Habari za wakati huu rafiki yangu,

Hongera kwa kuonesha nia ya kupenda kupata mafunzo ya semina ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, mafunzo ambayo yatakuwezesha kujijengea uhuru wa kifedha na utajiri. Hongera sana kwa hatua hii.

Napenda kuchukua nafasi hii kukupa sababu pekee ya mimi kurudia mafunzo haya ya semina ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA. Kila mwaka huwa kuna idadi ya semina naziendesha kwa njia ya mtandao na njia ya ana kwa ana. Huwa napanga mapema kabisa na vigezo vya kushiriki semina hizo. Na semina ikishapita, huwa sirudii tena, ni mpaka baadaye sana, labda mwaka kupita nakuja kutoa kitabu kinachotokana na semina ile.

Wakati semina ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA inaendelea, washiriki wengi walikuwa wakiona namna gani wamekuwa wanafanya makosa kwenye fedha, hasa kwenye matumizi, madeni na uwekezaji. Na wengi walikuwa wakiwasikitikia wale ambao wameshindwa kushiriki semina hii. Wakisema watu hao wamekosa msingi muhimu mno kwenye maisha yao.

Unaweza kuona maoni hayo hapo chini, na pia nimeweka picha ya mjadala halisi kwenye kundi la wasap;

Asante Coach.

Binafsi Namshukuru Mungu kuniweka hapa. Ni sawa na Mtume Yohana alivyofunuliwa siri za mbingu na motoni. Tujiulize je wale ambao hawamo humu sasa hivi na ambao hawatapata kabisa elimu hii watakuwa je. Sijutii Kuwa hapa. It’s never too late jamani msijilaumu tufanye kitu sahihi hata kama una 50yrs una ndugu watarithi na huwezi jua Mungu atakupa muda gani wa uhai. – Sebastian Kalugulu.

Naamini baadaye kocha atatoa hii kama kitabu. Itakuwa vizuri kwa ajili ya kuwashirikisha wengine ambao hawakushiriki. – MTABAZI GEOFREY SAHINI

Hiyo ni sehemu ndogo tu ya maoni ya wasomaji juu ya semina hii. Wengi walifunuliwa na kuona mambo ambayo wamekuwa hawayaoni siku zote.

Ni kweli kabisa nimepanga kutoa kitabu kuhusiana na mafunzo ya semina hii. Lakini kitabu kinachukua muda mpaka kitoke, siyo chini ya mwaka mmoja kutoka sasa. Hivyo hilo litawachelewesha wengi kupata elimu hii. Kwa sababu nataka kukuhakikishia jambo moja, kama hutapata elimu hii kwa mwaka mmoja kutoka sasa, utakuwa umepoteza fedha nyingi mno, siyo chini ya milioni moja, hata kama huna kipato kwa sasa. Kama huamini utaona mwenyewe kwenye semina hii.

Kitu kingine muhimu ni kwamba, kitabu ni bubu, kitabu utakisoma na kukazana kuelewa mwenyewe kwa kadiri utakavyoweza. Lakini semina hii, japo ni kwa njia ya mtandao, ni hai, ikiwa na maana kwamba, chochote ambacho utakuwa hujaelewa, unaweza kuuliza moja kwa moja na nikakupa majibu ya kina. Kwenye kila siku ya semina, kuna nafasi ya kuuliza maswali kwenye masomo ya siku husika, hapo unauliza kila kitu unachotaka kujua.

Hii ndiyo imepelekea mimi kurudia semina hii kwa wale ambao wameikosa, na nimeondoa kila sababu za kuikosa. Kwa sababu awali gharama za kushiriki ilikuwa tsh 50,000/= sasa hivi utashiriki semina hii kwa shilingi elfu 10,000/=. Hebu ona hapo rafiki, kutoka shilingi elfu HAMSINI mpaka ELFU KUMI, hiyo yote ni kuhakikisha wewe unapata mafunzo haya.

Rafiki yangu, ninachokuambia ni hichi, chukua hatua sasa hivi, siyo leo, sasa hivi. Lipa ada ya kushiriki semina hii tsh 10,000/= kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253 (majina; AMANI MAKIRITA) Kisha tuma ujumbe kwenye wasap namba 0717396253 wenye majina yako kamili na neno SEMINA YA FEDHA na nitakuweka kwenye kundi la semina.

Nakusisitiza tena rafiki yangu, usichelewe ukakosa tena semina hii, kwa sababu utakuwa umejinyima kitu kikubwa sana kwenye maisha yako. Fanya malipo sasa, kwa sababu nafasi ni chache. Semina tunaiendesha kupitia kundi la wasap, na ninaweza kuendesha kundi moja tu kwa wakati, hivyo likishajaa sina nafasi nyingine tena kwako.

Karibu sana rafiki upate elimu sahihi ili kuboresha maisha yako kwa kufikia uhuru wa kifedha na utajiri. fanya malipo sasa, tsh 10,000/= kwa namba 0717396253 au 0755953887. Karibu sana.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,