Ipo namna ambayo kila mtu anaiangalia au anaiona dunia kwa jicho lake. Kuna ambao wanaiona dunia ni nzuri na kuna wanayoiona dunia ni mbaya.

Utofauti upo kati ya mtu na mtu kwa jinsi kila mmoja anavyoitazama dunia. Mimi na wewe kila mtu ana mtazamo wake kwa jinsi anavyoiangalia dunia.

Kutokona na namna hizi za kuiangalia duia kwa namna tofauti, namna hizi pia ndio hupelekea maisha kuwa ya tofauti miongoni mwetu.

Lisha Akili

Kwa mfano, wapo watu wanaiangalia dunia katika jicho la woga , hofu na msongo wa mawazo. Kama unaiagalia dunia hivi mambo mengi sana yatakupita.

Mambo ambayo yatakupita itakuwa ni pamoja na taarifa na fursa muhimu kwako. Itakuwa hivyo kwako kwa sababu ndani yako umejaza wasiwasi na ndicho unachoona.

Unapokuwa ndani mwako umejijaza hofu, woga na pia msongo wa mawazo, hata kije kitu kizuri mbele yako huwezi kukiona zaidi utaona mambo hayo.

Hiyo ni sawa na tuchukulie unaendesha gari lako unaenda mjini kutafuta labda duka la maua, lakini ghafla ukatekwa ukiwa kwenye gari na kuwekewa bastola kichwani.

Unafikiri kwa kutekwa huko akili yako itakuwa ina waza nini? Unafikiri hilo duka la maua ulilokuwa ukilitafuta utaweza kuliona?

Naamini hutaweza kuliona, unajua ni kwa nini? Ni kwa sababu akili yako yote itakuwa ipo kwenye bastola, unawaza sijui nitakufa au itakuwaje.

Na maisha yetu kwa ujumla ndivyo yalivyo kwa mfumo kama huo. Ili uweze kufanikiwa hutakiwi kuwa na wasiwasi na mambo mengi.

Unapojenga wasiwasi mkubwa, hakuna fursa au chochote utakachoweza kukiona kwenye maisha yako.

Ndiyo maana maisha yako yanatakiwa kujengwa kwenye ujasiri sana, badala ya kujengwa kwenye hofu zisizo na maana ambazo zinakupoteza.

Unatakiwa kuweka makini kwenye mambo ambayo yanasaidia kukujenga na sio kukubomoa au kukupoteza.

Hapa ndipo unatakiwa ujue msingi wa mafanikio yako unatakiwa uweke wapi, jibu unalo unatakiwa uweke kwenye mambo yatakayokupa ujasiri.

Mambo yote yanayokupa hofu, woga na msongo unapaswwa kuachana nayo mara moja, maana yatakufanya upitwe karibu na kila aina fursa.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea www.amkamtanzania.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,

Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,

Tovuti; www.amkamtanzania.com

Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com