Unaendeleaje na harakati za kuyaboresha maisha yako rafiki yangu?

Ni imani yangu kwamba unaweka juhudi kubwa zaidi kila siku ili kuhakikisha maisha yako yanazidi kuwa bora zaidi kila siku. Vitu vyote vizuri vinakuja baada ya kuweka juhudi, hakuna kinachokuja kiurahisi. Hivyo endelea kuweka juhudi kubwa ili kupata matokeo bora zaidi.

Kazi kubwa ya vyombo vya habari ni kuwapasha watu habari. Kutoa taarifa ambazo zinawafanya watu kujua ni nini kinachoendelea. Ili kuhakikisha vinapata watu wengi wa kuvifuatilia, vyombo vya habari vimekuwa vinatumia hofu, watu wanaendeshwa na hofu na hivyo habari zinapokuwa za hofu zinawasisimua wengi.

Kwa kifupi tunaweza kusema ya kwamba vyombo vya habari vinatumia hofu za watu ili kuhakikisha vinapata wafuasi wengi zaidi. Vinazipa kipaumbele habari za hofu na ambazo ni hasi na watu wanazidi kufuatilia habari hizo zaidi. Kwa mfano kama kuna habari mbili, moja ni ya mwanasayansi mmoja kugundua dawa ya kutibu ugonjwa fulani na nyingine ya mtu mmoja ameua watu watatu, habari itakayopewa kipaumbele ni ile ya mtu aliyeua, japo ya kupatikana kwa sawa ni muhimu zaidi, habari ya mauaji inasisimua zaidi, inawapa watu hofu zaidi.

SOMA; Kwa Nini Habari Hasi Zinavuma Na Kupendwa Sana Na Wengi, Na Jinsi Ya Kujitoa Kwenye Mkumbo Huo.

Changamoto kubwa ya zama tunazoishi sasa ni kwamba vyombo vya habari siyo redio, tv na magazeti pekee, sasa hivi mitandao ya kijamii imekuwa kama vyombo vya habari. Na pia habari haitoki kwa waandishi wa habari pekee, bali zama hizi kila mtu ni mwandishi wa habari. Kila mtu popote alipo anapokutana na jambo la hofu, mara moja anakimbilia kuliweka kwenye mtandao. 

Mtu ameona ajali inatokea, badala ya kutoa msaada wa kuokoa, kwanza anapiga picha na kuzituma kwenye mtandao. Hii ni kwa sababu habari hasi zinawasisimua wengi kuliko habari chanya. Pia watu wengi wanapenda kuwa wa kwanza kutoa taarifa za habari za kusisimua.

Hizi ni nyakati ngumu na zenye changamoto mno kuishi, kwa sababu kila sekunde ya muda wetu, kuna habari nyingi mno ambao zinaletwa mbele ya macho yetu. Kwa kuingia tu kwenye mtandao, unakutana na habari nyingi mno kuliko unavyoweza kuzisoma zote, na nyingi ya habari hizo ni hasi na zenye kukupa hofu.

Kipo kitabu muhimu kwako kusoma ili uweze kuvuka changamoto hii ya zama hizi. Kitabu hichi kitakuwezesha kuidhibiti akili yako, kutokuianza siku yako kwa habari na hivyo kuwa na fikra sahihi za kuianza siku yako. Unaianza siku yako kwa hamasa kubwa ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa.

Ngoja nikupe mifano miwili na uniambie wapi mtu anaweza kufanya makubwa kwenye siku yake;

Mfano wa kwanza; mtu ameamka asubuhi na kufungulia habari ambapo amepata habari za mtu mmoja kuua mwenzake, mapigano ya wakulima na wafugaji yamesababisha vifo, magaidi wamesababisha milipuko na kuua watu, pia hai ya uchumi inazidi kuwa ngumu. Anamaliza hapo na kwenda kuanza kazi zake.

Mfano wa pili; mtu ameamka asubuhi, kaipangilia siku yake, na kaanza kwa kusoma kitabu kizuri cha hamasa, ambacho kinamwambia anaweza kufanya makubwa, kinampa mbinu za kujijengea nidhamu ya uwajibikaji na kutumia muda wake vizuri. Anamaliza hapo na kwenda kuanza kazi zake.

Unafikiri kati ya watu hawa wawili, yupi ambaye ataianza siku yake akiwa na hamasa kubwa ya kufanya kazi? Yupi ambaye atakuwa tayari kuweka juhudi kubwa akijua ya kwamba atapata matokeo bora zaidi?

Bila ya shaka tunakubaliana kwamba yule aliyeanza kwa kujifunza kwa kusoma kitabu chenye hamasa na mafunzo mazuri. Ila yule aliyeanza na habari hasi, anaianza siku yake akiwa na hofu, akiwa ameshakata tamaa kabisa na kuona dunia inaelekea mwisho kabisa.

Ukweli ni kwamba dunia haielekei mwisho, angalau siyo kwa siku za karibuni. Na kadiri siku zinavyozidi kwenda maisha yanazidi kuwa bora zaidi kuliko ya nyuma. Kama wewe umezoea kufuatilia habari tu, huwezi kuona haya ninayokuambia, kwa sababu hayana faida kihabari.
Ili kuweza kuvuka zama hizi salama, uachwe kuendeshwa na hofu za mambo kuwa mabaya na magumu zaidi, uweze kuianza siku yako ukiwa na hamasa kubwa ya mafanikio, kipo kitabu muhimu unachopaswa kukisoma. Kitabu hiki kitakuwezesha wewe kuianza siku yako kwa kujifunza, kitakuwezesha kupata muda zaidi kwenye siku yako kwa kuchagua aina ya habari unazotaka kuzifuatilia.

Kitabu hicho ni PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU, kitabu ambacho kinakuwezesha wewe kusimamia na kudhibiti matumizi ya muda wako. Kinakufanya wewe kuwa kiongozi wa maisha yako, kuweza kuchagua kufanya yale muhimu na kuacha yale ambayo siyo muhimu.

Katika kipindi hichi ambacho kila mtu anaweza kuripoti habari, unahitaji ulinzi mkubwa sana kwenye muda wako. Pata na usome kitabu hichi, kitakuwezesha kuacha kuwa mteja wa habari hasi na kukupa muda zaidi kwenye siku yako.

SOMA; Kama Kitu Hakina Sifa Hizi Tatu Usikisome Na Okoa Muda Wako Ili Ufanye Vyenye Manufaa Kwako.

Watu wengi wamekuwa wakifikiri hawawezi kuzianza siku zao bila habari, hii ni kwa sababu ndiyo maisha ambayo wameyazoea, lakini kwa kusoma kitabu hicho, nitakuonesha namna unavyoweza kuwa na maisha bora bila ya kuongozwa na habari.

Jipatie kitabu hichi kizuri na ukisome. Kitabu kipo kwenye mfumo wa softcopy na kinatumwa kwa email. Unaweza kukisomea kwenye simu yako, tablet au kompyuta. Kitabu hichi kinapatikana kwa gharama ndogo ya tsh 5,000/=. Kupata kitabu hichi, tuma fedha, tsh 5,000/= kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253 (kama unatumia airtel money tuma moja kwa moja kwenda namba ya tigo). Ukishatuma fedha, tuma ujumbe wenye email yako pamoja na jina la kitabu MASAA MAWILI na kisha utatumiwa kitabu chako.

Karibu sana upate maarifa ya kukuwezesha kuvuka changamoto kubwa ya zama hizi ambazo kila mtu ni mwandishi wa habari na kila mtandao wa kijamii ni chombo cha habari. Bado unaweza kushika hatamu ya maisha yako na ukazingatia yale ambayo ni muhimu kwako.

Soma kitabu hichi sasa na uwe na maarifa sahihi ya kusimamia na kudhibiti matumizi ya muda wako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.