Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari SIYO MUDA UNAOFANYA, BALI KIASI UNACHOFANYA…
Kwenye eneo la kazi, watu wamekuwa wanajidanganya sana.
Utawasikia watu wanasema nipo bize kweli, nafanya kazi masaa mengi sana kwa siku.
Lakini unapochukua hatua ya kuiangalia siku yake kwa umakini, unagundua muda mwingi hatumii kufanya kazi, bali anautumia kutoroka kazi.

Anatoroka kazi kwa kufanya vitu ambavyo havina matokeo yoyote kwenye kazi yake.
Wakati mwingine anachofanya siyo kazi, bali maandalizi ya kazi.
Na wanaoongoza kwa kujidanganya kwenye kazi ni wale walioajiriwa, ambayo kwenye masaa nane ya siku ya kazi, ukiangalia kwa kina, utagundua masaa hasa aliyofanya jazi hayazidi masaa mawili.

Muda mwingine unakuta ameupotezea kwenye vikao, kujiandaa kwenda kwenye chai, kupata chai, kurudi kwenye chai, kujiandaa kwenda kwenye chakula, kula na kupiga soga na wengine, kurudi kwenye kazi na hatimaye kujiandaa kumaliza kazi.

Mtu anachoka kweli, lakini ukipima alichozalisha, ni kidogo mno.
Rafiki, usipime kazi yako kwa muda uliofanya kazi, bali kwa thamani uliyozalisha, kwa kiasi ulichofanya.

Na nikupe kipimo rahisi kwako kutumia.
Unapokuwa kwenye kazi, kabla hujafanya chochote jiulize je hichi kinaingiza fedha kwenye kazi ninayofanya? Kama jibu ni hapana usikifanye.
Ni hivyo tu, unapopanga muda wako wa kazi, fanya vile vinavyoingiza fedha tu.
Vingine vyote achana navyo, ni usumbufu, ni kutoroka kazi, ni kujidanganya.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kufanya kazi kweli na siyo kutoroka kazi.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha