Rafiki yangu mpendwa,

Inapokuja kwenye swala la maisha bora, ya mafanikio na kuweza kupata chochote ambacho mtu unataka, sehemu ya kuanzia ni moja pekee.

Ukishaijua sehemu hiyo na kuweza kuifanyia kazi, dunia haikupi shida, hakuna chochote kitakachokusumbua na maisha yako yataenda vile unavyotaka wewe, hata kama hujapata kila ulichotaka kupata.

Kama unataka kuitawala dunia nzima, kama unataka dunia isikupe shida kwa chochote kile kinachotokea, basi unahitaji kumtawala mtu mmoja pekee hapa duniani.

Mtu huyo ni wewe mwenyewe, nafsi yako ambayo ndiyo inatengeneza dunia unayoiona wewe.

Chochote unachokiona hapa duniani, vyovyote unavyoichukulia dunia, jua kwamba siyo kwamba ndivyo ilivyo kwa watu wote, bali ndivyo ilivyo kwako wewe binafsi. Hii ina maana kwamba, mtazamo wako binafsi, una mchango mkubwa sana wa jinsi gani unaichukulia dunia na hata namna unavyoitawala au ikakutawala.

MIMI NI MSHINDI

Epictetus, aliyekuwa mwanafalsafa wa ustoa aliandika, siyo kile kinachotokea ndiyo kinakuvuruga, bali namna unavyotafsiri kila kinachotokea. Na hapa alikuwa sahihi sana, kwa sababu vitu vinatokea sawa kwa watu wote, lakini tafsiri zinakuwa tofauti.

Watu wawili wanaweza kushindwa kwenye kitu kimoja, mmoja akachukulia kushindwa huko kama kichocheo cha kufanya zaidi na akafanikiwa. Mwingine anaweza kuchukulia kushindwa huko kama sababu ya kukata tamaa na kushindwa kabisa.

SOMA; Fanya Mambo Haya 18 Pekee Na Mwaka 2018 Utakuwa Wa Mafanikio Makubwa Sana Kwako.

Tukio ni moja, tafsiri tofauti na matokeo tofauti kabisa.

Siyo kinachotokea, bali namna unavyotafsiri kinachotokea ndiyo inaleta madhara kwako.

Kwenye Falsafa ya Ustoa pia kuna dhana inayoitwa upili wa udhibiti. Dhana hii inaeleza kwamba vitu vyote vinavyotokea kwenye maisha yako, vinagawanyika katika makundi mawili, kundi la kwanza ni vitu unavyoweza kuviathiri, hivi vipo ndani ya uwezo wako. Kundi la pili ni vitu usivyoweza kuviathiri, hivi vipo nje ya uwezo wako.

Hivyo unapokutana na chochote na ukajiambia ni kigumu au kinakushinda, huna haja ya kusumbuka, badala yake jiulize je kipo ndani ya uwezo wako au nje ya uwezo wako. Kama kipo ndani ya uwezo wako chukua hatua sahihi, kama kipo nje ya uwezo wako kikubali kama kilivyo au kipuuze. Hakuna namna bora ya kuendesha maisha yako kama hii, kwa sababu hakuna chochote kitakachotokea, ambacho kitakuvuruga kabisa.

Rafiki, nikukumbushe tena ya kwamba kama unataka kuitawala dunia, kuna mtu mmoja unayepaswa kumtawala, na mtu huyo ni wewe mwenyewe. Hutaweza kujitawala wewe mwenyewe kwa mabavu au nguvu, badala yake utajitawala kwa kudhibiti mawazo yako na hisia zako.

Na kama utatumia misingi ya ustoa ambayo nimekushirikisha kwenye makala hii, hakuna chochote ambacho kitaweza kukukwamisha wewe kwenye maisha yako.

KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018.

Rafiki, nakukumbusha kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, ambayo itafanyika jumamosi ya tarehe 03/11/2018 jijini dar es salaam.

Kwenye semina hii tutajifunza na kuhamasika na kuweza kuweka mikakati ya mafanikio makubwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla.

Ada ya kushiriki semina hii ni tsh 100,000/= na mwisho wa kulipa ada hii ni tarehe 31/10/2018.

Malipo ya ada yanafanyika kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253 ukishalipa tuma ujumbe wenye majina yako na namba ya simu kwenye namba 0717396253 na utapewa maelekezo zaidi.

Karibu sana kwenye nafasi hii ya kipekee ya sisi kukutana pamoja kama wanamafanikio na kujifunza pamoja na kuhamasika ili kuweza kufanya makubwa zaidi.

Makala hii imeandikwa na Kocha Dr Makirita Amani.

Dr. Makirita ni Daktari wa binadamu, Kocha wa mafanikio, Mwandishi na Mjasiriamali.

Dr. Makirita anaendesha mafunzo ya mafanikio kwa wale waliojitoa hasa kufanikiwa kupitia program ya KISIMA CHA MAARIFA.

Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma sasa ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa njia ya wasap namba 0717 396 253 (tumia wasap tu)

Kupata huduma nyingine za ukocha tembelea www.amkamtanzania.com/kocha

Kupata vitabu vizuri vya kusoma tembelea www.amkamtanzania.com/vitabu

Usomaji