Habari rafiki yangu?

Kama nilivyokuambia kwenye email niliyokutumia jana, kesho nakwenda kuanza likizo yangu ya wiki moja, likizo ambayo ni mahususi kwa ajili ya kujipanga vyema kwa mwaka 2018.

Katika likizo hii mambo makubwa ninayokuwa nafanya ni kujifunza kwa kusoma vitabu kwa kina, kutafakari na kutahajudi na kuweka mipango ya kuboresha zaidi shughuli ninazofanya kwa mwaka 2018.

Jana nilichukua muda na kupanga vitabu ambavyo nitakwenda kusoma wakati huu wa likizo ya siku saba, inayoanza tarehe 21/12/2017 mpaka tarehe 27/12/2017. Nimepitia vitabu vingi ambavyo ninavyo, nilivyosoma na ambavyo sijavisoma bado na nimepata msukumo mkubwa wa kurudia baadhi ya vitabu ambavyo nilishasoma, vingine miaka kadhaa iliyopita.

Na hii hapa ndiyo orodha ya vitabu saba ninavyokwenda kusoma kwa kina kwenye siku saba za likizo yangu ya mwaka 2017.

 1. HOW TO LEAD cha JO OWEN.
 2. MINDFUL WORK cha DAVID GELLES
 3. THE ONE MINUTE MILLIONAIRE cha MARK VICTOR HANSEN na ROBERT ALLEN.
 4. WHY WE WANT YOU TO BE RICH cha DONALD TRUMP na ROBERT KIYOSAKI.
 5. UNIVERSITY OF SUCCESS cha OG MANDINO
 6. BILLIONAIRE IN TRAINING cha BRADLEY SUGARS
 7. THINK LIKE A BILLIONAIRE, BECOME A BILLIONAIRE cha SCOT ANDERSON.

vitabu likizo 2017

Kama unavyoona hii orodha rafiki yangu, inagusa maeneo muhimu ambayo nimekuwa nayafanyia kazi kwenye maisha yangu na kukushirikisha uyafanyie kazi pia. Kuanzia uongozi ambacho ni kitu muhimu sana kwa kila mmoja wetu, mafanikio kwa ujumla na fedha ambapo ndipo muhimu zaidi kutokana na changamoto nyingi za kifedha ambazo zinatokana na kukosa maarifa sahihi.

Ni matumaini yangu kwamba siku hizi saba nitakwenda kutengeneza mkakati bora ambao utakuwa na manufaa kwangu na kwako kwa mwaka ujao 2018.

Kama nilivyokuambia rafiki, kuanzia kesho mpaka tarehe 27 nitakuwa sipatikani kabisa. Hivyo nikutakie wakati mwema kwenye siku hizi saba zinazokuja.

ZAWADI YA VITABU KWAKO KUSOMA KWENYE KIPINDI HICHI.

Katika siku hizi saba ambazo nitakuwa likizo, nikijiweka vizuri kwa ajili ya kukupa huduma bora zaidi kwa mwaka 2018 napenda nikupe zawadi ambayo utakuwa unanufaika nayo kwa siku hizi sana.

Hivyo nakwenda kukupa zawadi ya vitabu vyote ambavyo nimeandika (vitabu nane mpaka sasa) ili uweze kujisomea na ujipange kuanza mwaka 2018 ukiwa mtu wa tofauti na wa kipekee kabisa.

Nakupa zawadi ya kupata vitabu vyote nane kwa mfumo wa softcopy kwa kulipia shilingi elfu 30 pekee (30,000). Hii siyo bei ya vitabu hivi, wala hata haifiki nusu ya bei ya vitabu vyote kwa jumla. Ni zawadi tu ambayo naitoa kwako rafiki yangu, kwa sababu nataka uwe na kitu cha kujifunza kwa siku saba zijazo.

Orodha ya vitabu softcopies;

 1. KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI; Sababu 25 kwa nini unaendelea kuwa masikini. Bei ya hichi ni tsh elfu 5.
 2. JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA; Maandalizi na njia bora ya kunufaika na mabadiliko kwenye maisha, kazi na biashara. Bei yake tsh elfu 5.
 3. JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, Jiajiri na utajirike kupitia mtandao wa intaneti. Bei yake elfu 10.
 4. KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, TOLEO LA KWANZA 2016; Nidhamu, Uadilifu Na Kujituma. Bei yake ni tsh elfu 10.
 5. BIASHARA NDANI YA AJIRA; Anzisha na kuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa. Bei yake tsh elfu 10.
 6. MIMI NI MSHINDI; Ahadi yangu na nafsi yangu. Bei tsh elfu 10.
 7. PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU; dhibiti muda wako ili uweze kufanya zaidi. Bei yake tsh elfu 5.
 8. IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING); Miliki biashara kubwa kwa kuanza na mtaji kidogo. Bei tsh elfu 5.

Kupata zawadi hii, tuma fedha tsh 30,000/= kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253 (majina AMANI MAKIRITA) kisha nitumie ujumbe kwenye moja ya namba hizo wenye maneno zawadi ya vitabu ukiwa umeambatanisha na email yako kisha nitakutumia vitabu hivyo nane kwenye email yako.

MUHIMU; Kesho naanza likizo yangu, hivyo sitapatikana, zawadi hii ya vitabu ni kwa leo tu. Hivyo tuma fedha sasa upate vitabu hivyo nane. Siku ya leo ikiisha hutaweza tena kupata zawadi hii, hivyo kama umechelewa kupata ujumbe huu, yaani kama umeupata zaidi ya tarehe 20/12/2017 basi zawadi hii umeshaikosa.

Kama umeupata ujumbe kwa wakati, yaani leo tarehe 20/12/2017 basi chukua hatua sasa ujipatie vitabu hivi nane vitakavyokuwezesha kuanza mwaka 2018 ukiwa mtu tofauti kabisa.

Asante sana rafiki yangu kwa kuwa pamoja kwa kipindi chote hichi, na karibu sana tuendelee kuwa pamoja, tukijifunza na kuhamasika ili kuweza kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yetu.

Usisahau zawadi ya vitabu inayopatikana leo tu. Chukua hatua ili usivikose.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog