKA MTANZANIA amekuwa wanalifanya ni kuamua KUHITIMU mafunzo haya. Wasomaji hawa wanafika mahali na kuona sasa tayari wameshajua kila kitu na hawana tena haja ya kuendelea kusoma na kujifunza. Wanakuwa wanaona wameshajua kila kitu na wapo tayari kuendelea na mambo yao bila ya kujifunza zaidi.

Hili ni kosa kubwa mno ambalo limewagharimu wengi mafanikio yao. Watu wanakuwa wameanza kuona mafanikio kwenye maisha yao, ghafla kila kitu kinaanza kwenda hovyo. Hii ni kutokana na kamba wamekata ule mzizi ambao umeshikilia mafanikio yao, ambao ni maarifa na taarifa sahihi za kuwawezesha kufanya maamuzi bora na sahihi.
Kujifunza na kuhamasika ni kama chakula, huli mara moja na ukasema tayari umetosheka kwa maisha yako yote. Bali unaendelea kula kila siku, kwa sababu unachokula leo, kesho kinapotea. Hivyo pia kwenye kujifunza, unachojifunza leo, kesho kinakuja kipya kabisa. Unapohamasika leo, kesho unakutana na wakatishaji tamaa wakubwa kuliko uliokuwa nao leo.

Dunia inayokuzunguka haitaki kukuona ukipiga hatua kubwa ya kuwa na mafanikio kwenye maisha yako. Hivyo wazingira na wanaokuzunguka wanahakikisha wanakuwekea kila aina ya kikwazo usiweze kupiga hatua. Wakati mwingine wanafanya kwa kujua, wakati mwingine hata hawajui.

Silaha yako pekee ya kushinda vita hii ni kuwa na taarifa na maarifa sahihi, yanayokupa hamasa na uwezo wa kufanya maamuzi bora ya maisha yako.

Elimu hii unaipata kwa uhakika kupitia AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA , kila siku. elimu hii haina mwisho, hakuna kuhitimu wala hakuna cheti, cheti chako ni maisha yako kuwa bora.

Kama kweli unataka kuchukua hatua kubwa kwenye maisha yako, kama kweli unataka kuwa na mafanikio yanayodumu na siyo ya kupanda na kushuka, basi hakikisha kila siku unapata taarifa na maarifa sahihi kupitia AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA.
Nimekuwa msomaji wa kila siku wa vitabu kuanzia mwaka 2012, mwaka 2014 nilianzisha kikundi cha kusoma vitabu viwili kila wiki. tangu kipindi hiko haiwezi kupita siku sijasoma kitabu. 

Kila wiki nasoma vitabu viwili, na kama nimebanwa sana basi angalau kitabu kimoja. Vitabu vingi ninavyosoma vinaendana, mawazo ni yale yale, lakini hata siku moja sijawahi kujidanganya kwamba hiki tayari najua, bali nimekuwa nakaa na kusoma kitabu. Na mara zote kuna kitu kipya ambacho nimekuwa nakipata kupitia kila kitabu.

Hii ndiyo hatua ambayo hata wewe unapaswa kuichukua, hata siku moja usithubutu kujiambia kwamba tayari unajua kila kitu, ukilinganisha vitu unavyojua sasa na vile unavyopaswa kuvijua, ni sawa na hujui chochote.
Hatua muhimu kwako kuchukua.
1. kila siku ingia kwenye AMKA MTANZANIA, www.amkamtanzania.com na kujifunza. Zipo makala zaidi ya 1000 ambazo ni nzuri sana kwako kupata maarifa na taarifa sahihi.

2. Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA, www.kisimachamaarifa.co.tz ka kulipia ada ya uanachama wa mwaka ili uweze kusoma makala za kila siku, na pia kuwa kwenye kundi la wasap ambapo utajifunza na kuhamasika kila siku.

3. Jiunge na mfumo wetu wa email, na utakuwa unapokea makala za mafunzo na hamasa moja kwa moja kwenye email yako. Kujiunga na mfumo huu wa email bonyeza maandishi haya na ujaze fomu.

Nikukumbushe lile muhimu zaidi rafiki, karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA, na muhimu zaidi, elimu hii haina kuhitimu, siku utakayochagua kuhitimu, basi jua ndiyo siku unayoanza kupotea.

Jifunze kila siku, na kila siku chukua hatua ya kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi. Nikukumbushe tena rafiki, hili ni zoezi la kila siku, mpaka siku ambayo unaondoka hapa duniani, hakuna kuhitimu kwa namna yoyote ile. Karibu sana tuwe pamoja.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: