Siri Ya kudumu Katika Mahusiano Ya Ndoa.

Sabrina Adriani ni miongoni mwa wanawake ambao wamedumu miaka mingi katika ndoa. Na alipoulizwa ni kwanini ameweza kukaa kwa miaka mingi katika ndoa bila kufarakana na mumewe alisema “siri kubwa ambayo imenifanya nidumu katika ndoa ni kwamba niliweza kutumia muda mwingi zaidi ya miaka kumi kuweza kumfahamu mume wangu vizuri, ninaposema kumfahamu hapa nina maana ya kwamba kujua tabia zake zote kiundani zaidi, nilifanya hivi ili kujua ni kipi hapendi na kipi anakipenda? baada ya kujua hivyo nikaweza kuishi naye vizuri maana wanasema ya kwamba mkimjua mbwa jina hakusumbui.”
Lakini sikuishia hapo nikaweza kutenga muda wangu angalau mara tatu kwa wiki kusoma saikolojia ihusuyo mahusiano hicho ndicho kitu kikubwa ambacho kimenisaidia.
Pia Sabrina hakuishia hapo aliendelea kusema ya kwamba moja ya sababu kubwa ya kufa kwa ndoa nyingi barani Afrika na duniani kote ni kutoshukuru kwa chochote ambacho amekipewa na mumewe, akatoa mfano ya kwamba utakuta mtu ameletewa zawadi na muwewe lakini kwa kuwa hajaipenda zawadi hiyo, utashangaa majibu ambayo yanamtoka kinywani mwa mwanamke huyo baadala ya kushukuru, utakuta mtu anasema ni kitu gani hiki ambacho umekileta? Na majibu mengine mengi kama hayo. 

Kwahiyo hiyo ndio sababu kubwa ya kufa kwa ndoa nyingi, hivyo baada ya mimi kufunga ndoa hata zawadi iwe nzuri au mbaya nilikuwa namshuru muwe wangu kwa kile ambacho ameniletea ili kumridhisha mume wangu, na nilifanya  hivyo ili kumthihirishia ya kwamba nimefurahi kwa zawadi aliyoniletea pia najivunia kuwa na yeye, pia nilifanya hivyo kila mara ili kutomkatisha tamaa na azidi kuelewa ya kwamba mimi ni mwanamke tofauti na wanawake wengine.
Lakini kabla hajamaliza kuzungumza siri ambazo zilimfanya  kukaa kwenye ndoa muda mrefu, alizungumzia muda mzuri ambao unafaa katika kufanya mazungumzo na mwezi wako, katika hili alisema ” katika tafiti ambazo zimewahi kufanywa miaka ya nyuma na watu ambao wanahusika na masuala ya saikolojia ya mahusiano waligundua ya kwamba mwanamke nyakati za asubuhi huwa hana uwezo mkubwa kuzungumza maneno mengi, ila nyakati za usiku huwa ana uwezo kuzungumza maneno mengi sana ambayo ndani ya maneno hayo huwa ni jazba au kwa maneno mengine tuite maneno yasiyo na mpangilio. 
Na kwa upande wa mwanaume ana uwezo wa kuzungumza maneno mengi sana wakati wa asubuhi kuliko nyakati jioni au usiku, hii ni kutokana na shughuli nyingi ambazo mwanaume huyo huzifanya kwa siku nzima, hivyo mwanaume anahitaji muda mzuri nyakati za jioni kwa ajili ya kupumzika.
Hata kwa kuwa wengi hawajui siri hii utashangaa mwanamke anamfokea mwanaume wake nyakati za usiku na kwa kuwa mwanaume kama nilivyosema hapo awali ya kwamba mwanaume nyakati za jioni au usiku huwa hapendi kuongea utashangaa mwanamke huyo anapigwa na mumuwe.
Hivyo basi baada ya kujua siri hii nikajua ya kwamba wakati mzuri ambao utatufaa mimi pamoja na mume wangu kwa ajili ya kuzungumza ni wakati wa asubuhi, muda huu ni mzuri kwa sababu  mume wangu  akili yake inakuwa imetulia na anakuwa ana uwezo mzuri kuzungumza. Hivyo nyakati hizo za asubuhi huwa natumia kuzungumza naye kuhusu masuala ya mafanikio na familia kwa ujumla.
Baada ya kusema hayo akawasisitiza wanandoa wote waweze kuyazingatia hayo ambayo yamemsaidia yeye kuweza kudumu katika ndoa. 
Bila shaka naamini ya kwamba umejifunza mambo mazuri kutoka kwa mwana mama Sabrina, hivyo nikusihi na wewe uweze kuyazingatia hayo machache  katika mahusiano yako ili kuweza kutengeneza mahusiano yaliyo bora kila wakati. Na mpaka kufikia hapo sina la ziada tukutane siku nyingine.
Makala hii imeandikwa na afisa mipango Benson Chonya,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: