Rafiki yangu mpendwa,

Kama umekuwa mwanachama na mfuatiliaji wa AMKA MTANZANIA hasa kupitia kundi la Telegram, utakuwa umegundua kwamba kwa siku za karibuni hulioni tena kundi lile.

Na wapo ambao wamekuwa wanauliza nini kimetokea mpaka hawapo tena kwenye kundi.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu kwamba kundi lile la AMKA MTANZANIA telegram limefutwa. Hii ni kutokana na kundi lile kuanza kutumika vibaya na baadhi ya watu na hivyo kuhitaji rasilimali nyingi kuliendesha.

Kundi lilikuwa na watu karibu elfu moja, na kujiunga ilikuwa bure kabisa, lengo lake lilikuwa kushirikishana maarifa mbalimbali ya mafanikio. Lakini watu walianza kujiunga na kufanya kuwa sehemu ya kutangaza kila kitu, mpaka vitu visivyokuwa sahihi.

Pia kundi lilipoa sana na watu kuanza kulichukulia kawaida kiasi kwamba ile hamasa ya mwanzo ya kujifunza na kushirikishana haikuwepo tena. Hivyo kundi lilianza kuwa mzigo, likihitaji muda mwingi wa kufuta vitu visivyo sahihi na kuwaondoa wanachama wanaolitumia vibaya.

Baada ya kufanya tathmini ya kina, kundi lilionekana kuwa mzigo kuliko kuwa msaada kwa wengi. Na hivyo nilifikia maamuzi ya kulifuta mara moja.

Kwa sasa kundi pekee ninaloendesha ambalo yeyote anaweza kujifunza maarifa sahihi ya mafanikio ni kundi la KISIMA CHA MAARIFA lililopo kwenye mtandao wa wasap. Hili ni kundi ambalo nimeweka nguvu zangu zote na nataka litoe thamani kubwa zaidi kwa wanachama wote.

Hivyo kwa wale waliokuwa wananufaika na kundi la AMKA MTANZANIA telegram, mnakaribishwa kujiunga na kundi la KISIMA CHA MAARIFA. Maelezo ya kujiunga yapo hapo chini.

cropped-mimi-ni-mshindi

JINSI YA KUPATA MAKALA ZA KILA SIKU MOJA KWA MOJA.

Kwa wale ambao walishazoea kupata makala za kila siku moja kwa moja kupitia mtandao wa telegram, bado ipo njia ya kuendelea kupata makala hizo. Unachopaswa kufanya ni kufungua kiungo hiki; https://t.me/Coachmakiritabot kisha unajiunga ili kupokea makala moja kwa moja. Hii ni kama unatumia mtandao wa telegram.

Kwa wale ambao hawatumii mtandao wa telegram, makala mpya zinawekwa kila siku kwenye mtandao wa www.amkamtanzania.com na www.kisimachamaarifa.co.tz hivyo weka utaratibu kila siku unapoianza siku yako, kupitia kwanza mitandao hiyo na kusoma makala mpya zilizopo, na hata za zamani pia.

Mwisho kabisa, nimeanzisha kipengele kipya cha makala za DAKIKA MOJA, ambapo kila siku asubuhi unapata makala mpya fupi na ya kujifunza moja kwa moja kwenye email yako. Kama bado hujaanza kupata makala hizi fungua kiungo hiki ili kujunga; https://amkamtanzania.com/jiunge/

Karibu sana rafiki yangu tuendelee kuwa pamoja, tujifunze na kuchukua hatua ili kuweza kufikia mafanikio makubwa sana kwenye maisha yetu. Hakuna linaloshindikana unapokuwa na maarifa sahihi na kuwa tayari kuchukua hatua kubwa.

Makala hii imeandikwa na Kocha Dr Makirita Amani.

Dr. Makirita ni Daktari wa binadamu, Kocha wa mafanikio, Mwandishi na Mjasiriamali.

Dr. Makirita anaendesha mafunzo ya mafanikio kwa wale waliojitoa hasa kufanikiwa kupitia program ya KISIMA CHA MAARIFA.

Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma sasa ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa njia ya wasap namba 0717 396 253 (tumia wasap tu)

Kupata huduma nyingine za ukocha tembelea www.amkamtanzania.com/kocha

Kupata vitabu vizuri vya kusoma tembelea www.amkamtanzania.com/vitabu