Ili kukamilisha jambo lolote, ni muhimu sana jambo hilo kuliweka kwenye akili yako kila mara. Inatakiwa liwe jambo ambalo unalifikiria kila wakati kwa kutafuta kila aina ya njia kuweza kulitimiza, bila ya hivyo huwezi kufanikisha jambo hilo.

Watu wengi wanashindwa kuishi maisha ya ndoto zao kwa sababu ya kushindwa kuweka akilini yale mambo ambayo wanataka kuyatimiza. Utakuta mtu ana lengo labda la kutengeneza saluni, lakini utakuta akili yake inawaza mambo mengine tofauti.

Sasa kwa mtindo huo huwezi kufanikiwa. Kila wakati unatakiwa jambo unalolitaka ulifanikishe  kwenye maisha yako, unatakiwa kuliweka kwenye akili yako sana, hapa yaani inatakiwa jambo hilo uwe na picha nalo kamili na inayoeleweka.

brain fit press release elementsInapotokea unataka kulipotezea inabidi kulirudisha mara moja kwenye akili yako tena. Inapotokea kuna mambo yakaingiliana na ukajikuta unasahau jambo lako unalotaka kulitimiza hata kwa bahati mbaya, unatakiwa kulirudisha mara moja akilini wako.

Ikiwa hautafanya hivyo, elewa kabisa hautaweza kufanikiwa kwani akili yako kwa jinsi ilivyo kimaumbile, haiwezi kukupa jambo ambalo hulizingatii, unapata kile unachokizingatia kwenye akili yako bila kujali sana kitu hicho ni kizuri au ni kibaya kwako.

Kwa msingi huo hapa unapata picha kwamba, ili kufanikiwa unahitaji si kuweka tu nguvu za uzingativu eneo moja unalotaka ufanikiwe, bali unatakiwa kufanya kitu cha zaida kwa kuweka nguvu endelevu za uzingativu kwa kile unachotaka kufanikiwa.

Kwa hiyo msisistizo wako si kuzingatia kile unachokitaka kwa leo tu na kesho ukaacha, unatakiwa kujikumbusha kila siku na kila mara mpka jambo hilo unalolitaka ili liweze kuumbika ipasavyo kwenye akili yako. kwa njia hiyo utalifanikisha.

Unayo nafasi kubwa sana ya kufikia ndoto na maisha ya mafanikio ikiwa utaweka uzingativu. Wengi wanajikuta wanashindwa kufikia mafanikio kwa kukosa uzingativu na mwelekeo. Haya ni mambo ambayo yanawaangusha wengi sana.

Jiulize ndoto zipi ulizonazo? maisha yapi ambayo unayotaka? au ni kitu gani unachotaka kukitimiza kwenye maisha yako? Kitu hicho jifunze kukiweka kwenye akili yako sana, ikiwezekana kitengenezee picha yake uwe unakiona mara kwa mara.

Ukiweka sana kwenye akili yako jambo unalotaka kulitimiza. Uwe na uhakika jambo hilo utaweza kulifanikisha na ndoto zako zitatimia. Nini unachosubiri sasa? Chukua hatua kwa kuweka akilini sana jambo unalolitaka ili ufanikiwe.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kila siku kujifunza maisha na mafanikio.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,

Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,

Tovuti; http://www.amkamtanzania.com

Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com