Habari za leo rafiki yangu?

Tupo mwishoni kabisa mwa mwaka 2017, mwaka ambao wakati unaanza watu wengi waliweka malengo mengi na makubwa. Hivi ndivyo watu huwa wanafanya kila mwanzo wa mwaka, wanajiwekea malengo makubwa kwa mwaka husika.

Lakini habari kubwa ya kusikitisha ni kwamba, watu wengi wamekuwa wanaweka malengo yale yale kila mwaka kwa zaidi ya miaka kumi, na mbaya zaidi katika kipindi chote hicho hawayafikii malengo hayo.

Wengi huweka malengo siku za mwanzo za mwaka, lakini kadiri muda unavyokwenda wanayasahau malengo yao na kujikuta wanarudi kwenye maisha waliyozoea kuishi.

Zipo sababu nyingi sana zinazopelekea watu kushindwa kufikia malengo waliyojiwekea wenyewe, na nyingi nitaendelea kukushirikisha kwenye makala mbalimbali ninazokuandalia.

Lakini leo nataka tuiangalie sababu kubwa sana inayowaangusha wengi wanapoweka malengo. Ukiweza kuitatua sababu hii moja, una uhakika wa kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako na kufikia mafanikio makubwa.

Sababu kubwa kabisa ambayo inawazuia watu kufikia malengo wanayojiwekea ni kutaka mabadiliko ya nje lakini siyo mabadiliko ya ndani. Watu wengi wamekuwa wanaweka malengo yanayohusisha vitu vya nje. Utawasikia wakisema nataka kupata hichi, nataka kufika pale na kadhalika. Lakini ni mara chache sana utawasikia watu wakisema mwaka huu nabadili tabia hii, au nataka kuwa hivi. Na hata wale wanaosema wanataka kubadili tabia, bado huwa wanapanga kwa nje.

Kama unataka kupiga hatua yoyote kubwa kwenye maisha yako, lazima hatua kubwa uanze kwako binafsi. Kazi kubwa sana ya mafanikio yako inaanzia kwako, inaanza na wewe binafsi. Haijalishi umeweka malengo makubwa kiasi gani, kama hutaanza kujifanyia kazi wewe mwenyewe, hutaweza kupiga hatua unayotarajia kupiga.

Hivyo ambacho nimekuwa nawashauri marafiki zangu wote, ni kupunguza nguvu kwenye kuweka malengo ya nje na kuweka nguvu kubwa kwenye kutengeneza mfumo wa maisha ambao utawawezesha kufika pale wanapotaka kufika.

Iko hivi rafiki, kama utatengeneza mfumo bora wa maisha, unaokuwezesha kupiga hatua fulani kila siku bila ya kuacha hata siku moja, mfumo huo utakuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako. Hata kama hutakazana na malengo, lakini kama utakuwa na kitu unachofanya kila siku, utapiga hatua kubwa.

Nikupe mifano miwili;

Mfano wa kwanza ni kuwa na afya bora. Unaweza kuwa na mipango mikubwa ya namna gani utakuwa na afya bora, jinsi gani utapunguza uzito, lakini ukashindwa kufikia malengo hayo. Lakini kama ukitengeneza mfumo wa maisha ambao unahusisha ulaji wa kiasi na chakula sahihi, na kila siku kufanya mazoezi, na ukaishi hivyo kila siku baada ya muda utajikuta ukiwa na afya bora.

Mfano wa pili ni uandishi. Unaweza kupanga nataka kuandika kitabu, halafu ukawa unaahirisha tu usipate muda na hamasa nzuri ya kuandika kitabu hicho. Lakini ukitengeneza mfumo unaokuwezesha wewe kuandika kila siku, mfano kuandika maneno 500 kila siku, ndani ya mwezi utaandika maneno elfu 15, miezi miwili maneno elfu 30, ambacho ni kitabu cha kutosha kabisa.

Hivyo rafiki yangu, ambacho nimekuwa nawashauri marafiki zangu, ni kutengeneza mfumo wa maisha, unaokuwa na hatua za kuchukua kila siku, KILA SIKU, ambazo kwa kurudia hivyo kila siku zinatengeneza maisha ambayo ni bora kabisa.

Karibu kwenye semina ya kuanza mwaka 2018.

Rafiki yangu,

Nimekuandalia semina ya kuanza mwaka 2018, semina itakayokuwezesha kubadilika wewe na kutengeneza mfumo wa maisha utakaokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Kwa kushiriki semina hii, utauanza mwaka 2018 ukiwa na ramani ya maisha yako kwa mwaka huo na utaacha kukimbizana na malengo ambayo huyafikii.

Ili kushiriki semina hii unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Na ili kuwa mwanachama unapaswa kulipa ada ya KISIMA CHA MAARIFA ambayo ni tsh 50,000/= (elfu 50) hii ni ada ya mwaka mzima, yaani miezi 12 tangu unapolipa ada hiyo.

Ukiwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA, kila siku kwa mwaka mzima unaendelea kujifunza na kupata hamasa ya kuchukua hatua na kufanikiwa zaidi. Unasoma makala kila siku na pia unapata madarasa yanayokupa mbinu za mafanikio na hamasa ya kupiga hatua zaidi.

Malipo yanafanyika kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253. Ukishafanya malipo tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo na utaunganishwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA.

Karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, tujifunze na kwenda pamoja kwenye safari hii ya mafanikio.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO