Habari za leo rafiki yangu?

Napenda kuchukua nafasi hii kukushirikisha utaratibu na mwaka wetu wa mafanikio 2017/2018 ambao umeanza mwezi huu wa kumi na moja mwaka 2017 na utamalizika mwezi wa kumi mwaka 2018.

Huu ni mwaka tofauti na wa kipekee kwa wanamafanikio, mwaka ambao tunapanga kufanya makubwa na tunayafanyia kazi kweli ili kuweza kuyabadili maisha yetu na kufanikiwa zaidi.

Mwaka wetu wa mafanikio tunaupima kwa wiki, yenye siku saba kuanzia jumatatu mpaka jumapili.

Ndani ya mwaka zipo wiki 52, ambapo mipango yetu inakwenda kwa wiki hizo.

Msingi Mkuu

Utaratibu wa kujifunza kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Kila siku kutakuwa na TAFAKARI ya kuianza siku, ambayo inatufanya tufikiri na kuchukua hatua za tofauti kabisa. Tafakari hii inatumwa kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, pia kuwekwa kwenye blog.

Kila wiki, siku ya jumapili saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku tunakuwa na darasa la jumapili. Darasa hili linaendeshwa kupitia mtandao wa wasap. Kwenye madarasa haya tunajifunza na kushirikishana mambo muhimu katika kuishi maisha ya mafanikio.

Jumapili ya kwanza ya mwezi tutakuwa na darasa linalohusu mafanikio na falsafa ya maisha ya mafanikio. Hapa tunajijengea na kuimarisha misingi yetu ya maisha ya mafanikio.

Jumapili ya pili tunakuwa na darasa linalohusu biashara na biashara. Hapo tutajifunza mambo muhimu ya kuzingatia katika shughuli zetu mbalimbali tunazofanya ili kuweza kufanikiwa zaidi.

Jumapili ya tatu tutakuwa na darasa linalohusu FEDHA NA UWEKEZAJI. Hapa tutajifunza mambo yote muhimu kuhusu fedha, kuanzia kuongeza kipato, kudhibiti matumizi, kuweka akiba na kuwekeza.

Jumapili ya nne tutakuwa na darasa la uchambuzi wa KITABU CHA MWEZI. Hichi ni kitabu ambacho mimi nitakichagua na kukichambua kwa kina kwenye darasa la jumapili ya mwisho wa mwezi. Taarifa za kitabu ninazitoa mapema ili anayependa kukisoma afanye hivyo na tuweze kuwa na mjadala wa kina kuhusu kitabu husika. Uchambuzi huu utakuwa wa tofauti kabisa, kwani unakuwa wa mtindo wa mjadala na kila mtu anaondoka na mambo ya kwenda kufanyia kazi.

RATIBA ZA SEMINA ZA MWAKA WA MAFANIKIO 2017/2018.

Mwaka wa mafanikio 2017/2018 tutakuwa na semina tatu, mbili kwa njia ya mtandao na moja ya kukutana pamoja.

Semina za mtandao zitaendeshwa kwa njia ya wasap.

Semina ya kwanza itakuwa mwanzoni mwa mwezi januari 2018, kuanzia tarehe 08/01/2018 mpaka tarehe 14/01/2018. Semina itahusu mafanikio na falsafa ya maisha ya mafanikio. Hapa tutapata maneno matatu ya mwaka 2018.

Semina ya pili itakuwa mwanzoni mwa mwezi julai 2018, kuanzia tarehe 02/07/2018 mpaka tarehe 08/07/2018. Semina hii itahusu biashara, fedha na uwekezaji.

Semina ya kukutana ana kwa ana itakuwa mwishoni mwa mwezi oktoba 2018, itafanyika jumamosi ya tarehe 27/10/2018. Eneo la kufanyika semina hii litatangazwa baadaye.

Semina zote hizi ni kwa ajili ya wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA ambao ada zao zipo hai. Hivyo kuhakikisha hukosi semina hizi na mafunzo mengine, hakikisha unalipa ada yako kwa wakati.

Kwa wale ambao siyo wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ili kuweza kunufaika na mafunzo yote muhimu.

Ada ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ni tsh 50,000/= kwa mwaka, ambapo unapata mafunzo yote na semina mbili za njia ya mtandao, bila kuongeza gharama ya ziada. Ila kwa semina ya kukutana ana kwa ana, kutakuwa na ada ya tofauti kulingana na gharama za uendeshaji wa semina hiyo.

Kulipa ada ya KISIMA CHA MAARIFA, tuma fedha tsh 50,000/= kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253. Ukishatuma fedha unayuma ujumbe wenye majina yako kamili kwa njia ya wasap namba 0717396253 kisha unaunganishwa.

Karibu sana kwenye mwaka wa mafanikio 2017/2018, tusafiri pamoja, tukijifunza, kuhamasika na kuchukua hatua.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.kisimachamaarifa.co.tz

KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO