Rafiki yangu mpendwa,
Mwaka huu nilitoa nafasi ya kipekee kwa wale ambao wangependa tufanye kazi kwa ukaribu zaidi ili kuweza kukuza zaidi biashara zao.
Nafasi hii niliitoa baada ya semina ya UKUAJI WA BIASHARA iliyofanyika kwa njia ya mtandao kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Kwenye semina hiyo tulijifunza mbinu zaidi ya 50 za kuongeza wateja, kuongeza mauzo, kuongeza faida na hatimaye kukuza zaidi biashara yako.
Nafasi nilitoa kwa wale ambao tayari wana biashara ambazo zinakua na zimeshaajiri. Lakini kutokana na kubanwa na muda, sikuweza kuwapa watu wengi nafasi hizo.
Sasa natoa tena nafasi za kuweza kufanya kazi pamoja na wewe kwa kipindi cha mwaka mzima ili kuiwezesha biashara yako kukua zaidi. Nafasi za sasa hazitachagua kwamba uwe na biashara inayokua na ambayo imeshaajiri, badala yake unaweza kupata nafasi hii hata kama ndiyo unapanga kuanza biashara. Muhimu tu ni uwe tayari kufanya biashara na kuwa tayari kujisukuma zaidi ndani ya mwaka mmoja.
Rafiki, kuna nafasi 10 za kufanya kazi pamoja na mimi kuweza kuikuza zaidi biashara yako. Kwa pamoja, kwenye kikundi hichi cha watu 10 tutajifunza na kuhamasika ili kuweza kuchukua hatua kubwa na kukuza zaidi biashara yako.
Itakuwa ni moja ya programu zangu za ukocha, programu ninayoiita LEVEL UP, lakini nitaitoa kwa msisitizo wa hali ya juu. Ninatenga mwaka mzima ambao nitaacha shughuli nyingi ili kuweza kupata muda wa kutosha wa kuwafuatilia kwa ukaribu sana watu hao 10 watakaopata nafasi hizi.
Programu hii itaanza tarehe 05/11/2018 na kwenda mpaka tarehe 31/10/2019.
Ili kupata nafasi ya kushiriki kwenye programu hii ya mwaka mzima, kwanza kabisa unapaswa kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, ambayo itafanyika tarehe 03/11/2018. Maelezo zaidi kuhusu semina yapo hapo chini.

Baada ya kushiriki semina, nitatoa maelezo zaidi kuhusu programu hii na jinsi tutakavyoiendesha. Kwa wale watakaojiunga na programu hii, tutakutana tena kwa pamoja tarehe 04/11/2018 kwa ajili ya kuweka mipango na mikakati ambayo kila mmoja wetu anakwenda kuifanyia kazi kwa mwaka mzima. Pia tutaweka utaratibu ambao utatumika katika kufuatiliana kwa karibu ili hata mmoja asirudi nyuma.
Rafiki, kama umekuwa na ndoto za kuikuza zaidi biashara yako, kuiondoa biashara kwenye utegemezi wako na iweze kujiendesha yenyewe, kama umekuwa unafikiria ni kwa namna gani unaweza kuikuza zaidi biashara yako, basi jibu umelipata sasa. Kwa pamoja, ndani ya mwaka mmoja tutafanya kazi kubwa ya kuiwezesha biashara yako kukua zaidi baada ya wewe kukua zaidi pia.
Rafiki, nafasi ni kumi pekee kwa sababu nitaweka kazi kubwa sana ya kumfuatilia kila mmoja. Pia kila mwezi nitamtembelea mmoja wa walio kwenye programu hiyo na kuiangalia kwa kina biashara yake pamoja na kushauriana vizuri zaidi kwenye eneo la biashara.
Pia kwa wale ambao biashara zao tayari zimeshaajiri, kutakuwa na nafasi ya kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa biashara hiyo, ili kuweza kujenga timu imara zaidi itakayoiwezesha biashara kukua zaidi.
Karibu sana rafiki yangu kwenye programu hii ya LEVEL UP ili uweze kuikuza biashara yako zaidi ya hapo ilipo sasa. Nafasi hii utaipata baada ya kuwa umeshiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018.
KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018.
Rafiki, tarehe 03/11/2018 ndiyo siku ya SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, semina hii itafanyika kwenye moja ya hoteli zilizopo jijini dar es salaam.
Itakuwa ni semina ya siku nzima, kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa moja jioni. Yatakuwa ni masaa 12 ya kujifunza, kujuana na wengine, kuhamasika na kuweka mkakati wa kwenda kufanyia kazi kwa mwaka mzima.
Ada ya kushiriki semina hii ni tshs 100,000/= (laki moja) ada ambayo itajumuisha huduma zote za siku ya semina, kuanzia chai, chakula cha mchana, vitafunwa vya jioni, vijitabu vya kuandikia na kalamu.
Ili kupata nafasi ya kushiriki semina hii, unapaswa kulipa ada yako kabla ya tarehe 31/10/2018, ambayo ndiyo tarehe ya mwisho ya kulipia ada.
Pia nafasi za kushiriki semina hii ni 100 pekee, na zilizobaki ni chache sana. hivyo kama hutaki kukosa nafasi hii, lipa ada yako mapema ili tuweze kuwa pamoja kwenye semina hii.
Nakusubiri kwa hamu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, kwa sababu yapo mengi mazuri nimekuandalia kwa mafanikio yako kwa mwaka 2018/2019.
Namba za kufanya malipo ili kushiriki semina hii ni MPESA- 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY – 0717 396 253. Majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA. Ukituma fedha tuma na ujumbe wa kueleza umefanya malipo ya semina, ukiambatana na jina lako na namba yako ya simu kwa ajili ya kupewa taarifa zaidi za semina.
Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha
Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; http://eepurl.com/dDZHvL