Rafiki yangu mpendwa,

Maarifa yote mazuri ambayo yanaweza kukutoa hapo ulipo sasa na kukufikisha kule unakotaka kufika yapo kwenye vitabu.

Majibu ya changamoto zote unazopitia sasa, ambazo zinakukwamisha sana, yapo kwenye vitabu.

Na kitu kipekee kinachokuzuia wewe usiwe na yale maisha unayotaka kuwa nayo, ni maarifa ambayo umeyakosa.

Mwandishi Charlie Tremendous Jones amewahi kunukuliwa akisema; tofauti yako ya leo na miaka mitano ijayo itakuwa vitabu ulivyosoma na watu uliokutana nao. Sasa watu wengi wamekuwa hawana tofauti kubwa kwenye maisha yao kwa sababu hawakutani na watu wapya wengi lakini pia hawasomi vitabu.

Naye Mark Twain amewahi kunukuliwa akisema; kama mtu anajua kusoma lakini hasomi vitabu, basi hana tofauti na mtu asiyejua kusoma.

Rafiki, yote haya ni kuonesha ni jinsi gani ilivyo muhimu kwa mtu yeyote ambaye yupo makini na maisha yake kusoma vitabu.

Watu wamekuwa na sababu nyingi kwa nini hawasomi vitabu, wapo wanaosema vitabu vingi vizuri vipo kwa lugha ya kiingereza ambayo hawaielewi. Wapo wanaosema hawana muda wa kusoma vitabu, wapo wanaosema hawawezi kumudu kununua vitabu vingi.

Leo nakwenda kukuonesha jinsi ambavyo unaweza kusoma vitabu 50 kabla mwaka huu 2019 haujaisha, na ukaweza kupata maarifa bora na yatakayokusukuma sana kwenye safari yako ya mafanikio.

Kwenye kitabu kipya nilichotoa, kinachoitwa TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA, nimechambua vitabu 50 bora kabisa vya mafanikio kwa lugha rahisi kwako kuelewa na kukupa hatua za kuchukua kwenye kila kitabu.

KITABU; TANO ZA MAJUMA YA MWAKA

Hivyo kama utapata na kusoma kitabu hiki, utaondokana na changamoto ya lugha, kwa sababu kitabu ni cha kiswahili, utaondokana na changamoto ya muda, kwa sababu unahitaji dakika 10 tu kwa siku za kusoma na pia utaondokana na changamoto kwamba huna fedha ya kununua vitabu vingi, kwa sababu uchambuzi wa vitabu vyote upo kwenye kitabu hicho kimoja.

Hivyo ukiweza kujipatia kitabu cha TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA utaweza kusoma uchambuzi wa vitabu bora 50, utajifunza siri 50 za mafanikio na mafunzo mengine mazuri kama ya kifedha na hata kupata tafakari zinazoadili kabisa mtazamo wako.

Vifuatavyo ni vitabu 50 vilivyochambuliwa kwenye kitabu cha TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA. Soma orodha hiyo na kile kikubwa cha kujifunza, kisha mwisho kabisa nitakupa njia ya kupata vitabu vyote 50 bure kabisa.

Orodha hii nimeiweka kwa mtiririko wa majuma ambayo kitabu husika kimechambuliwa.

Juma #1; Born to Win: Find Your Success Code by Tom Ziglar and Zig Ziglar. Umezaliwa kushinda, lakini ili uweze kushinda unahitaji kwanza upange kushinda, ujiandae kushinda kisha ndiyo utegemee kushinda.

Juma #2; Secrets of the richest man who ever lived by Mike Murdock. Mfalme Selemani ni mmoja wa watu matajiri sana kuwahi kuwepo hapa duniani. Selemani alikuwa na siri 31 zilizomfikisha kwenye mafanikio makubwa na siri kuu ilikuwa kupenda hekima.

Juma #3; The Small Business Bible: Everything You Need to Know to Succeed in Your Small Business by Steven Strauss. Uchumi wa dunia unategemea sana kwenye biashara ndogo na njia ya uhakika ya kuwatoa watu kwenye umasikini ni kuingia kwenye biashara ndogo. Lakini ili kufanikiwa kwenye biashara ndogo, unahitaji maarifa sahihi ya kuanzisha na kukuza biashara yako.

Juma #4; Be Obsessed or Be Average by Grant Cardone. Kwenye maisha unaweza kuchagua kufanikiwa au kuchagua kuwa kawaida. Kama umechagua kufanikiwa, basi unapaswa kupenda sana kile unachofanya.

Juma #5; The Longevity Project: Surprising Discoveries for Health and Long Life from the Landmark Eight-Decade Study by Howard S. Friedman, Leslie R. Martin. Kuna watu ambao wanaishi maisha marefu kuliko wengine, watu hawa wanaijua siri kuu moja, kujipenda wenyewe, kupenda wengine, kupenda maisha na kupenda wanachofanya.

Juma #6; The Craving Mind: From Cigarettes to Smartphones to Love – Why We Get Hooked and How We Can Break Bad Habits by Judson Brewer. Usipoweza kuidhibiti akili yako, itakufanya wewe uwe mtumwa wa tabia zisizo na manufaa kwako.

Juma #7; The Total Money Makeover: A Proven Plan for Financial Fitness by Dave Ramsey. Kanuni ya kuelekea kwenye utajiri na uhuru wa kifedha ni kuondoka kwenye madeni, kuweka akiba na kuwekeza.

Juma #8; Evolutionary Enlightenment: A New Path to Spiritual Awakening by Andrew Cohen. Dini ni kikwazo kwenye ukuaji wa kiroho, wengi wanashikilia dini kuliko kukazana kukua kiroho na kiimani.

Juma #9; Predictably Irrational: The Hidden Forces That Shape Our Decisions

by Dan Ariely. Hisia zetu huwa zinaathiri maamuzi yetu, ukitaka kufanya maamuzi sahihi, fanya wakati ukiwa huna hisia kali.

Juma #10; Harmonic Wealth: The Secret of Attracting the Life You Want by James Arthur Ray,

Linda Sivertsen. Mafanikio na utajiri wa kweli, ni pale maeneo matano ya maisha yako yanapokwenda sawa,maeneo hayo ni FEDHA, MAHUSIANO, AKILI, MWILI NA ROHO/IMANI. Mafanikio yoyote ambayo hayahusishi maeneo hayo matano hayawezi kuwa mafanikio ya kweli na yatakayodumu.

Juma #11; Primary Greatness: The 12 Levers of Success by Stephen R. Covey. Msingi mkuu wa mafanikio ni kuiishi misingi ya mafanikio, huwezi kufanikiwa kama huijui misingi ya mafanikio na kuifuata. Kila kitu hapa duniani kinaendeshwa na misingi ya sheria za asili, kuna kupanda na kuvuna, kuna kutoa na kupata. Usipoijua misingi hii na kuiishi, huwezi kufanikiwa.

Juma #12; A Gift to My Children: A Father’s Lessons for Life and Investing by Jim Rogers. Ili kuwa na maisha bora kabisa kwako unapaswa kujijua wewe mwenyewe kwanza na kuishi maisha ambayo ni halisi kwako badala ya kuishi maisha ya kuigiza. Usishindane wala kujilinganisha na mtu yeyote, kimbia mbio zako mwenyewe.

Juma #13; Everything I Know about Business I Learned at McDonald’s: The 7 Leadership Principles That Drive Break Out Success by Paul Facella, Adina Genn. Uaminifu na uadilifu ni msingi muhimu sana wa mafanikio kwenye biashara na maisha kwa ujumla. Ukiangalia biashara zote zilizofanikiwa na kudumu kwenye mafanikio kwa muda mrefu, utaona uadilifu na uaminifu kama msingi muhimu. Wapo wafanyabiashara wanaotumia njia zisizo za uaminifu, wanapata mafanikio lakini hayadumu kwa muda mrefu.

Juma #14; The Psychology of Selling: Increase Your Sales Faster and Easier Than You Ever Thought Possible by Brian Tracy. Kitu kimoja kinachowatofautisha wajasiriamali wenye mafanikio na wanaoshindwa ni uwezo wa kuuza, wale ambo wanaweza kuuza wanafanikiwa kuliko wasioweza kuuza. Na kadiri mtu anavyokuwa bora kwenye kuuza, ndivyo anavyoweza kupiga hatua zaidi. Watu wa mauzo ni moja ya watu wenye mafanikio makubwa sana kwa ujumla ukilinganisha na watu wengine. Hivyo kadiri unavyokuwa bora kwenye kuuza, ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi ya kufanikiwa.

Juma #15; The Healing Power of Mind: Simple Meditation Exercises for Health, Well-Being, and Enlightenment by Tulku Thondup. Tahajudi (meditation) ni zoezi rahisi ambalo linakuwezesha kuwa na afya imara ya akili na hata ya mwili. Tahajudi inatuwezesha kutumia nguvu ya akili zetu kutuliza akili, kuondoa changamoto za mwili na kuwa na furaha wakati wote.

Juma #16; Factfulness: Ten Reasons We’re Wrong About the World – and Why Things Are Better Than You Think by Hans Rosling, Ola Rosling, Anna Rosling Rönnlund. Mambo mengi tunayoyajua kuhusu dunia siyo sahihi, vyombo vya habari vimekuwa vinakuza mabaya machache kuhusu dunia, lakini ukweli ni kwamba dunia inapiga hatua na kuwa bora zaidi kila siku.

Juma #17; Skin in the Game: The Hidden Asymmetries in Daily Life by Nassim Nicholas Taleb. Chochote unachofanya kwenye maisha yako, kazi, biashara, mahusiano, imani na mengineyo, unahitaji kuwekeza kila ulichonacho kiasi kwamba ukifanya makosa unapoteza kila kitu. Na kama upo kwenye mahusiano au ushirikiano ambapo mwingine ananufaika na faida ila hasara haimgusi, ondoka haraka.

Juma #18; Perennial Seller: The Art of Making and Marketing Work That Lasts by Ryan Holiday. Chochote unachofanya, usifikirie leo, kesho au mwaka ujao, bali fikiria miaka 100 ijayo. Kwa kufikiria miaka mingi utaifanya kazi ambayo ni bora zaidi.

Juma #19; 12 Rules for Life: An Antidote to Chaos by Jordan B. Peterson. Ukizijua kanuni za maisha na kuzifuata utaepuka machafuko kwenye maisha yako na kuwa na maisha yenye mpangilio mzuri. Tunaingia kwenye matatizo mbalimbali kwa sababu hatuzijui au hatuzifuati kanuni za maisha.

Juma #20; Own the Day, Own Your Life: Optimised practices for waking, working, learning, eating, training, playing, sleeping and sex by Aubrey Marcus. Jinsi unavyoiishi siku yako moja ndivyo unavyoyaishi maisha yako yote. Kama unataka kuyadhibiti maisha yako na kuwa na maisha ya mafanikio, anza kwa kudhibiti kila siku yako, tangu unapoamka mpaka unapolala.

Juma #21; Selling You!: A Practical Guide to Achieving the Most by Becoming Your Best by Napoleon Hill. Maisha ni kuuza na wale wanaoweza kuuza vizuri, kwa kuanzia na kujiuza wao wenyewe, kuuza bidhaa au huduma zao, ndiyo wanaofanikiwa sana. jifunze kuuza na hutakuwa na maisha magumu.

Juma #22; The Million-Dollar, One-Person Business: Make Great Money. Work the Way You Like. Have the Life You Want. by Elaine Pofeldt. Maendeleo ya teknolojia yamerahisisha sana ufanyaji wa biashara. Kwa sasa unaweza kuanzisha na kukuza biashara ukiwa peke yako kwa kutumia vizuri teknolojia.

Juma #23; 13 Things Mentally Strong People Don’t Do: Take Back Your Power, Embrace Change, Face Your Fears, and Train Your Brain for Happiness and Success by Amy Morin.  Maisha ni magumu, usiyotegemea yatokee ndiyo yanayotokea na licha ya kuweka mipango mizuri, mambo yanaenda tofauti na ulivyopanga. Unapaswa kuwa na uimara wa kifikra ili kuweza kupambana na hali hizi za maisha na kuweza kufanikiwa.

Juma #24; The 22 Immutable Laws of Marketing: Violate Them at Your Own Risk by Al Ries, Jack Trout. Sheria ya 18; sheria ya mafanikio.

Mafanikio huwa yanaleta kiburi na kiburi huwa kinaleta kushindwa. Watu wanapofanikiwa huwa wanajiona wameshajua kila kitu, wanaacha kuweka juhudi walizoweka mwanzo na wanaanza kushindwa.

Haijalishi umefanikiwa kiasi gani, epuka sana kuwa na kiburi, epuka kujiona umeshajua kila siku, na kila wakati endelea kujifunza na kuchukua hatua kama vile ndiyo unaanza.

Juma #25; How to Sell Anything to Anybody by Joe Girard. Kuna vitu viwili muhimu sana unapaswa kuvipata kwenye mauzo, cha kwanza unapaswa kupata fedha, na cha pili unapaswa kupata urafiki. Sasa watu wengi huangalia cha kwanza, kupata fedha pekee na hivyo huwa tayari kufanya chochote wauze. Ila kama utamuuzia mtu kitu ambacho hakimfai, jua siyo tu umempoteza mteja huyo, bali umepoteza wateja wengine wengi. Unahitaji kutengeneza urafiki na kila mteja wako, kwa kujali hasa hitaji lake na kuhakikisha anarudi kununua kwako na anawaambia wengine kuhusu unachofanya. kama utapata fedha na ukakosa urafiki, hutadumu kwenye biashara kwa muda mrefu.

Juma #26; Marketing That Matters: 10 Practices to Profit Your Business and Change the World by Chip Conley, Eric Friedenwald-Fishman. Usiogope kuitangaza biashara yako. Masoko ndiyo msingi muhimu wa biashara yoyote ile. Kikwazo namba moja kwenye biashara yako ni wateja kutokujua kuhusu uwepo wako. Hivyo unahitaji kuitangaza biashara yako na kuhakikisha kila mteja inayemfaa anajua uwepo wa biashara hiyo. Na unapotangaza, eleza kile ambacho biashara yako inafanya, yaani wateja wananufaikaje na biashara hiyo. Ili ufanikiwe kwenye biashara, lazima uwe na mkakati mzuri wa kutangaza na kufikia soko la biashara yako.

Juma #27; Sell or Be Sold: How to Get Your Way in Business and in Life by Grant Cardone. Mauzo ndiyo njia ya maisha, mauzo ni hitaji muhimu la maisha, ili ule lazima uuze, na lazima pia watu wakuuzie kitu. Kama kuna kitu kimoja unapaswa kujifunza sana kwenye maisha yako, ni jinsi gani unaweza kuuza vizuri chochote unachouza. Kama umeajiriwa unauza muda wako na ujuzi wako pia. Kama upo kwenye biashara unauza bidhaa na huduma ulizonazo. Maisha yanaendeshwa kwa kamisheni ambazo tunazipata kwenye mauzo yetu, inategemea tu jina gani unaita, kwenye biashara utasema ni faida, kwenye kazi mshahara, kwenye mauzo ni kamisheni. Tambua, hakuna kitakachotokea kwenye maisha yako mpaka umuuzie mtu kitu. Amka sasa na anza kuuza kile unachouza kwa kuwa maisha yako yanategemea wewe kuuza.

Juma #28; The Wisdom of Life by Arthur Schopenhauer. Msaada wa nje hauwezi kumsaidia mtu yeyote ambaye ameshajiwekea ukomo ndani yake. Huwezi kujikimbia wewe mwenyewe, kama ambavyo mtu hawezi kuondoka ndani ya ngozi yake. Mabadiliko ya kweli kwenye maisha ya mtu, lazima yaanzie kwenye utu wake, lazima awe tayari kubadilika yeye mwenyewe. Ukomo wa mtu kwenye maisha, ni ule ambao amejiwekea wewe mwenyewe. Hebu jiangalie ni vitu hani umewahi kukosa kwenye maisha yako na ona kama hakuna ukomo umekuwa unajiwekea wewe mwenyewe.

Juma #29; The Power of Relentless: 7 Secrets to Achieving Mega-Success, Financial Freedom, and the Life of Your Dreams by Wayne Allyn Root. Bila ya kuwa mbishi hutaweza kufanikiwa kwenye haya maisha, unapaswa kuwa mbishi na mgumu ili kufanikiwa. Kwenye safari ya mafanikio utakutana na kikwazo cha kila aina, ubishi wako ndiyo utakaokuwezesha kuvuka vikwazo hivi na kupata kile unachotaka.

Juma #30; Spiritual Solutions: Answers to Life’s Greatest Challenges by Deepak Chopra. Kila changamoto tunayokutana nayo kwenye maisha, suluhisho lake linaanzia ndani yetu, na linaanzia kwenye imani yetu. Unapoangalia kila kitu kwenye maisha yako, kama ukiwa muwazi kabisa, kama utaondoa kutafuta sababu, utaona jinsi ambavyo wewe mwenyewe umechangia kwenye tatizo uliloingia na suluhisho lake linaanzia ndani yako.

Juma #31; Blur: How to Know What’s True in the Age of Information Overload by Bill Kovach, Tom Rosenstiel. Tunaishi kwenye zama za mapinduzi ya taarifa, hakuna tena mwenye uwezo wa kumiliki taarifa au kuzuia watu wasipate taarifa fulani. Kwa sababu kila mtu anayo nguvu ya kusambaza na kupokea taarifa yoyote. Japo hili linakuwa faida kwa walaji wa taarifa, lakini pia linakuja na hatari moja, ni vigumu sana kujua usahihi wa taarifa unazopata hasa kwenye mtandao. Watu wengi wamefanya maamuzi kwa taarifa zisizo sahihi kitu ambacho kimewagharimu sana.

Juma #32; Mindfulness in Plain English by Henepola Gunaratana. Tahajudi inatusaidia kuweza kudhibiti akili na mawazo yetu, kuweza kuweka umakini kwenye chochote tunachofanya na kuacha kuendeshwa kwa hisia na matukio na badala yake kuwa na utulivu kwenye chochote ambacho mtu umechagua kufanya.

Juma #33; Your First 100 Million by Daniel S. Peña. Mafanikio makubwa siyo kwa watu laini laini. Dunia ya sasa watu wamekuwa laini sana. Wanataka mafanikio makubwa na wakati huo huo wanataka wamfurahishe kila mtu kwenye maisha. Hicho ni kitu ambacho hakiwezi kutokea kwa namna yoyote ile. Kwenye mafanikio makubwa hakuna urafiki, na kama unatafuta rafiki nunua mbwa, maana hao ndiyo rafiki wazuri, wengine mtasumbuana sana inapokuja kwenye mafanikio makubwa.

Juma #34; Mastery: The Keys to Success and Long-Term Fulfillment by George Leonard. Ili uweze kufikia mafanikio makubwa na ya kudumu kwenye maisha yako, unapaswa kuwa na ubobezi kwenye eneo fulani. Na ili kufikia ubobezi unahitaji vitu viwili, muda na kuweka kazi.

Juma #35; Rework by Jason Fried, David Heinemeier Hansson. Siyo lazima kila biashara iwe na matawi ndiyo ionekane kufanikiwa. Mfano chuo kikuu cha Havard ni chuo kikubwa na chenye mafanikio makubwa sana duniani, lakini kipo kimoja tu. Ingekuwa rahisi kusema wangeweza kufungua matawi dunia nzima, lakini hiyo siyo njia sahihi kwao kupima mafanikio.

Juma #36; The Perfect Day Formula: How to Own the Day and Control Your Life by Craig Ballantyne. Kanuni ya siku ya mafanikio imejengwa kwenye misingi mikuu mitatu; moja, KUDHIBITI yale yaliyo ndani ya uwezo wako na kupokea yale ambayo huwezi kuyadhibiti. Ili kuwa na siku ya mafanikio, unahitaji kuwa na udhibiti mkubwa kwenye ASUBUHI YAKO.

Msingi wa pili ni KUSHINDA kelele na usumbufu wa kila siku ili kuweza kufanya yale muhimu. Ili kuwa na siku ya mafanikio, unahitaji kushinda kelele na usumbufu kwenye MCHANA WAKO.

Msingi wa tatu ni UMAKINI. Hapa unahitaji kuweka umakini kwenye yale ya muhimu zaidi kwako na kupuuza mengine ambayo siyo muhimu. Ili kuwa na siku ya mafanikio, unahitaji kuweka umakini kwenye yale yaliyo muhimu sana kwenye JIONI YAKO.

Juma #37; Buying Customers by Bradley J. Sugars. Ili biashara yako iweze kukua lazima uwekeze fedha kwenye kupata wateja wa biashara hiyo. Bila ya kuwekeza fedha kupata wateja, biashara yako haitajulikana na hili litapelekea biashara hiyo kufa.

Juma #38; How to Run a Country: An Ancient Guide for Modern Leaders by Marcus Tullius Cicero, Philip Freeman. Ili kuwa kiongozi mzuri, unapaswa kufuata sheria za asili. Sehemu ya sheria hizo za asili ni kwamba watu wote ni sawa, kila mtu anastahili kupata haki, kila mtu ana uhuru wa kuishi na kufanya maamuzi yake, na pia kila mtu anayo haki ya kuwa na furaha kwenye maisha yake. Kama kiongozi, lazima uhakikishe watu wako wana uhuru huo wa maisha, tofauti na hapo uongozi utakuwa mgumu.

Juma #39; This Is Going to Hurt: Secret Diaries of a Junior Doctor by Adam Kay. Kuchagua kazi yoyote ila kwa kigezo cha kipato ni kujiandaa kuumia, kwa sababu kazi nyingi hazitakupa kipato kinachoendana na juhudi unazopaswa kuweka kwenye kazi hiyo. Hivyo kitu cha kwanza unachopaswa kutumia kufanya maamuzi ya kazi ni mapenzi na kujali. Ikiwa unafanya kile unachopenda, na unakijali kwa sababu kina maana kwako, hata kama hutapata fedha nyingi kwa haraka, utakuwa na maisha bora na baadaye kipato chako kitakuwa kizuri.

Juma #40; Stoic Week 2018 Handbook. Ustoa ni falsafa ya matendo, ni falsafa ambayo imelenga kumwezesha mtu kuwa na maisha bora, kwa kufikiri sahihi na kuchukua hatua sahihi kwenye maisha yake. Falsafa ya ustoa siyo kama falsafa nyingine za kubishana na kutaka kuonekana unajua zaidi, badala yake ni falsafa ya kufikiri sahihi na kuchukua hatua sahihi. Falsafa ya ustoa inalenga kudhibiti hisia zetu na kuishi kulingana na asili. Kwa njia hiyo, tunakuwa na maisha bora wakati wote.

Juma #41; The Go-Giver: A Little Story About a Powerful Business Idea by Bob Burg, John David Mann. Zipo kanuni kuu tano za kukuwezesha kupata mafanikio makubwa sana, kutoa thamani kubwa, kuwahudumia wengi zaidi, kuweka mbele maslahi ya wengine, kuishi maisha ya uhalisia wako na kuwa tayari kupokea.

Juma #42; The Art of the Good Life by Rolf Dobelli. Inapokuja upande wa fedha, kuwa na kiasi cha fedha kitakachokuwezesha kuendesha maisha yako bila ya kutegemea kipato cha moja kwa moja, usijilinganishe na yeyote kifedha na hata kama una fedha nyingi kiasi gani, ishi maisha ya kawaida, utajiri hujenga wivu.

Juma #43; Charlie Munger: The Complete Investor by Tren Griffin. Charlie Munger ni mmoja wa watu ambao wamejenga msingi wao wameujenga kwenye maarifa na hekima. Munger anaamini sana katika kujifunza, siyo tu kwenye lile eneo ambalo mtu unafanyia kazi, bali kwenye maeneo mengine pia.

Munger ana mfumo wake anaouita MENTAL MODELS, ambapo anasema ili kuweza kufanya maamuzi sahihi, lazima uweze kufikiri kwa mifumo mbalimbali. Lazima uweze kutumia mifumo tofauti na kile unachofanyia kazi. Kwa mfano kwenye uwekezaji, lazima uweze kufikiria kama mwanahisabati, mwanafizikia, mwanasaikolojia, mwanahistoria, mwanabaiolojia na mwanafalsafa.

Juma #44; Winning the Loser’s Game: Timeless Strategies for Successful Investing by Charles D. Ellis. Njia ya uhakika ya kufanikiwa kwenye uwekezaji siyo kukazana kulishinda soko, bali kuwekeza kwa muda mrefu, ukiamini kwamba ndani ya muda mrefu, soko litakuwa na kuzalisha thamani. Data zimekuwa zinaonesha kwamba kwa miaka mingi, licha ya kupanda na kushuka kwa soko la hisa, kwa wastani soko limekuwa linapanda kwa silimia 10. Hivyo kama mtu atawekeza kwa muda mrefu, ataibuka mshindi na hatakuwa na tatizo la kuhangaika na mabadiliko ya muda mfupi kwenye soko.

Juma #45; The Boron Letters by Gary Halbert, Bond Halbert. Ili kuwa na afya bora, fanya mazoezi kila siku, hasa kukimbia, funga siku moja kwa wiki na kula chakula bora.

Juma #46; The Great Game of Business: Unlocking the Power and Profitability of Open-Book Management by Jack Stack, Bo Burlingham. Njia bora ya kuendesha biashara ni kuwa na uwazi, kwa kila aliye kwenye biashara, hasa waajiriwa kujua kila kitu kinachoendelea kwenye biashara. Kujua kiasi cha mtaji, mauzo, gharama za uendeshaji na hata faida. Makampuni mengi yamekuwa yanafanya taarifa hizi kuwa siri, lakini usiri huu ndiyo unapelekea makampuni mengi kufa.

Juma #47; 151 Quick Ideas to Increase Sales by Linda Sparks. Zipo njia nyingi za kuwafikia wateja wa biashara yako, tumia nyingi uwezavyo na usitegemee moja au chache pekee. Njia unazoweza kutumia; matangazo, maonesho ya kibiashara, taarifa kwa uma, tovuti, mauzo ya moja kwa moja, uandishi na mafunzo mbalimbali.

Juma #48; The Art of Money Getting: Golden Rules for Making Money by P.T. Barnum. Njia ya kuelekea kwenye utajiri iko wazi kama njia ya kuelekea kisimani. Fursa zipo nyingi na kwenye kila sekta kwa yeyote anayetaka kupata fedha. Kwa kuijua na kuifuata misingi ya kupata mafanikio na utajiri, kila mtu anaweza kutengeneza utajiri mkubwa kwenye maisha yake.

Juma #49; The Attractor Factor: 5 Easy Steps for Creating Wealth (or Anything Else) from the Inside Out by Joe Vitale. Sheria ya mvutano inasema kwamba chochote kinachotokea kwenye maisha hakiji kama ajali, badala yake kimevutwa. Hii ina maana kwamba, chochote ambacho kimewahi kutokea kwenye maisha yako na kila kitakachoendelea kutokea, hakiji kama ajali au bahati mbaya, bali ni wewe mwenyewe umevutia hicho kilichotokea. Wewe ndiye umekikaribisha na kukiruhusu kitokee.

Juma #50; The Daily Entrepreneur: 33 Success Habits for Small Business Owners, Freelancers and Aspiring 9-to-5 Escape Artists by S.J. Scott, Rebecca Livermore. Kanuni kuu ya mafanikio kwenye ujasiriamali ni kuanzia sokoni, wengi huanza kufanya kitu kwa mapenzi yao wenyewe na siyo mapenzi ya soko. Kama unataka kufanikiwa, anza kujua watu wanataka nini kisha wape hicho wanachotaka.

Rafiki yangu mpendwa, hivyo ndivyo vitabu 50 ambavyo nilikushirikisha kwenye kitabu cha TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA. Pata muda wa kupitia kusoma vitabu hivi na utaweza kuyaboresha maisha yako.

JINSI YA KUPATA KITABU CHA TANO ZA JUMA.

Kitabu cha TANO ZA MAJUKA 50 YA MWAKA kimechapwa na kinapatikana kwa kuletewa pale ulipo (kama upo dar) au kusafirishiwa kama upo mkoani.

Kitabu hiki kinapatikana kwa uwekezaji wa tsh elfu 50 (50,000/=), lakini kwa sasa kuna ofa ya kukipata kwa shilingi elfu 40 (40,000) na ofa hii itaisha kabla ya tarehe 01/08/2019.

Jipatie kitabu chako leo ili uweze kujifunza siri za mafanikio, upate uchambuzi huo wa vitabu vya mafanikio na mafunzo mengine muhimu kwa mafanikio yako.

Kupata kitabu piga simu au tuma ujumbe kwenye namba 0717 396 253 au 0755 953 887 kisha utapewa maelekezo ya kukipata kitabu.

JINSI YA KUPATA VITABU 50 VILIVYOCHAMBULIZA BURE.

Vitabu vyote 50 vilivyoorodheshwa hapa unaweza kuvipata kwa mfumo wa nakala tete ukijiunga na programu ya TANO ZA JUMA ambayo inaendeshwa kupitia mtandao wa Telegram.

Ukinunua kitabu cha TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA unapata nafasi ya kuunganishwa kwenye channel hiyo ya TELEGRAM na hivyo utaweza kupakua vitabu vyote hivyo 50 bure kabisa.

Ukishanunua kitabu, tuma ujumbe kwa telegram kwenda namba 0717396253 wenye maneno TANO ZA JUMA utaunganishwa kwenye programu hiyo na kuweza kupakua vitabu vyote 50 kwa ajili ya kujisomea zaidi.

KARIBU KWENYE UZINDUZI WA VITABU.

Rafiki, jumamosi ya tarehe 03/08/2019 tutakuwa na uzinduzi wa vitabu viwili nilivyotoa ambavyo ni ELIMU YA MSINGI YA FEHA na TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA.

Uzinduzi huu utafanyika GOLDEN PARK HOTEL sinza, kuanzia saa 8 mchana mpaka saa 12 jioni.

Ili kushiriki uzinduzi huu, ambapo utajifunza mengi kuhusu vitabu, unapaswa kujiwekea nafasi kwa kutuma ujumbe kwenda namba 0717396253 wenye majina yako kamili na namba ya simu na maelezo kwamba utashiriki uzinduzi wa vitabu.

Ada ya kushiriki uzinduzi huu ni tsh elfu 10 (10,000/=) na unapaswa kuilipa kabla ya tarehe 01/08/2019.

Usikose uzinduzi huu, kwani utajifunza mengi sana kuhusu usomaji wa vitabu na mafanikio kwa ujumla. Tuma sasa ujumbe wa kushiriki ili ujiwekee nafasi yako.

Karibu sana.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge