Kwa muda sasa nimekuwa nikafatilia kwa ukaribu tabia ambazo watu wengi ambao wana mafaniko wanazo. Kuanzia waandishi nguli wa vitabu na hata wawekezaji wakubwa wote kwa pamoja nimekuwa nikafatilia tabia zao, kujua ni kipi wakifanyacho.

Kitu ambacho nimekuwa nikigundua sana ni kwamba watu hao wana tabia karibu zinazofanana za kimafanikio. Na tabia hizi ndizo ambazo huwaweka juu kimafanikio na kwa kuwa wewe huna tabia hizo au huzijui unabaki pale ulipo.

Kwa sehemu tumewahi kuelezea tabia za kimafaniko kupitia mtandao huu wa AMKA MTANZANIA ambazo unatakiwa kuwa nazo. Kwa msisitizo na umuhimu wa somo hili, leo kupitia makala haya nakukumbusha tabia hizi za msingi unazotakiwa kuwa nazo.

vitabu softcopy

Pasipo wewe kuwa na tabia hizi ambazo naweza kusema ndio msingi wa maendeleo yako makubwa huwezi kufika popote. Utaweka juhudi sana lakini mwisho wa siku juhudi zako zitakuwa ni sawa na kusema ni kazi bure tu, hakuna utakachoweza kukipata.

Zifuatazo Ni Tabia Unazotakiwa Kuzijenga Wakati Wote, Ili Zikupe  Mafanikio Ya Kudumu:-

Tabia ya kujifunza kila siku.

Watu wenye mafanikio ni watu ambao wana tabia ya kujifunza kila siku. Hutumia muda wao kujifunza sana kupitia vitabu. Ukifatilia unaona wanaofanikiwa sana wanajifunza, hivyo hii ni tabia ambayo hata wewe unatakiwa kujijengea ili ikusaidie kukuwezesha kufanikiwa.

Kama si mtu wa kusoma vitabu unaweza ukaanza kusoma kitabu angalau nusu saa kwa siku, ambapo baada ya muda utazoea na utakuwa unasoma kwa muda mrefu. Unapokuwa unajifunza hiyo inakupa maarifa yatakayokusadia kujenga mafaniko ya kudumu kwako.

Tabia ya kujenga Mahusiano sahihi na watu wengine.

Watu wenye mafanikio hawaishii tu kwenye kujifunza bali ni watu ambao wana tabia ya kujenga mahusiano sahihi na watu wengine. Kila wakati hutafuta watu sahihi ambao wataenda pamoja katika safari ya mafanikio.

Ni ukweli uliowazi unapokuwa na watu sahihi, si rahisi sana wao kuweza kukuangusha. Hivi ndivyo watu wenye mafanikio wanavyojenga mafanikio yao kwa kiasi kikubwa. Kwa sababu hiii hata wewe ukifata tabia hii ni lazima itakupa mafanikio ya kudumu.

Tabia ya kujaribu mambo mapya.

Watu wenye mafanikio wana tabia ya kujaribu mambo mapya kila wakati. Si watu wa kufanya mambo kwa njia na mtindo uleule kwa wakati wote. Mara nyingi hujaribu kupima njia nyingine ambayo inaweza ikaleta matokeo tofauti.

Tabia hii ndio huwafanya kufikia mafanikio makubwa. Katika kujaribu hiki au kile mwisho wa siku hujikuta wamefanikiwa sana. Hata wewe hukatazwi kujaribu mambo mapya kwani kwa kujaribu huko hukusogeza kwenye mafanikio yako.

Tabia ya kuweka malengo na kuyafanikisha.

Kuweka malengo si kazi, bali kazi huanza katika kuyafikia malengo hayo. Watu wengi wanaweka malengo sana, lakini inapofika wakati wa kuyafanikisha hapo ndio changamoto kubwa huanza kujitokeza na kushindwa kuyafanikisha.

Utakuta watu hawa wana sababu nyingi sana. Ikiwa lakini unataka kufanikiwa na kujenga mafanikio ya kudumu, inabidi ujue jinsi ya kujenga tabia ya kuweka malengo na kuweza kuyafikia. Hii ni tabia ambayo itakupa mafanikio maishani mwako.

Tabia ya kujitoa mhanga.

Kujaribu kufanikiwa huku ukiwa hutaki kuingia katika hali hatarishi wakati mwingine naweza kusema ni sawa na kujidanganya. Unatakiwa ufike mahali ujkajenga tabia ya kujitoa mhanga pasipo kuogopa kitu chochote.

Watu wenye mafanikio wanajitoa sana mhanga katika kuhakikisha ndoto zao zinatimia. Ni watu ambao hawaogopi kitu chochote hufanya kila linalowezekana na hadi kufanya ndoto zao zinaweza kutumia kwenye maisha yao.

Ukifanikiwakujena tabia hizo, utakuwa na wakti bora wa kujenga mafaniio ya kudumumaishani mwako.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kila siku kujifunza maisha na mafanikio.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,

Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,

Tovuti; http//www.amkamtanzania.com,

Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com