Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KESHO YA JANA NI LEO…
Hakuna maneno rahisi kujiambia kama NITAFANYA KESHO.
Huwa tunajiambia maneno haya tukifikiri kesho ni mbali sana na kuna utofauti mkubwa utakaokuwepo kwenye hiyo kesho ukilinganisha na siku husika.

Lakini kesho huwa haifiki,
Kwa sababu kama tunavyofikiri kesho iko mbali, basi inakuwa mbali kweli.
Maana hata ile kesho inapofika, tunajiambia tena tutafanya kesho.
Siku zinaenda na inafika siku tunastuka muda umeenda sana na hakuna makubwa tuliyofanya.

Rafiki, leo kaa chini na utafakari hili, kesho ya jana ni leo.
Kila unapojiambia utafanya kesho, basi jikumbushe kwamba kesho ya jana ni leo.
Jikumbushe hili kwa kuelewa kwamba unavyofikiri kwamba kesho ni mbali, wala siyo mbali sana, ni karibu mno.

Hivyo kama una jambo lolote muhimu la kufanya, inabidi ulifanye sasa, usisubiri kesho, maana kesho siyo mbali, lakini pia kesho inaweza isifike.
Jipe msimamo wa kufanya jambo sasa, au kutokufanya jambo hilo kabisa.
Lakini usijidanganye lwa kesho.

Kama umebanwa kabisa kabisa, kila dakika una cha kufanya, na namna pekee ni kufanya keshom basi andika ni kida gani kesho utafanya na usipange kingine chochote kwenye muda huo.

Ukawe na siki bora sana ya leo rafiki, siku ya kufanya leo na siyo kusubiri kesho.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha