Maisha ni magumu, ila huwa tunachagua kuyafanya kuwa magumu zaidi ya yanavyostahili.
Kuyarahisisha maisha yako kwa mwaka 2020, fanya mambo haya 20.
- Jiwekee lengo moja kubwa ambalo utalifanyia kazi kila siku kwa mwaka mzima.
- Ongeza kipato chako kwa angalau asilimia 20 ya kipato cha mwaka 2019.
- Kila siku kazana kuwa bora zaidi ya jana, shindana na wewe mwenyewe na siyo mtu mwingine.
- Kwenye kila kipato unachoingiza, tenga asilimia 10 na weka pembeni kabla hujaana kutumia.
- Asilimia 10 unayoiweka pembeni, iwekeze sehemu ambayo inazalisha zaidi.
- Soma kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, kupata mwongozo sahihi kufikia uhuru wa kifedha. Kupata vitabu piga simu 0678 977 007.
- Punguza sana au acha kabisa kutumia mitandao ya kijamii kama haikuingizii kipato.
- Usianze siku yako kwa kufuatilia habari.
- Soma angalau kurasa 10 za kitabu kila siku.
- Amka mapema zaidi ya ulivyozoea, angalau saa moja na tumia muda huo kusali/kutahajudi, kujisomea na kufanya mazoezi.
- Pangilia siku yako kabla hujaianza, tafakari siku yako kabla hujaimaliza.
- Weka muda kwenye kujenga mahusiano yako, hasa ya wale wa karibu.
- Weka juhudi zaidi kwenye kazi/biashara, nenda hatua ua ziada kwa kila unachofanya.
- Usitoe ushauri kwa mtu ambaye hajakuomba, usichukue ushauri kwa ambaye hujamwomba.
- Usijisumbue kuwabadilisha watu, watu huwa hawabadilishwi.
- Shukuru kwa kila jambo, pokea kila hali unayokutana nayo na igeuze kuwa bora.
- Usilalamike wala kumlaumu yeyote kwa chochote, beba jukumu la maisha yako.
- Fanya kilicho sahihi mara zote na siyo kilicho rahisi.
- Jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA na upate vitabu na chambuzi zake mwaka mzima. Kujiunga fungua; https://www.t.me/somavitabutanzania
- Ianze kila siku yako kwa maarifa na hamasa kutoka AMKA MTANZANIA, fungua; https://amkamtanzania.com
Ni hayo 20 rafiki, fanya hayo kila siku kwa siku 366 za mwaka 2020 na utakuwa mwaka bora sana kwako.
Kumbuka nipo na wewe kwenye safari hii ya mafanikio.
Rafiki na Kocha wako,
Dr Makirita Amani.
OMBI; Tafadhali sambaza ujumbe huu kwa wengine ili nao waweze kuwa na mwaka bora 2020.