Habari za leo rafiki yangu?

Hongera sana kwa nafasi hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni siku nyingine bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wetu wa maisha ya mafanikio, ambao ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA, tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Rafiki, mwaka 2016 nilitoa toleo la kwanza la kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA. Hichi ni kitabu ambacho nililenga kuwapa watu maarifa sahihi ya kuweza kuanza na kukuza biashara zao hata kama wanaona hawana muda kabisa.

BIASHARA NDANI YA AJIRA SOFT

Niliandika kitabu hichi baada ya kuona watu wengi wakiwa wamenasa kwenye ajira, ambazo haziwatoshelezi kwa upande wa kipato, lakini pia hawawezi kuziacha kwa sababu ndiyo wanazitegemea kuendesha maisha yao ya kila siku.

Hivyo wengi wanakuwa wanafikiria hawawezi kuanza biashara kwa sababu ajira zao zinawabana. Na wakati huo huo hawawezi kuacha ajira zao na kwenda kuanza biashara kwa sababu ajira hizo ndiyo wanazitegemea kwa asilimia 100. Unaona jinsi hali ilivyo ngumu hapo?
kwenye toleo la kwanza la kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA, nimeonesha ni namna gani mtu anaweza kuanza biashara akiwa bado yupo kwenye ajira yake. Na tena nimefundisha kwa nini ni muhimu mtu kuanza biashara akiwa bado ameajiriwa.

Kwenye kitabu hichi nimegusia mambo muhimu sana yanayohusu biashara, kuanzia wazo la biashara, kupata mtaji, kusimamia biashara na pia njia mbalimbali za kuingiza kipato, yaani mifereji mbalimbali ya kuingiza kipato.

Sasa rafiki, vitabu nilivyochapa kwenye toleo la kwanza vinaelekea kuisha kabisa. Nichukue nafasi hii kuwashukuru sana marafiki zangu wote na wasomaji ambao mmenunua kitabu hichi na kujifunza mengi kupitia kitabu hichi.

Sasa najiandaa kuchapa vitabu vingine, lakini sitachapa kama kilivyokuwa, bali naandaa toleo la pili la kitabu hichi cha BIASHARA NDANI YA AJIRA.

Na hapa ndipo ninapohitaji sana msaada wako kama rafiki yangu na msomaji wa kazi zangu.

Kama umekisoma kitabu cha biashara ndani ya ajira, iwe ni nakala tete (softcopy) au nakala ngumu (hardcopy) ninahitaji sana msaada wako katika maandalizi ya toleo la pili.

Msaada ninaohitaji kwako ni mrejesho kutoka kwenye toleo la kwanza la kitabu hichi cha BIASHARA NDANI YA AJIRA.

Kama umesoma kitabu hichi, tafadhali chukua dakika chache kujibu maswali ambayo ni mafupi sana kuhusiana na kuanzisha biashara ukiwa ndani ya ajira.

Hata kama huna biashara, au haupo kwenye ajira ila unafanya au unataka kufanya biashara, nahitaji maoni yako ili kitabu kinachotoka kiweze kuwa msaada kwa wengi.

Nimeandaa fomu ya kukusanya maoni haya, ambayo ni rahisi kujaza, hivyo naomba sana unisaidie kwenye hili. Kadiri ninapopata maoni yako mapema, ndivyo nitakavyoweza kuyatumia kwenye maandalizi ya toleo la pili la kitabu hichi cha BIASHARA NDANI YA AJIRA.

Kutuma maoni na mrejesho wako tafadhali bonyeza maneno haya, itafunguka fomu ambayo itakuwa na maswali utakayojibu.

Nichukue nafasi hii kukushukuru sana wewe rafiki na msomaji wangu, ni kwa sababu yako ndiyo naendelea kuandika makala mbalimbali kila siku na hata vitabu.

Ni imani yangu kwamba utachukua hatua ya kunisaidia, ili niweze kukusaidia zaidi. Ninahitaji sana maoni yako kuhusu kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA, toleo la pili ninalofanyia maandalizi.

Nakuomba tena rafiki, bonyeza maandishi haya na jaza fomu kisha tuma maoni yako ili niweze kuyafanyia kazi.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog