Kwa kawaida lipo jambo moja tu kwenye maisha yako ambalo ukilikosa basi naweza kusema utakuwa umejiweka kwenye hatari kubwa sana ya kutokufanikiwa.

Huhitaji kushangaa sana, huo ndio ukweli na uhalisia wake, ikiwa utakosa jambo hilo kuyafikia  mafanikio yako itakuwa ni ngumu sana.

Jambo hili si lingine bali ni uaminifu. Naomba uniambie ni mafanikio gani au biashara gani katika dunia hii ambayo utaifanya bila uaminifu?

Ukiangalia vizuri utagundua msingi mkubwa wa maisha ya mafanikio umejikita sana katika uaminifu na si vinginevyo.

Kuaminiwa au uaminifu huo tunaouzungumzia hapa, pia huwa hauji kwa bahati mbaya, kuna namna unayoweza kufanya ili kujenga uaminifu huo.

vitabu softcopyUnatakiwa kuelewa uaminiwa kwa jambo lolote lile, kunatokana na ukweli. Hata kama ukweli huo unauma sana, lakini chanzo cha kuaminiwa ndiko kinapoanzia huko.

Hautaweza kuaminiwa na mtu yeyote kama ndani yako huna alama za ukweli ambazo zinaonekana, zaidi utazidi kuonekana ni wa kawaida.

Kama nilivyosema na bila kuaminiwa pia, hakuna kitu ambacho utaweza kukifanikisha sana. Hiyo yote ni kwa sababu mafanikio mara nyingi yanaanza kujengwa na kuaminiwa.

Ukiweza kuaminiwa hata ukiwa huna mtaji unaweza ukafanya biashara, lakini kosa kubwa linakuja hasa pale unaposhindwa kwa mwaminifu, hakuna atayekuhitaji.

Kwa hiyo unaona uamifu pekee ni kama mtaji, lakini uaminifu hauanzi hivi hivi tu, lazima kwanza ukweli ndani yako uwepo.

Ili uweze kuaminika unatakiwa uelewe hata unapofanya kazi na wengine unatakiwa uwe mkweli sana kutoka kwenye kauli zako na mengineyo mengi.

Bila uaminifu kuwepo kwenye maisha ya kawaida basi mambo mengi ni yatakwama sana. na zipo huduma zitakufa kabisa.

Unaona mpaka hapo unatakiwa kujenga uaminifu mkubwa sana kwenye kila ukifanyacho ili kikupe mfanikio, lakini sehemu ya kuanzia ni kwenye ukweli.

Je, wewe ni mkweli kiasi gani na kwa akina nani, hapo ndipo nguzo ya kuaminiwa inapoanzia na watu wengi wakakubali.

Hakuna mtu ambaye yupo duniani hapa anaaminiwa lakini asiwe mkweli, ukweli ni kitu ambacho kinasaidia sana kujenga uaminifu.

Hivyo  unaona bila ukweli hakuna uaminifu wowote. Hiyo inadhihirisha kabisa bila mambo haya mawili hakuna mafanikio ya kweli.

Mafanikio ya kweli na kwa wengine yanaanza kwa wewe kuwa mwaminifu na pia uaminifu huo utakusaidia tu kuweza kupata kile unachokitaka.

Unachotakiwa kufanya hapa, ni kuamua kutengeneza uaminifu wako kwa kuama kuwa mkweli kwa kila unachokifanya.

Kwa kujenga uaminifu, ndivyo utajikuta ukizidi kuyafikia mafanikio yako kila kukicha. Anza leo kuwa mwaminifu na utafika mbali sana kimafanikio.

Unatakiwa kuweka akilini mwako kwamba, kama utakosa jambo hili yaani ukakosa uaminifu utahangaika sana kuyatafuta mafanikio na hutaweza kuyapata.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kila siku kujifunza maisha na mafanikio.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,

Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,

Tovuti; www.amkamtanzania.com

Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com