SEMINA; Elimu Ya Msingi Ya Fedha (Basic Financial Education).

Habari za leo rafiki yangu,

Mwanzoni mwa mwaka huu 2017 niliendesha semina yetu ya kwanza ya mwaka 2017 kwa njia ya mtandao. Na nilikuahidi nitakuwa na semina mbili tu kwa mwaka huu 2017, ile ya kwanza ya mwanzoni mwa mwaka, na ya pili katikati ya mwaka 2017. Kama ulishiriki semina ya mwanzo wa mwaka, nina imani yapo mengi uliyojifunza na ambayo unayafanyia kazi mpaka sasa. Ikiwepo kauli mbiu yetu ya mwaka huu wa mafanikio 2017 ambayo ni KUTHUBUTU, USHINDI na SHUKRANI. Haya ni maneno matatu ambayo yana maana sana kwetu mwaka huu 2017.

 

Sasa kama nilivyokuahidi, umefika wakati sasa wa kupata semina yetu ya pili, ambayo itakuwa kwa njia ya mtandao kama ile ya kwanza. Hii ni semina ya pili na ya mwisho kwa mwaka huu 2017, itakuja nyingine lakini hii itakuwa siyo kwa njia ya mtandao, bali kwa kuhudhuria. Nitatoa taarifa zaidi kuhusu semina hii kuanzia mwezi wa saba.

Napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha kwenye semina ya ELIMU YA MSINGI YA fedha (BASIC FINANCIAL EDUCATION). Hii ni semina ya kipekee kabisa kwetu, ambapo tunakwenda kupata maarifa sahihi kuhusu fedha. Hii ni elimu muhimu sana ambayo hatukupata bahati ya kuipata kwa kina. Mashuleni haifundishi, na hapa kwenye jamii zetu, ukitaka kugombana na watu, basi anzisha mjadala wa fedha. Ukionekana unaongea sana kuhusu fedha basi unaonekana una tamaa au una roho mbaya. Lakini cha kushangaza, kila mtu hapati usingizi vizuri usiku linapokuja swala la fedha, hasa nyakati zinapokuwa ngumu.

Nimekuwa naandika makala nyingi kuhusu fedha, kwenye AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA, pia nimeandika kwenye kitabu cha KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI, lakini makosa ninayoona watu wanayafanya kwenye fedha, naona tunahitaji semina nzito na ya maana kwenye eneo hili la fedha. Hivyo nimekuandalia semina ya siku kumi kupitia mtandao, ambayo itafanyika kwa njia ya wasap ambapo tutakwenda kujifunza mambo yote muhimu na ya msingi kabisa kuhusu fedha.

SOMA;Hizi Ni Sababu Kwa Nini Baadhi Ya Watu Wanaopata Fedha Nyingi Huishia Kufa Masikini, Na Hatua Za Wewe Kuchukua.

Tutaichambua fedha kuanzia kwenye maana yake, na msingi wake. Kila kitu kina misingi yake, na fedha nayo ina misingi yake. Kutokuijua misingi hii utapata shida sana. Zipo pia sheria za fedha, ambazo wanaozijua wanaziheshimu na kuzifanyia kazi, ila huwa hazifundishwi, na wale wasiozijua wanazivunja kila siku kama wanavyojisikia wao wenyewe. Hili ni eneo ambalo lazima ulijua, la sivyo matatizo ya fedha hayataondokana na wewe.

Pia tutaangalia kwa kina kuhusu kupata na kutumia fedha. Najua wengi tunachojua ni kuzipata fedha, baada ya hapo zinajijua zenyewe. Sasa kupitia semina hii tutakwenda kuchimba kwa undani kuanzia kipato mpaka matumizi. Namna ya kuongeza kipato na kuwa na mifereji mingi ya kipato.

Tutakwenda kuangalia eneo jingine muhimu sana kwenye fedha ambalo ni uwekezaji. 

Hakuna mtu anayekuwa tajiri bila ya kuwekeza. Uwekezaji hauepukiki linapokuja swala la fedha na utajiri. Lakini cha kushangaza, watu wengi hawajui kabisa kuhusu uwekezaji. 

Ukitaka kumpoteza mtanzania wa kawaida, mwulize anajua nini kuhusu hisa. Ni kitu ambacho kinaogopwa na wengi, lakini ni kitu kinachoeleweka na ambacho kina misingi yake. Hivyo kwenye semina hii, tutayaangalia maeneo yote tunayoweza kuwekeza, kuanzia kwenye ardhi, majengo, hisa, vipande, hatifungani, biashara na kadhalika.

Kitu kimoja muhimu ambacho utajifunza kwenye semina hii, ambacho hujawahi kujifunza popote ni jinsi ya kurithisha elimu hii ya msingi ya fedha kwa watoto wako. Kwa sababu wazazi wengi huwa tunawatenga watoto mbali kabisa na fedha. Tunaona wakati wao bado na wao wakazane kusoma au kufanya mambo yao. Inapotokea mzazi amefariki na watoto wakarithi mali, basi ndiyo unakuwa mwisho wa mali zile. Zinatumiwa hovyo, kuuzwa na kupotea kabisa. Sasa sisi tunakwenda kulizuia hili, kwa kuhakikisha tunaondoka na msingi wa kuwajengea watoto wetu kuhusu fedha.

Eh! Ni vitu vingi hivyo, halafu vyote lazima viishe ndani ya siku kumi. Hivyo nakuhakikishia zitakuwa siku 10 za mchaka mchaka wa kipekee, lakini baada ya hapo, utaondoka na amani ya moyo linapokuja swala la fedha kwako na hata kwa vizazi vyako. Sijui utajiteteaje pale utakapokosa semina hii ya kipekee sana, ambayo unaweza kushiriki popote pale ulipo duniani, na wala haikutaki uache kufanya kile unachofanya sasa. Na taarifa nimekupa mapema sana, kiasi kwamba unaweza kujichanga na kuhudhuria semina hii.

Hii siyo semina ya kukosa rafiki yangu, maana tutakwenda kufanya mapinduzi makubwa kwenye uelewa wetu wa kifedha na kuweza kuchukua hatua na kuwa bora zaidi.

SOMA; Jinsi Unavyoweza Kuwa Sumaku Ya Fedha, Njia Kumi (10) Za Kuivuta Fedha Ije Kwako Muda Wote.

GHARAMA ZA KUSHIRIKI SEMINA HII.

Hii ni semina ya bure kabisa kwa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo hakuna ada ya kushiriki semina hii. Unachopaswa ni uwe mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA ambaye ada yako itakuwa haijamaliza muda wake wakati huo wa semina.

Kwa wale ambao siyo wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, ili uweze kushiriki semina hii, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo ni Tsh 50,000/=. Unapolipa ada hii unapata nafasi ya kusoma makala kwenye blog ya KISIMA CHA MAARIFA na pia kuwa kwenye kundi la wasap kwa mwaka mzima, ambapo kila siku unajifunza. Unapolipa ada hiyo ya elfu hamsini ni kwa maka mzima, yaani miezi 12 baada ya kulipa. Kama umelipa mwezi wa tano 2017 basi ada hiyo itaisha mwezi wa tano 2018.

Hivyo rafiki yangu, ambaye ungependa sana kushiriki semina hii, ila bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA unachopaswa kufanya sasa, ni kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kujiunga unatuma ada tsh 50,000/= kwa namba za simu 0717 396 253 au 0755 953 887 majina yatakayokuja ni Amani Makirita. Ukishatuma fedha, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 na utaweka kwenye kundi la 
KISIMA CHA MAARIFA na kuwa na uhakika wa kushiriki semina hii.

SEMINA NI LINI?

Semina hii ya kipekee itaanza jumatatu ya tarehe 03/07/2017 na kumalizika ijumaa ya tarehe 14/07/2017. Hizi ni siku muhimu sana kwetu kwa mwaka huu 2017 maana tunakwenda kutengeneza mapinduzi ya kifedha kwenye maisha yetu.

MWISHO WA KUJIUNGA KWA WASIO WANACHAMA.

Ili tuweze kwenda sawa, semina hii tunapaswa kuanza wote kwa pamoja na kumaliza wote kwa pamoja. Hivyo ikishaanza huwezi kuingia katikati, hii ina maana kwamba hakuna mtu yeyote atakayepokelewa katikati ya semina.
Ili kuhakikisha unapata nafasi ya kushiriki semina hii, unapaswa kuwa umelipa ada yako mpaka kufikia ijumaa ya tarehe 30/06/2017. Baada ya siku hiyo, hutaweza tena kupata nafasi ya kushiriki semina hii.

Hivyo rafiki yangu, nakushauri ufanye uchukue hatua mapema, ama ulipe sasa, na kuendelea kujifunza huku umejihakikishia kushiriki. Au uandike mahali ambapo kila siku utaona kwamba unahitaji kulipia semina hii na uweze kulipa kabla ya tarehe ya mwisho kulipa haijapita.

Nakusisitiza hivi kwa sababu kwa uzoefu, watu wengi wamekuwa wanajisahau na wanapouja kukumbuka muda unakuwa umeshapita. Sitaki wewe rafiki yangu ukose nafasi hii. Utakuwa umekosa kitu kikubwa sana kwenye maisha yako.

Mwisho kabisa naomba niwasaidie wale watakaokuja na sababu za kushindwa kushiriki, kwa kuweka majibu ya maswali ambayo kwa uzoefu wengi huwa wanauliza.

Ada ni kubwa sana.

Ndiyo, ni kweli kabisa ada ni kuvwa, elfu 50 siyo ndogo. Ila kumbuka utajifunza mwaka mzima, na semina ya mwanzoni mwa mwaka 2018 pia utashiriki bila kulipa ziada.

Kama kweli unataka kushiriki semina hii, ada kamwe haiwezi kuwa kikwazo. Kwa sababu ukihesabu kuanzia leo, kuna ziku zaidi ya 50 mpaka kufikia semina. Hivyo kama kila siku utaweka pembeni tsh elfu moja tu, utaweza kushiriki semina hii.

Je naweza kulipa kidogo kidogo?

Ndiyo unaweza, ila hakikisha unakuwa umekamilisha mpaka kufikia tarehe ya mwisho ya kulipia. Pia hutawekwa kwenye kundi mpaka uwe umekamilisha malipo yako.

Ni manufaa gani zaidi nitapata ukiacha semina?

Utaweza kusoma makala nzuri kuhusu biashara, fedha, uwekezaji, na mafanikio kwenye KISIMA CHA MAARIFA kwa mwaka mzima. Pia kwenye kundi la wasap kila siku unajifunza na kila jumapili huwa tuna darasa la jumapili ambapo tunajifunza mambo muhimu kwa mafanikio.

Rafiki, nimalize kwa kusema, hii siyo semina ya kukosa. Itafanya makubwa kwenye maisha yako, na kumbuka haitajirudia tena.

MUHIMU; NIAMBIE KIPI UNATAKA KUJIFUNZA ZAIDI KWENYE SEMINA HII.

Nimekupa kwa ujumla yale ambayo tutajifunza kwenye semina hii. Lakini sijakupa mgawanyiko wa masomo yatakuwaje. Na nimefanya hivi kwa makusudi kwa sababu nataka semina hii iwe yako zaidi. Hivyo kama una uhakika utashiriki semina hii, niambie kile ambacho ungependa kujifunza zaidi kuhusu fedha na utajiri. Uliza swali lolote kwa kujibu email hii au kwa kutuma maelezo yako kwa njia ya email kwenda kwenye email yangu ya amakirita@gmail.com Nitaomba uandike kwa ufafanuzi mzuri ili niweze kukuelewa moja kwa moja na nitatumia maswali na maoni yenu katika kupanga mtiririko wa masomo ya semina hii. Kadiri utakavyoniandikia mapema, ndivyo nitakavyofanyia kazi kile unachopenda kujifunza.

Karibu sana rafiki, andika mahali hili ili usisahau. Nitaendelea kukukumbusha mara kwa mara ili wewe kama rafiki yangu usiikose fursa hii ya kipekee kwenye maisha yako.

Mimi rafiki na kocha wako,

Makirita Amani.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: